I'm proud of my country,japo hatupo exposed na hatuna elimu sana ila hua nakubaliana kua most of the times ignorance is bliss. Ujinga wetu ni faida sana kwetu.
Watanzania ni watu flani hivi maskini jeuri and I proud of that. Japo hatuna pesa ila hatushoboki Kwa watu,pia hatupendi kulia Lia njaa.
Hivi kwanini watanzania tunapenda kujidharau? Si kweli kwamba hatuna elimu. Elimu ya Tanzania inazidi nchi nyingi saana za hapa Africa. Hata kimataifa elimu ya Tanzania inakubalika na wakati mwingine kuna nchi zenye diaspora wengi lkn elimu za nchi zao hazikubaliki nje.
Mfano, Somalia inaongoza kwa kuwa na Diaspora wengi, kuna nchi kama Eritrea na Ethiopia uwezi linganisha elimu zao na Tanzania.
Swala la Diaspora limetokana na ugumu wa maisha ktk nchi nyingi za Africa na vita. Mfano Nigeria japo kuwa na uchumi mzuri lkn kunamaisha magumu saana kiasi vijana wengi ukimbia nchi kutafuta maisha.
Hapo hapo Nigeria ukiuliza kabila la fulani uwa awakimbii nchi wengi wapo Nigeria wakila maisha. Ni kabila lililo na utajiri mkubwa, na mamilionea wengi utoka katika kabila hili. Wao wanaenda tu nje kutembea na kurudi kwao.
Kenya tu hapa wakikuyu wengi ni matajiri na wafanya biashara si wengi wao wanao kimbilia nje, ni makabila yale mfano Wakisii, wakamba, waruya na wengineo.
Tanzania maisha si magumu ya kiasi cha kumfanya mtu akimbie nchi. Na watanzania wanapenda nchi yao. Kwa sababu hata wakienda nje si wakubabaika sana. kama ulivyosema wabongo uwa tunajeuri. Tunapima maisha, tunapigana kutafuta fursa hapa hapa nchini.
Kwa maisha ya nje nenda nje kama kweli umeshindwa pata fursa Tanzania, ila kuna vijana wengi Tanzania wana win na kuwa na maisha mazuri kuliko nje.
Huko nje mshahara unaishia kwenye kodi ya nyumba, chakula na mafuta ya gari. Ulaya biashara ni ngumu sana. Watu ukaa miaka 10 hadi 20 lakini wanarudi Tanzania hawana kitu.
Vijana wengi wa Tanzania wametajirika wakiwa hapahapa Bongo kuliko hao walio toka kuishi ughaibuni.
Mbona wabongo wengi wanasafiri nje na kurudi Tanzania, hivyo exposure wabongo wanayo.
Wabongo tumetulia tu na mama yetu Samia. Si unaona marais wengine wanahangaika kujigonga kwa wazungu waonekane, ha ha ha! Kama Ruto...Lakini mama yeye katulia tuli hana haraka.
Hii ndo Tanzania na watanzania! Hatubabahiki!