Muccigang
JF-Expert Member
- Apr 9, 2022
- 1,313
- 1,918
Deni la taifa limeongezeka for almost 15T within a year.View attachment 2241219
Mama anaupiga mwingi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Deni la taifa limeongezeka for almost 15T within a year.View attachment 2241219
Baada ya serikali kupata huu mkopo tuwe tunaambiwa kabisa kuwa tumefikia deni kiasi gani hadi hapo?Maana imezoeleka hapa kwetu,mikopo inageuzwa kuwa mapato ya ndani na mapato ya ndani yanakuwa kwa akili ya kuinufaisha CCM na serikali zake.Haiwezekani miradi iliyotekelezwa kwa fedha za mikopo tuambiwe ni CCM imetekeleza kwa sababu kukopa siyo ilani wala umahiri.Unakopa kwa sababu huna mbinu nyingine/as the last option.Benki ya Dunia imeipa Serikali ya Tanzania trilioni 1.2 kwaajili ya tabia nchi, barabara na viwanja vya ndege.
Nadhani sasa ni muda wa kuondoa tozo au kuambiwa siku ya ukomo.
Kiuchumi mkopo unakwenda kusisimua mzunguko wa fedha hasa kama sehemu kubwa ya hizi tenda yatapewa makampuni ya hapa nchini, pesa zitatembelea mifuko ya wananchi na shughuli za uzalishaji zitaongezeka kupokea pesa za wananchi hawa. Hasara yake, tunaandika deni jipya katika madeni ya Serikali.
======
Tanzania imepokea mkopo wa masharti nafuu wa Sh1.2 trilioni utakaofungua milango ya kuboresha usalama, ustahimilivu wa tabianchi, uwezo wa barabara za ndani na viwanja vya ndege vya Mikoa.
Taarifa iliyotolewa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Benki ya Dunia (IDA) leo Mei 27, imesema mkopo huo utaiwezesha Tanzania kufanikisha maeneo hayo chini ya Mradi wa Ushirikiano wa Usafiri Tanzania (TanTIP) utakaowezesha pia taasisi husika katika kupanga na kusimamia sekta hiyo.
Imesema ufadhili huo utasaidia uboreshaji na ukarabati wa barabara zenye urefu wa kilomita 500, zikiwemo za Mtwara-Mingoyo-Masasi (kilomita 201), Lusahunga-Rusumo (kilomita 92), Songea-Rutukila (kilomita 111) na Iringa-Msembe (kilomita 104), huku ikishughulikia hali ya hewa ili kuongeza ustahimilivu wa barabara.
Benki ya Dunia imeipa Serikali ya Tanzania trilioni 1.2 kwaajili ya tabia nchi, barabara na viwanja vya ndege.
Hapana ila tumepata mikopo ya kufidia na kuzidi,hivyo vijisenti ndiyo mnaulizia leo?Hivi zile trillion 1.5 za CAG ziliwahi kujulikana zilipo?
duh jamaa husahau tu!! ile imeisha mkuu! tugange yajayo!Hivi zile trillion 1.5 za CAG ziliwahi kujulikana zilipo?
Aliiona msoga? We Huoni DSM to msoga full Lami.Safi sana Mama Samia. Muangalie na mkoa wa Pwani.
Barabara ya Kisarawe inahitaji lami lakini pia barabara ya kuunganisha makao makuu ya mkoa - Kibaha na wilaya zake hakuna.
Ajabu Jakaya hakuliona hili licha ya kutoka mkoa husika.
Tutawapa bilion 400 tu.Trilioni 1.2 kutoka Benki ya Dunia Pemba na Unguja wanapewa ngapi?
Mzee wa kongwa ndio alikuwa mesmaji pekee wa T'nyika aliyekuwa amebaki!! Tumwombee tu afya njema atakuja kuibuka kivingine 2025!!Mc tuletee Mzee ****** wa Kongwa, tupate nasaha zake tafadhali
Ni kweli, ukifuatilia migao waliyokuwa wanapata!! Safari hii wako kimya utafikiri hawajapata!! wanachekea tumboni ili kutowakera wat'nyika!Tutawapa bilion 400 tu.
Kwani raia wa "nchi" ya zenji ni asilimia ngapi ya raia waTz?Asilimia 20
Mama anaupiga mwingi.
Eti barabara, hivi ni vichekesho,trilioni 1.2 kwaajili ya tabia nchi, barabara na viwanja vya ndege.
Hawajafikia asilimia 30 ya wakazi wa DarKwani raia wa "nchi" ya zenji ni asilimia ngapi ya raia waTz?
Zanzibar zetu ngapi kwenye T 1.2?