Tanzania yashindwa kwenye kesi, yaamuriwa kulipa fidia ya zaidi ya Tsh. Bilioni 260

Tanzania yashindwa kwenye kesi, yaamuriwa kulipa fidia ya zaidi ya Tsh. Bilioni 260

Kituo cha Kimataifa cha Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji (ICSID) kimeiamuru Tanzania kulipa dola milioni 109.5 (zaidi ya bilioni 260 za Tanzania) kwa kampuni za uchimbaji madini zilizosajiliwa Uingereza, Ntaka Nickel Holdings Ltd na Nachingwea UK Ltd, kufuatia uamuzi wa mwaka 2018 kufuta Leseni yao ya Kuhifadhi madini ya Nikeli.

Kampuni hizo zilifanikiwa kuishitaki Tanzania katika mahakama ya Benki ya Dunia kwa kukiuka majukumu yake chini ya Mkataba wa Uwekezaji wa Nchi Baina ya Uingereza na Tanzania (BIT) na sheria za kimataifa kwa kunyang'anya leseni hiyo.

Tanzania pia imetakiwa kulipa dola milioni 3.859 za gharama za kisheria kwa wadai, pamoja na ada na gharama za mahakama ya ICSID.

Kampuni ya Indiana Resources Ltd iliyoorodheshwa kutoka Australia, ambayo ndiyo wanahisa wengi wa mradi wa nikeli wa Ntaka, iliwahi kutishia kukamata ndege zinazoendeshwa na Kampuni ya Air Tanzania (ATCL). Indiana inasema sasa itachukua hatua haraka kutekeleza tuzo ya mahakama

Kampuni za EcoDevelopment na EcoEnergy za Uswidi mwaka jana zilishinda uamuzi wa $165m dhidi ya Tanzania kwenye ICSID kufuatia uamuzi wa serikali ya Magufuli kuwanyang'anya wawekezaji hao ardhi ya Bagamoyo, kinyume na Mkataba wa Uwekezaji wa Nchi Baina ya Sweden na Tanzania (BIT)

Kampuni hizo zilikamata ndege ya Airbus inayomilikiwa na Wakala wa Serikali wa Ndege za Serikali (TGFA) inayoendeshwa na ATCL ili kutekeleza hukumu ya ICSID.

Ndege hiyo yenye namba za usajili 5H-TCH hivi karibuni ilirejea Tanzania baada ya serikali kumaliza kesi hiyo.

View attachment 2691787

Pia soma: Maamuzi ya Magufuli yaigharimu Tanzania zaidi ya Bilioni 266
hii ndo mikataba ya kijinga am,bayo ccm kwa mgongo wa serikali wanasaini, sasa hii cha mtoto subiri ule wa bandari usainiwe tutalimia meno
 
Halafu bado wapo wengi wanaotaka CCM itawale milele kisa eti “hakuna upinzani makini” nchini. Eti kuliko Lissu au Mbowe awe Rais hata kwa awamu moja bora tuendelee na hawa hawa.

Ni ujinga uliokithiri kuipa mijizi gerentii ya kufisidi nchi kupitia CCM. Huo ndio MSIBA mkuu wa taifa hili. Na bado.
 
Sakata la bandari ni ‘blessings in disguise’ kwa Tanzania.

Lipo wazi kwanini awashindi hizo kesi; ata walimu wao wa sheria hao hakina Shivji hawana fundamentals za contract law.

Kwa wanasheria mbali mbali niliowasikia kwenye sakata la bandari, Tanzania aishindi kesi ya biashara nje ya mipaka yake.
 
Sasa huo unaousema wewe mbovu qatu wanajichotea mi dollars bila kufanya kazi.

Kumbuka huo siyo wa kwanza na huo siyo wa mwisho. Juzi ndege imetoka kukombolewa Uholanzi, na hizi tukichelewa kulipa deni linaongezeka kila kukicha, wazungu walivyo wahuni wanawacha ziongezeke, wajiingizie ziyada bila jasho.
Si mnasapoti mikataba mibovu wajukuu watatucheka sana
 
Kufuta ni kitu kimoja ila namna unavyofuta ndio kitu kingine. Unaweza tafuta kipengeke kilichovunjwa ukaenda ICSID huko ukadai mkataba uvunjwe. Ila sio unaamka tu asubuhi unaenda kunyang'anya leseni hata kama una haki ila mchakato uliotumika utaku-cost.
Lakini kiini cha yote ni kuingia mikataba mibovu.
 
Kufuta ni kitu kimoja ila namna unavyofuta ndio kitu kingine. Unaweza tafuta kipengeke kilichovunjwa ukaenda ICSID huko ukadai mkataba uvunjwe. Ila sio unaamka tu asubuhi unaenda kunyang'anya leseni hata kama una haki ila mchakato uliotumika utaku-cost.
Wakati mwingine ni heri kuumia mara moja ukaachana naye, kuliko kuishi katika mateso milele
 
Kituo cha Kimataifa cha Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji (ICSID) kimeiamuru Tanzania kulipa dola milioni 109.5 (zaidi ya bilioni 260 za Tanzania) kwa kampuni za uchimbaji madini zilizosajiliwa Uingereza, Ntaka Nickel Holdings Ltd na Nachingwea UK Ltd, kufuatia uamuzi wa mwaka 2018 kufuta Leseni yao ya Kuhifadhi madini ya Nikeli.

Kampuni hizo zilifanikiwa kuishitaki Tanzania katika mahakama ya Benki ya Dunia kwa kukiuka majukumu yake chini ya Mkataba wa Uwekezaji wa Nchi Baina ya Uingereza na Tanzania (BIT) na sheria za kimataifa kwa kunyang'anya leseni hiyo.

Tanzania pia imetakiwa kulipa dola milioni 3.859 za gharama za kisheria kwa wadai, pamoja na ada na gharama za mahakama ya ICSID.

Kampuni ya Indiana Resources Ltd iliyoorodheshwa kutoka Australia, ambayo ndiyo wanahisa wengi wa mradi wa nikeli wa Ntaka, iliwahi kutishia kukamata ndege zinazoendeshwa na Kampuni ya Air Tanzania (ATCL). Indiana inasema sasa itachukua hatua haraka kutekeleza tuzo ya mahakama

Kampuni za EcoDevelopment na EcoEnergy za Uswidi mwaka jana zilishinda uamuzi wa $165m dhidi ya Tanzania kwenye ICSID kufuatia uamuzi wa serikali ya Magufuli kuwanyang'anya wawekezaji hao ardhi ya Bagamoyo, kinyume na Mkataba wa Uwekezaji wa Nchi Baina ya Sweden na Tanzania (BIT)

Kampuni hizo zilikamata ndege ya Airbus inayomilikiwa na Wakala wa Serikali wa Ndege za Serikali (TGFA) inayoendeshwa na ATCL ili kutekeleza hukumu ya ICSID.

Ndege hiyo yenye namba za usajili 5H-TCH hivi karibuni ilirejea Tanzania baada ya serikali kumaliza kesi hiyo.

View attachment 2691787

Pia soma: Maamuzi ya Magufuli yaigharimu Tanzania zaidi ya Bilioni 266
Hawatuwezi na hawatatuyumbisha kwa kesi zao na mahakama zao, sisi tutatumia sheria na mahakama zetu.
 
Ni hivi,Magufuli hakuwahi kuwa na nia ya kuwasaidia watz kwa ujumla.Mfano ni KIWANDA CHA SARUJI CHA DANGOTE.Kikwete aliwaangalia raia na kuwatafutia njia za kuwafanyia wepesi katika kupiga hatua kimaendeleo.Ujio wa Dangote ulilenga kuwasaidia raia katika kuleta makazi bora kwa kila raia,alikiruhusu kiwanda kizalishe Saruji ya viwango vyote ili kuwawezesha raia wa vipato vya kawaida pia kumudu gharama ya kununua Saruji kwa ujenzi wa makazi.
Kiwanda cha Dangote kilifanya Saruji huku mikoani kuuzwa kwa Tsh12000 kwa mfuko.
Magufuli alipoingia madarakani alimzuia Dangote kuzalisha Saruji ya viwango vyote na kumtaka abaki akizalisha Saruji ya viwango vya kimataifa tu ambayo mfuko mmoja ni kati ya Tsh 25000 hadi 35000.
Leo hii hakuna tena Saruji ya Dangote madukani huku mikoani,bei ya Saruji kwa sasa ni kati ya Tsh 18000 hadi 22000.

Sasa kwa mfano huu unaweza kusema Magufuli alikuwa akiwajali raia na maisha yao?.
Huo uzalendo mnaouimba toka kwake ni upi hasa?.
Kwa hiki alichokifanya kwa Saruji ya Dangote,alikifanya kwa manufaa ya nani?.
Tunawezaje muamini mtu wa aina yake katika malengo ya kuivunja mikataba hii tukiangalia mfano wa kiwanda cha Dangote?.
Kuna kitu wanakiita standard
 
Back
Top Bottom