Tanzania yaongoza Afrika kwa kuwa na asilimia chache ya raia wake ambao ni diaspora

Tanzania yaongoza Afrika kwa kuwa na asilimia chache ya raia wake ambao ni diaspora

Ningependekeza kila anayemaliza form six (21) aende nje hata kwa miezi sita, mwaka mmoja kwa kudhaminiwa na serikali / vyuo.

Ingesaidia sana kuongeza exposure. Miaka 16 kila Mtanzania apewe passport, NIDA, kitambulisho cha kupiga kura.
👏👏👏🙏🙏🙏
Vichwa vya sampuli hii ndivyo vilipaswa kuongoza nchi.
 
Shangaa serikali Yako.

Inatia ugumu upatikanaji wa passport ila kwenye mikataba fasta inatia Saini bila hata kufikiria.

Passport tu yaweza ongeza Pato kwa serikali just imagine raia milioni 15 waziombe na kupewa so Hela ndefu hio.
Viongozi wengi hawana fikra za kijasiriamali. Kutoa passport ni faida kwa Serikali na wananchi.
 
I'm proud of my country,japo hatupo exposed na hatuna elimu sana ila hua nakubaliana kua most of the times ignorance is bliss. Ujinga wetu ni faida sana kwetu.

Watanzania ni watu flani hivi maskini jeuri and I proud of that. Japo hatuna pesa ila hatushoboki Kwa watu,pia hatupendi kulia Lia njaa.
Umasikini sio sifa mkuu tupambane tuuondoe
 
I'm proud of my country,japo hatupo exposed na hatuna elimu sana ila hua nakubaliana kua most of the times ignorance is bliss. Ujinga wetu ni faida sana kwetu.

Watanzania ni watu flani hivi maskini jeuri and I proud of that. Japo hatuna pesa ila hatushoboki Kwa watu,pia hatupendi kulia Lia njaa.
Hivi kwanini watanzania tunapenda kujidharau? Si kweli kwamba hatuna elimu. Elimu ya Tanzania inazidi nchi nyingi saana za hapa Africa. Hata kimataifa elimu ya Tanzania inakubalika na wakati mwingine kuna nchi zenye diaspora wengi lkn elimu za nchi zao hazikubaliki nje.

Mfano, Somalia inaongoza kwa kuwa na Diaspora wengi, kuna nchi kama Eritrea na Ethiopia uwezi linganisha elimu zao na Tanzania.
Swala la Diaspora limetokana na ugumu wa maisha ktk nchi nyingi za Africa na vita. Mfano Nigeria japo kuwa na uchumi mzuri lkn kunamaisha magumu saana kiasi vijana wengi ukimbia nchi kutafuta maisha.

Hapo hapo Nigeria ukiuliza kabila la fulani uwa awakimbii nchi wengi wapo Nigeria wakila maisha. Ni kabila lililo na utajiri mkubwa, na mamilionea wengi utoka katika kabila hili. Wao wanaenda tu nje kutembea na kurudi kwao.

Kenya tu hapa wakikuyu wengi ni matajiri na wafanya biashara si wengi wao wanao kimbilia nje, ni makabila yale mfano Wakisii, wakamba, waruya na wengineo.

Tanzania maisha si magumu ya kiasi cha kumfanya mtu akimbie nchi. Na watanzania wanapenda nchi yao. Kwa sababu hata wakienda nje si wakubabaika sana. kama ulivyosema wabongo uwa tunajeuri. Tunapima maisha, tunapigana kutafuta fursa hapa hapa nchini.

Kwa maisha ya nje nenda nje kama kweli umeshindwa pata fursa Tanzania, ila kuna vijana wengi Tanzania wana win na kuwa na maisha mazuri kuliko nje.

Huko nje mshahara unaishia kwenye kodi ya nyumba, chakula na mafuta ya gari. Ulaya biashara ni ngumu sana. Watu ukaa miaka 10 hadi 20 lakini wanarudi Tanzania hawana kitu.

Vijana wengi wa Tanzania wametajirika wakiwa hapahapa Bongo kuliko hao walio toka kuishi ughaibuni.

Mbona wabongo wengi wanasafiri nje na kurudi Tanzania, hivyo exposure wabongo wanayo.

Wabongo tumetulia tu na mama yetu Samia. Si unaona marais wengine wanahangaika kujigonga kwa wazungu waonekane, ha ha ha! Kama Ruto...Lakini mama yeye katulia tuli hana haraka.
Hii ndo Tanzania na watanzania! Hatubabahiki!
 
Yote haya yalisababishwa na Nyerere alizuia watu kutoka nje ya nchi ili kuepuka watu kuwa na mawazo tofaut na yake
 
Dada wa kazi tu wanawazuia kwenda kutafuta maisha nje kisa wivu tu ili wengi wabakie masikini nchini.
Dada wa kazi omani anakula mshahara mkubwa kuliko msomi wa masters mwajiriwa wa Serikali.
 
Watz wengi kwa akili zetu fupi tunafikiri kuwa na diaspora wengi ndio mafanikio.

Ni kweli kuna changamoto katika taratibu za kutoka nje. Pia kuna shida na tabu nyingi ndani ya nchi hii, zikichangiwa zaidi na mfumo wetu wa kiutawala.

But all in all, we should thank God a thousand times for the way we are. Ukitaka kuelewa kidogo tu Tz tulivyo safi vuka border hapo Sirari uone maisha yalivyo tofauti kule utakakoingia, hata salamu utatamani uinunue.

Kuna watu humu juzikati nimeshangaa kuona wakiwasifia Somalia kwa kuwa na diaspora wengi, huku wakiwish nasi tuwe kama Somalia! Wonderful!
Nakukatalia,waache ujinga kubana passport watu tuzurure duniani
 
Kenya nje kitambo sana hakuna nchi haina Mkenya anabeba box Duniani nenda hata Cyprus, Malta,Kiribati, Chechnya,nk kwa mwaka wanatuma pesa nyingi sana nyumbani kuboost uchumi wa Kenya.
 
World Bank wametoa report inayoitwa 'Ratio of persons living abroad to origin country population' ambapo kwenye report hiyo Tanzania inapungufu ya asilimia moja ya raia wake wanaishi nje ya nchi.

View attachment 2667693

Asilimia hizo ni chache kuliko mataifa yote ya nchi za Africa.

Mind you, Tanzania ni nchi pekee yenye wazungumzaji wengi wa Kiswahili.

Je, huu uthibitisho kwamba Kiswahili hakivuki maji? Au ni kwamba watanzania wengi wana mapenzi na nchi yao?
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
 
Ukweli ni kuwa watz wengi hawaongei kiingereza fasaha sababu ya kusoma kwa Kiswahili. Nje kuna fursa nyingi tunazikosa na lugha inayotumika zaidi duniani ni English. Watawala wengi Wana roho mbaya hawataki watz kwenda kunufaika nje! Nchi inakosa remittance na kubaki maskini.
Solution ni kubadili lugha ya kufundishia kutoka Kiswahili kuwa English.
Watz wanapenda kwenda nje hasa vijana wasio na ajira ila Njia zote zimefungwa!
Aseeee? Somalia na Eritrea wanaongea Lugha gani?
 
Na nchi zinazoongoza ni zile zenye machafuko......
Middle east na ukanda wa Red sea, ndio zinaongoza hapo.
Unataka watanzania waondoke wanakimbia nini?
Kuliko kupoteza mda kutembeza bahasha bongo au kuwa bodaboda au machinga upate TB si Bora ukapate exposure nje
 
World Bank wametoa report inayoitwa 'Ratio of persons living abroad to origin country population' ambapo kwenye report hiyo Tanzania inapungufu ya asilimia moja ya raia wake wanaishi nje ya nchi.

View attachment 2667693

Asilimia hizo ni chache kuliko mataifa yote ya nchi za Africa.

Mind you, Tanzania ni nchi pekee yenye wazungumzaji wengi wa Kiswahili.

Je, huu uthibitisho kwamba Kiswahili hakivuki maji? Au ni kwamba watanzania wengi wana mapenzi na nchi yao?
Watanzania waoga sana, akili za kijamaa zimedumaza sana akili...leo hii Watanzania wanaamini Rwanda na Burundi bado kuna vita kwa hiyo hawathubutu kusafiri kutafuta fursa za biashara huko wakati Wakenya wamejazana huko wanapiga hela tu
 
Watanzania waoga sana, akili za kijamaa zimedumaza sana akili...leo hii Watanzania wanaamini Rwanda na Burundi bado kuna vita kwa hiyo hawathubutu kusafiri kutafuta fursa za biashara huko wakati Wakenya wamejazana huko wanapiga hela tu
We umeenda kupiga hela mkuu?
Mnalazimisha vitu ambavyo havipo.
 
Roho mbaya ya utawala ndo kisa.
Passport tu kuipata mpaka uulizwe tupe letter mfano ya chuo unachoenda. Na chuo unachoomba hawakupi letter wanataka uwape passport number ili waandike letter. Sasa wangapi watatoka?

Chuo wanakuomba maombi yako ili wayafikirie wanataka barua ya TCU kwamba una qualify kusoma hicho ulichoomba, unakimbia TCU kuwaomba barua, wao TCU wanakwambia ili wakuandikie wanataka admission letter ya hicho chuo.
Hizo sababu zako hazina msingi, ni visingizio tu
 
Back
Top Bottom