Tanzania yashindwa kwenye kesi, yaamuriwa kulipa fidia ya zaidi ya Tsh. Bilioni 260

Wewe ndio huna maarifa,mkataba wowote mahali popote,wakati wowote ukiuvunja,ukisitisha,ukiuondoa kwa namna yoyote lazima ile kwako.Tumia maarifa.
Kwa akili za namna hii ya kuogopa kuvunja mkataba, ukikutana na mkataba mbovu utakuwa mtumwa wa mkataba maisha yako yote
 
Sasa huo unaousema wewe mbovu qatu wanajichotea mi dollars bila kufanya kazi.

Kumbuka huo siyo wa kwanza na huo siyo wa mwisho. Juzi ndege imetoka kukombolewa Uholanzi, na hizi tukichelewa kulipa deni linaongezeka kila kukicha, wazungu walivyo wahuni wanawacha ziongezeke, wajiingizie ziyada bila jasho.
Unasema wazungu walivyo wahuni, huku unashangilia mikataba ambayo Kuna kila dalili ya uhuni. Hiyo ni kuikosea hata nafsi yako
 
Bora uvunje mkataba wa ndoa hata kama sheria inataka kugawana nusu kwa nusu na mtu ambaye hajachaingia chochote ili nusu itakayobaki ule kwa furaha
 
Kituo cha Kimataifa cha Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji (ICSID) kimeiamuru Tanzania kulipa dola milioni 109.5 (zaidi ya bilioni 260 za Tanzania) kwa kampuni za uchimbaji madini zilizosajiliwa Uingereza, Ntaka Nickel Holdings Ltd na Nachingwea UK Ltd, kufuatia uamuzi wa mwaka 2018 kufuta Leseni yao ya Kuhifadhi madini ya Nikeli.

Kampuni hizo zilifanikiwa kuishitaki Tanzania katika mahakama ya Benki ya Dunia kwa kukiuka majukumu yake chini ya Mkataba wa Uwekezaji wa Nchi Baina ya Uingereza na Tanzania (BIT) na sheria za kimataifa kwa kunyang'anya leseni hiyo.

Tanzania pia imetakiwa kulipa dola milioni 3.859 za gharama za kisheria kwa wadai, pamoja na ada na gharama za mahakama ya ICSID.

Kampuni ya Indiana Resources Ltd iliyoorodheshwa kutoka Australia, ambayo ndiyo wanahisa wengi wa mradi wa nikeli wa Ntaka, iliwahi kutishia kukamata ndege zinazoendeshwa na Kampuni ya Air Tanzania (ATCL). Indiana inasema sasa itachukua hatua haraka kutekeleza tuzo ya mahakama

Kampuni za EcoDevelopment na EcoEnergy za Uswidi mwaka jana zilishinda uamuzi wa $165m dhidi ya Tanzania kwenye ICSID kufuatia uamuzi wa serikali ya Magufuli kuwanyang'anya wawekezaji hao ardhi ya Bagamoyo, kinyume na Mkataba wa Uwekezaji wa Nchi Baina ya Sweden na Tanzania (BIT)

Kampuni hizo zilikamata ndege ya Airbus inayomilikiwa na Wakala wa Serikali wa Ndege za Serikali (TGFA) inayoendeshwa na ATCL ili kutekeleza hukumu ya ICSID.

Ndege hiyo yenye namba za usajili 5H-TCH hivi karibuni ilirejea Tanzania baada ya serikali kumaliza kesi hiyo.

View attachment 2691787

Pia soma: Maamuzi ya Magufuli yaigharimu Tanzania zaidi ya Bilioni 266
Hasara nyingine ya maamuzi ya yule Rais wenu wa Wanyonge.
Mkataba huu je CCM italaani mabeberu na kuitisha maandamano nchi nzima kuhusu kesi za fidia za namna hii ?

Serikali ya CCM itambue hakuna mwekezaji aliye na fedha mfukoni.

Mwejezaji akisha saini kuenda kunadi mradi wake ktk mabenki na wabia wengine ili ku mobilise resources yaani kupata rasilimali fedha, watu mfano kutafuta mine engineers, kuhamisha heavy equipments ma caterpillar, excavator, drilling machine n.k tena kwa kukodisha, kutayarisha usafiri wa mavifaa haya mazito n.k, kulipa insurance n.k n.k

Hivyo ghafla ukimfutia mkataba au leseni wengi walio nyuma ya mwekezaji wanapata hasara ya mali, fedha,watu, wakati, kukosa kipato walichotarajia, hadhi / goodwill ya aliyesuka deal hili na serikali ya Tanzania kushuka kwa kudhaniwa hawakufanya makubaliano yaliyostahili na waswahili hivyo wanaweza kukosa kazi siku za usoni sehemu zingine za dunia n.k

Hakuna namna hasara hizo lazima Tanzania iilipe kwa maamuzi ya kutoona mbali wakati wa kumkubali mwekezaji ukifikiri ana fedha kibao mfukoni zimekaa tu kumbe jamaa hawa wana watu wengi wanaocheza upatu a.k.a chungu cha kibubu kuchangishana fedha wengine wamekopa kwa jirani mtaa mmoja kwa riba kubwa kwa ajili miradi mikubwa ya uwekezaji wakisubiri kwa hamu mgao wao halali mambo yakilipa walipowekeza.

NACHINGWEA U.K. LIMITED (UK), NTAKA NICKEL HOLDINGS LIMITED (UK) AND NACHINGWEA NICKEL LIMITED (TANZANIA) V. TANZANIA refence Case ID:

ICSID Case No. ARB/20/38

N.B
Mkataba mbovu wa DP World nao una sifa hizo hizo za wawekezaji na huja na gharama zake kama hizo.
Hasara nyingine Tzn inapata kutokana na maamuzi mabovu ya yule Rais wa kina John the babtist
 
Na bado itashindwa nyingi tu hadi tupate akili, baadhi ya watu wamefanya nchi ni mali ya familia zao na tumekaa kimya tu kwa uoga. Bado tuuzwa mnadani kama mbuzi kwa kuuendekeza unyani.
 
Hasara nyingine ya maamuzi ya yule Rais wenu wa Wanyonge.
Hasara nyingine Tzn inapata kutokana na maamuzi mabovu ya yule Rais wa kina John the babtist

Sielewi kivipi mnajaribu kuwatenganisha viongozi wa CCM? Nijuavyo wote ni wale wale kama ilivyo CCM ni ile ile. Kikwete aliyetoa leseni mbovu na Magufuli aliyeifuta kihuni ni dugu moja wa chama kile kile - CCM. Hawajali nchi wala Watanzania. Hawasikii, hawaambiliki. Wote wamejaa jeuri na kibri. Hakuna wa kuwafanya kitu...

Hadi siku Watanzania watakapoamka na kuiona picha kubwa kuwa CCM ndio msiba mkuu wa taifa hili. The real NATIONAL TRAGEDY!
 
Ni upumbavu nchi kukaa na mwekezaji anayeingiza 98%ya mapato yote, halafu nchi inagewa 2%tu! Kisa mkataba

Ni bora kama nchi tuanze upya!
 
Mkataba huu je CCM italaani mabeberu na kuitisha maandamano nchi nzima kuhusu kesi za fidia za namna hii ?

Serikali ya CCM itambue hakuna mwekezaji aliye na fedha mfukoni.

Mwejezaji akisha saini kuenda kunadi mradi wake ktk mabenki na wabia wengine ili ku mobilise resources yaani kupata rasilimali fedha, watu mfano kutafuta mine engineers, kuhamisha heavy equipments ma caterpillar, excavator, drilling machine n.k tena kwa kukodisha, kutayarisha usafiri wa mavifaa haya mazito n.k, kulipa insurance n.k n.k

Hivyo ghafla ukimfutia mkataba au leseni wengi walio nyuma ya mwekezaji wanapata hasara ya mali, fedha,watu, wakati, kukosa kipato walichotarajia, hadhi / goodwill ya aliyesuka deal hili na serikali ya Tanzania kushuka kwa kudhaniwa hawakufanya makubaliano yaliyostahili na waswahili hivyo wanaweza kukosa kazi siku za usoni sehemu zingine za dunia n.k

Hakuna namna hasara hizo lazima Tanzania iilipe kwa maamuzi ya kutoona mbali wakati wa kumkubali mwekezaji ukifikiri ana fedha kibao mfukoni zimekaa tu kumbe jamaa hawa wana watu wengi wanaocheza upatu a.k.a chungu cha kibubu kuchangishana fedha wengine wamekopa kwa jirani mtaa mmoja kwa riba kubwa kwa ajili miradi mikubwa ya uwekezaji wakisubiri kwa hamu mgao wao halali mambo yakilipa walipowekeza.

NACHINGWEA U.K. LIMITED (UK), NTAKA NICKEL HOLDINGS LIMITED (UK) AND NACHINGWEA NICKEL LIMITED (TANZANIA) V. TANZANIA refence Case ID:

ICSID Case No. ARB/20/38

N.B
Mkataba mbovu wa DP World nao una sifa hizo hizo za wawekezaji na huja na gharama zake kama hizo.
Juzi kiongozi wa dini kasema,tusiwalaumu mabeberu kwa sababu ya ujinga wetu.Hivyo tukiandamana tutahesabiwa wapumbavu heri tubaki na ujinga wetu
 
Maumivu mengine kutokana na maamuzi ya Mwendazake Magufuli..

Too painful.....Kodi tunazokatwa Kila mwezi zinaenda kulipa watu.!

Kwa Nini tusijitoe kwenye Mahakama ya kinyonyaji?
 
Aliyeingia ndio mpumbavu, aliyevunja ndio alitumia akili, huwezi kuingia mkataba wa kipuuzi usio na maslahi kwa taifa halafu uje kumlaumu yule aliyeuvunja, wewe ndie utumie akili.
Acha kutetea ujinga
 
Kituo cha Kimataifa cha Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji (ICSID) kimeiamuru Tanzania kulipa dola milioni 109.5 (zaidi ya bilioni 260 za Tanzania) kwa kampuni za uchimbaji madini zilizosajiliwa Uingereza, Ntaka Nickel Holdings Ltd na Nachingwea UK Ltd, kufuatia uamuzi wa mwaka 2018 kufuta Leseni yao ya Kuhifadhi madini ya Nikeli.

Kampuni hizo zilifanikiwa kuishitaki Tanzania katika mahakama ya Benki ya Dunia kwa kukiuka majukumu yake chini ya Mkataba wa Uwekezaji wa Nchi Baina ya Uingereza na Tanzania (BIT) na sheria za kimataifa kwa kunyang'anya leseni hiyo.

Tanzania pia imetakiwa kulipa dola milioni 3.859 za gharama za kisheria kwa wadai, pamoja na ada na gharama za mahakama ya ICSID.

Kampuni ya Indiana Resources Ltd iliyoorodheshwa kutoka Australia, ambayo ndiyo wanahisa wengi wa mradi wa nikeli wa Ntaka, iliwahi kutishia kukamata ndege zinazoendeshwa na Kampuni ya Air Tanzania (ATCL). Indiana inasema sasa itachukua hatua haraka kutekeleza tuzo ya mahakama

Kampuni za EcoDevelopment na EcoEnergy za Uswidi mwaka jana zilishinda uamuzi wa $165m dhidi ya Tanzania kwenye ICSID kufuatia uamuzi wa serikali ya Magufuli kuwanyang'anya wawekezaji hao ardhi ya Bagamoyo, kinyume na Mkataba wa Uwekezaji wa Nchi Baina ya Sweden na Tanzania (BIT)

Kampuni hizo zilikamata ndege ya Airbus inayomilikiwa na Wakala wa Serikali wa Ndege za Serikali (TGFA) inayoendeshwa na ATCL ili kutekeleza hukumu ya ICSID.

Ndege hiyo yenye namba za usajili 5H-TCH hivi karibuni ilirejea Tanzania baada ya serikali kumaliza kesi hiyo.

View attachment 2691787

Pia soma: Maamuzi ya Magufuli yaigharimu Tanzania zaidi ya Bilioni 266
 
Juzi kiongozi wa dini kasema,tusiwalaumu mabeberu kwa sababu ya ujinga wetu.Hivyo tukiandamana tutahesabiwa wapumbavu heri tubaki na ujinga wetu
Kuandamana dhidi ya “mabeberu” ni ujuha uliopitiliza. Tatizo letu ni serikali tunayoiendekeza inayoongozwa na watu wenye jeuri mbaya sana.

Kama ni maandamano basi yalenge kuwaondoa madarakani hao viongozi muflis, la sivyo heri tubaki na ujinga wetu!
 
Tutafilisika, inabidi ifike mahali tukatae tu kulipa liwalo na liwe.
 
Back
Top Bottom