Tanzania yapokea mkopo wa trilioni 1.2 kutoka Benki ya Dunia. Kuboresha tabia nchi, usalama na barabara

Tanzania yapokea mkopo wa trilioni 1.2 kutoka Benki ya Dunia. Kuboresha tabia nchi, usalama na barabara

UVCCM-TAIFA
MEI 30, 2022

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan unaosimamia matumizi sahihi ya fedha za umma kwa maendeleo, ukuaji wa Uchumi unaotokana na mazingira bora ya Biashara na Uwekezaji pamoja na uhimilivu wa Deni la Taifa kwa kiwango cha kuridhisha kumeiwezesha Tanzania kupata mkopo wa masharti nafuu wa Shilingi Trilioni 1.2 kutoka Benki ya Dunia.

Mkopo huo ni kwaajili ya kuboresha usalama, ustahimilivu wa tabia ya nchi ,uwezo wa barabara za ndani na viwanja vya ndege vya Mikoa hapa nchini.

Ufadhili huu utasaidia kuboresha na kukarabati wa barabara zenye urefu wa kilomita 500, huku ikilenga kujenga na kuboresha Miundombinu katika hali ambayo itaweza kuendana na mazingira pamoja na athari za hali ya hewa ili kuongeza ustahimilivu wa barabara.

#AwamuYa6Kazino
#TunajengaTaifaLetu
#2022JiandaeKuhesabiwa
#Kaziiendelee
IMG-20220530-WA0416.jpg
 
Back
Top Bottom