Tanzania yapokea Msaada wa Dawa ya kufubaza COVID-19 kutoka Madagascar

Tanzania yapokea Msaada wa Dawa ya kufubaza COVID-19 kutoka Madagascar

Jana Prof Kabuni alisema kuwa dawa iliyotetwa kutoka Madagascar itafanyiwa utafiti kwanza kabla ya kutumika.

Swali 1: Mbona yeye Prof Kabudi anaonekana akipiga glass ya dawa hiyo, je ameshaifanyia utafiti?
Swali 2: Kwanini serikali itume ndege kuchukua dawa ambayo bado haijafanyiwa utafiti?

View attachment 1444553
Mkuu hawa viongozi wetu wameshachanganyikiwa kitambo sana
 
Kabudi kasema yeye kainywa ili kuonyesha shukrani kwa aliyetoa msaada.
 
Kama hawa ndiyo maprofesa wa Tanzania. Unaanza kutumia, utafiti baadaye.

Haishangazi maana kama hata madokta walishindishwa kwenye mistari mirefu na babu wa Loliondo, hakuna cha ajabu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe unavyokunywa mbege ilifanyiwa utafiti na nani?
 
Hiyo dawa kaletewa jiwe na team yake, na na ndio maana wameleta chache tu, sasa ili kuepuka maswali mengi pale itakapouliziwa kuwa mbona haifumiki huko mahospitalini, ndio wakaja na hii via eti wanaifanyia utafiti, wakati yeye na kina jiwe tayari wameshakunywa,.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jana Prof Kabuni alisema kuwa dawa iliyotetwa kutoka Madagascar itafanyiwa utafiti kwanza kabla ya kutumika.

Swali 1: Mbona yeye Prof Kabudi anaonekana akipiga glass ya dawa hiyo, je ameshaifanyia utafiti?
Swali 2: Kwanini serikali itume ndege kuchukua dawa ambayo bado haijafanyiwa utafiti?

View attachment 1444553
Hivi Kabudi alipataje uprofesa ?
 
Msomi akishaingia siasa kila kitu kina change.
 
Back
Top Bottom