Tanzania yaongoza Afrika kwa kuwa na asilimia chache ya raia wake ambao ni diaspora

Tanzania yaongoza Afrika kwa kuwa na asilimia chache ya raia wake ambao ni diaspora

Wakoloni weusi wanapenda tuendelee kubakia hapa tusipate akili ili waendelee kutuburuza.

Ila watoto wao wanawapeleka nje kusoma na wao wanakwenda kutibiwa na kufanya shoping.
Mkoloni wetu ni Elimu mbovu, Umasikini,CCM
 
Dada wa kazi tu wanawazuia kwenda kutafuta maisha nje kisa wivu tu ili wengi wabakie masikini nchini.
Dada wa kazi omani anakula mshahara mkubwa kuliko msomi wa masters mwajiriwa wa Serikali.
Ni kweli!

Namfahamu mtu mmoja aliyekuwa dereva kwenye taasisi moja hapa Tanzania niliyokuwa nikiifanyia kazi. Mke wake alikuwa anafanya kazi za ndani Omani. Japo alikuwa ni dereva ti, alikuwa na simu "kali" kuizidi yangu ingawa nilikuwa bosi wake. Alinieleza alivyoipata simu ya gharama kuzidi mshahara wake. Alitumiwa na mke wake aliyekuwa akifanya kazi za ndani Omani.

Rafiki yangu tuliyemaliza naye Chuo, alikataa kuajiriwa Tanzania baada ya kuhitimu. Alienda Dubai akawa akifanya kazi ambayo kwa huku Tanzania isingeonekana kama ina hadhi kivile, hasa kwa mtu mwenye degree. Lakini baada ya miaka kadhaa, alirejea Tanzania kuwekeza alichokichuma Uarabuni. Uchumi wake ulionekana bora kuzidi wa wenzake wengi aliomaliza nao chuo.
 
Hiyo inaweza ikawa ni sababu mojawapo lakini si kubwa kama inayosababishwa na Serikali.

Passport! Kwa namna tu inavyobana passport, ni rahisi watu wengi kutokufikiria kutoka nje ya mipaka yao.

Serikali inahusika pakubwa sana na hayo.
Huwezi taka toka nje ukakwama kisa passport ambayo ukinyoosha shati waipata ndani ya masaa 24
 
Ndo maana watu waliambiwa Kamala Harris anakuja kuwalazimisha waingiliane wanaume Kwa wanaume wakaandaa Hadi maandamano... little exposure ni ugonjwa mbaya Sana..
Hadi maandamano ya kupinga Dpworld kisa Wengi wanaamini waarabu wanakuja kueneza dini...
Ongeza na kuua Albino na wazee wenye macho mekundu
Watanzania bado tuna ujinga kichwani.

Leo hii ukiwauliza wanaopinga DPW wakueleze jinsi gani watawekeza pale bandarini hawana jawabu la msingi.

Walianza kwa kusema Miaka 100, wamehamisha magoli sasa wanasema Mkataba hauko sawa
 
Kenya nje kitambo sana hakuna nchi haina Mkenya anabeba box Duniani nenda hata Cyprus, Malta,Kiribati, Chechnya,nk kwa mwaka wanatuma pesa nyingi sana nyumbani kuboost uchumi wa Kenya.
Wakenya wanajiongeza na lugha inawasaidia
 
Sababu kubwa ni kuwa Tanzania bado haijaharibika kisiasa, kiuchumi na ubora wa maisha kila mwananchi. Nchini Tanzania hata mwananchi wa kipato cha chini anaweza miliki ardhi. Huko vijijini wananchi kibao wanamiliki ardhi kubwa zenye rutuba. Hali ya hewa ya Tanzania ni ya kipekee sana. Pia majanga ya kiasili sio mengi. Na idadi yetu ni kubwa kiasi kwamba mfanyabiashara smart hawezi kuhama hii nchi kutafuta soko kwingine. Kimsingi Tanzania ni sehemu salama kabisa kuishi.

Sababu nyingine isiyosemwa ni uwepo wa CCM kwenye kuongoza nchi. Uongozi imara wa kidemokrasia chini ya chama pendwa CCM unafanya wananchi wasitake kabisa kutoka nje ya nchi hii. Chini ya mwenyekiti wa CCM Mheshimiwa Samia Suluhu tumeona jinsi watanzania waliokuwa nje ya nchi wakizidi kurudi nyumbani.
 
I'm proud of my country,japo hatupo exposed na hatuna elimu sana ila hua nakubaliana kua most of the times ignorance is bliss. Ujinga wetu ni faida sana kwetu.

Watanzania ni watu flani hivi maskini jeuri and I proud of that. Japo hatuna pesa ila hatushoboki Kwa watu,pia hatupendi kulia Lia njaa.
Hatushoboki au ugumu wa kwenda hizo nchi za watu tunaowekewa na waTanzania wenzetu ndo unafanya tutulize fuvu?
 
Huwezi taka toka nje ukakwama kisa passport ambayo ukinyoosha shati waipata ndani ya masaa 24
Ndiyo, ukinyoosha shati, karibia kila kitu kinawezekana Tanzania.

Lakini ujue kuna watu dhamiri zao haziwaruhusu kufanya hivyo.

Tanzania, ikiwa utakuwa tayari kunyoosha shati, unaweza kubeba abiria kwa basi lisilo na breki toka Mwanza hadi Dar Es Salaam, na njiani Trafiki wakaishia tu kukushauri kuwa uendeshe kwa umakini.

Ndiyo, ukinyoosha shati...
 
Back
Top Bottom