Tanzania yapokea Msaada wa Dawa ya kufubaza COVID-19 kutoka Madagascar

Tanzania yapokea Msaada wa Dawa ya kufubaza COVID-19 kutoka Madagascar

😃😃😃😃 Hii kali
Angwaambia hivi kule, angerudi alivyokwemda bila mzigo.
 
Utafiti? Hawa jamaa wamechemsha baada ya tamko LA WHO.
Dawa ya kufanya utafiti mnapeleka ndege kuchukua tank nzima?
Utafiti wakati Kabudi keshapiga chupa nzima?
Hii nchi ni ya WAGAGAGIGIKOKO kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Utafiti Caton 12 Halafu mbona caton 9 zinaenda chato au mtafiti mkuu yupo chato? Taifa la kipumbavu sana.
 
Dawa isipothibitishwa na WHO inakuwa sio dawa?

Kweli ukoloni umenata kwenye akili yako!

Sent using Jamii Forums mobile app
Sio kuthibitishwa na WHO lakini dawa iwe imekithi vigezo.
Ngoja nikupe somo.Ugunduzi wa dawa unapitia njia nyingi na si jambo la siku moja au mwezi mmoja.Mmea huo walioona Madascara kuwa unatibu Corona jambo la kwanza unaingizwa maabara na kuangaliwa kama hauna kemikali au vitu ambavyo vina madhara kwa binadamu.Ikipita hapo inajaribiwa kwa wanyama hasa panya na hapo inajulikana kama ina madhara,inakaa muda gani mwilini,vipi athari zake kwa figo,maini (mara nyingi hawa panya huuliwa na viungo vyao kuchunguzwa).ikipita hapo wanapewa watu wachache amabao hawana ugonjwa na watu hawa wanafuatiliwa ili kugundua kama kuna madhara.Baada ya hapo wanaanza kupewa wagonjwa na dawa inaendelea kufuatiliwa.
Unakumbuka usemi wa Babu wa Loliondo,"Pamoja na kikombe hiki,usiache dawa zako"
 
Namsikiliza hapa Waziri Kabudi anasema walifuata dawa madagascar wafanyie utafiti kwanza kabla ya matumizi.

My take;

Tanzania tumechukua majukumu ya WHO ? kwanini Madascar wasingepeleka wenyewe kwanza hiyo dawa ipitishwe na WHO.


Lakini jana Kabudi kaonekana akibugia dawa hadharani bila hata ya huo utafiti anaousema...
Tani zaidi ya 2 za kufanyia utafiti? Wallahi reseach ya kipekee hii.
 
Anasema yeye alipewa kunywa kwa heshima ya kipekee na kuwatia moyo watu wa Madagascar
 
Jana Prof Kabuni alisema kuwa dawa iliyotetwa kutoka Madagascar itafanyiwa utafiti kwanza kabla ya kutumika.

Swali 1: Mbona yeye Prof Kabudi anaonekana akipiga glass ya dawa hiyo, je ameshaifanyia utafiti?
Swali 2: Kwanini serikali itume ndege kuchukua dawa ambayo bado haijafanyiwa utafiti?

1589012939128.png
 
Back
Top Bottom