Azimio la Bunge : 10 June 2023
APPENDIX ONE
Mheshimiwa Spika, Mwenyekiti wa Kamati ya Pamoja
ambayo imeshughulikia alisema haya ni makubaliano na
makubaliano haya yanaweka msingi wa kitu kitakachokuja
kufanyika, hiyo mikataba itakayokuja kujengwa huko mbele. Huu
sio mkataba wameshazungumza watu, huu sio mkataba,
tunawatoa hofu Watanzania wayasikilize hayo maelezo vizuri,
lakini mikataba itakuja mmoja mmoja katika eneo moja moja.
Mheshimiwa Spika, ukienda katika mkataba huu kuna
appendix I ambayo kuna mambo ambayo phase one project
zitakazofanyika. Kwa hiyo, ndani ya project zile zitakapofanyika
ndipo kutakuwa kuna hiyo mikataba midogo midogo na mimi
nilitoe hofu Bunge hili na wananchi wa Tanzania sio kwamba kila
kilichotajwa kwamba kitafanyika kwa yote. Ukisikia kutafanyika
development, ukisikia kutafanyika improvement ukisikia
kutafanyika management, ukisikia kutafanyika operations, kuna
miradi au kuna phase au kuna project ziko katika hatua tofauti
tofauti. Ziko nyingine tutaanza kweli ku–develop kwa sababu ni
kitu kipya, lakini kuna vingine vinatakiwa kufanyiwa management,
lakini kuna vingine vitafanyiwa operation. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, sasa ukitazama kuanzia hiyo gati zero
mpaka gati number seven utakuja kuona kwamba ni kweli, ukiijua
ile bandari kwamba kuna maeneo kutafanyika operation na kuna
maeneo mengine wao wata-improve lakini wataachiwa bandari
wenyewe waendeleze. Sasa na mimi na stick pale pale kwenye
ushauri wa Kamati kwamba ni lazima tuhakikishe hiyo mikataba
sasa iwe ina tija kwa Watanzania. Tuhakikishe hiyo mikataba
wanashirikishwa wadau husika tutakapoingia hiyo mikataba
mmoja mmoja, lakini pia mikataba hiyo ni lazima itoe ukomo au
itaje ukomo kama wananvyosema wengine na maoni mwengine
ambayo Mwenyekiti ameshauri na Wajumbe wengine Wabunge
wengine wameshauri.
Mheshimiwa Spika, lakini hofu nyingine kwamba huu
mkataba hauna ukomo, mkataba huu unao ukomo nao
umetajwa, sisi kama Wabunge wa Bunge lako hili tukufu tumekaa
hapa kwamba tunaelewa nini kinaendelea....
Soma zaidi toka : 10 June 2023 Bunge kuhusu pendekezo la kuridhiwa mkataba baina ya serikali ya Tanzania na serikali ya Dubai
:
Parliament of Tanzania
Bunge la Tanzania / Parliament of Tanzania