Tanzania yashindwa kwenye kesi, yaamuriwa kulipa fidia ya zaidi ya Tsh. Bilioni 260

Tanzania yashindwa kwenye kesi, yaamuriwa kulipa fidia ya zaidi ya Tsh. Bilioni 260

Utawala wa CCM unaiingiza nchi ktk matatizo na umaskini kila uchao!
Hii mikataba iliingiwa na kikwete kifisafdi (kama kawa yake) Mwendazake akaivunja kutokana na ufisadi aliofanya!
Sasa imekwenda kulekule UK na ndio tunatakiwa kulipa hizi fedha! CCM CCM huu ushetani wenu Mola atatulipia!
Wewe hujayaona matatizo, unayasikia tu.

Hamia Kenya.
 
Ngoja tupigwe mpaka tuamuke na kujua kujitetea. Yaani ni kama vile hii mikataba inawekeza pia kuvuna sio tu kwenye uwekezaji bali hata kwenye kesi- wanavuna kotekote…hatari na nusu..
 
Sio maamuzi ya magufuli ni maamuzi ya Samia nanmagufuli
 
Walipe hiyo na wakimaliza watalipa za DP world ukijua kula ujue kuna kuliwa pia
 
Ngoja tupigwe mpaka tuamuke na kujua kujitetea. Yaani ni kama vile hii mikataba inawekeza pia kuvuna sio tu kwenye uwekezaji bali hata kwenye kesi- wanavuna kotekote…hatari na nusu..
Wanakuja tu na wazo. Shamba lako.pale Bush nitalima na kukwambia utavuna gunia 25 badala ya 5 za sasa na nitakupa gunia 9 . Kwa hiyo ukighairi nakupiga faini ya kwa nini umenikosesha gunia 250 kwa miaka 10 bila kujali 90 zako.
 
Km imeweza kuikopesha Zanzibar zaidi ya Billion 470 Cash kupitia Bank ya NBC, watashindwa kuzilipa hizo Pesa ndogo za kujengea tudaraja pale kalenga busisi
Serikali ya Tanganyika inachezewa na wazanzibari haswa.

Watanganyika wamelala, Tutakuja kulipa ela Nyingi Sana za DP world kutoka na Mkataba wa sasa Kati ya Tanzania na DP world.
 
Serikali ya Tanganyika inachezewa na wazanzibari haswa.

Watanganyika wamelala, Tutakuja kulipa ela Nyingi Sana za DP world kutoka na Mkataba wa sasa Kati ya Tanzania na DP world.
Propaganda
 
Nimesoma humu dp world wanataka billion 250 + kama pesa iliyotumika kushika uchumba(rushwa) kwa viongoz flani, Sasa na hii kesi mbona ni kama mulemule, ,najaribu kuunga doti
Kuna documents yeyote Mkuu share huku tuone mkuuu

Asifiwe Mvua imemnyea
 
Kituo cha Kimataifa cha Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji (ICSID) kimeiamuru Tanzania kulipa dola milioni 109.5 (zaidi ya bilioni 260 za Tanzania) kwa kampuni za uchimbaji madini zilizosajiliwa Uingereza, Ntaka Nickel Holdings Ltd na Nachingwea UK Ltd, kufuatia uamuzi wa mwaka 2018 kufuta Leseni yao ya Kuhifadhi madini ya Nikeli.

Kampuni hizo zilifanikiwa kuishitaki Tanzania katika mahakama ya Benki ya Dunia kwa kukiuka majukumu yake chini ya Mkataba wa Uwekezaji wa Nchi Baina ya Uingereza na Tanzania (BIT) na sheria za kimataifa kwa kunyang'anya leseni hiyo.

Tanzania pia imetakiwa kulipa dola milioni 3.859 za gharama za kisheria kwa wadai, pamoja na ada na gharama za mahakama ya ICSID.

Kampuni ya Indiana Resources Ltd iliyoorodheshwa kutoka Australia, ambayo ndiyo wanahisa wengi wa mradi wa nikeli wa Ntaka, iliwahi kutishia kukamata ndege zinazoendeshwa na Kampuni ya Air Tanzania (ATCL). Indiana inasema sasa itachukua hatua haraka kutekeleza tuzo ya mahakama

Kampuni za EcoDevelopment na EcoEnergy za Uswidi mwaka jana zilishinda uamuzi wa $165m dhidi ya Tanzania kwenye ICSID kufuatia uamuzi wa serikali ya Magufuli kuwanyang'anya wawekezaji hao ardhi ya Bagamoyo, kinyume na Mkataba wa Uwekezaji wa Nchi Baina ya Sweden na Tanzania (BIT)

Kampuni hizo zilikamata ndege ya Airbus inayomilikiwa na Wakala wa Serikali wa Ndege za Serikali (TGFA) inayoendeshwa na ATCL ili kutekeleza hukumu ya ICSID.

Ndege hiyo yenye namba za usajili 5H-TCH hivi karibuni ilirejea Tanzania baada ya serikali kumaliza kesi hiyo.

View attachment 2691787

Pia soma: Maamuzi ya Magufuli yaigharimu Tanzania zaidi ya Bilioni 266
Hii nchi itamalizwa na madeni.
 
Hii mikataba ifutwe isifutwe tunaliwa. Ukiwaacha wanaiba tena kwa kuwalipia na gharama za kukuibia, ukiwaindoa unalipa kwa kushindwa kesi kwa terms za mikataba zilizoingiwa zikiwa za ovyo. Mfano mkataba huu unaosema bandari zote. Siku wakikukaba ukavunja mkataba unalipa, ukiwaacha wanaiba.
UKOLONI na KUGAWANYWA kwa waafrika kupitia viongozi VIBARAKA sasa ni zaidi kupita kipindi cha karne ya 18.
Ukishaona mikataba ni ya SIRI na watu hawaruhusiwi kuhoji, na watu wengi wanapangwa kushabikia wee jua hakuna kitu.

Kibaya zaidi wapo viongozi ambao kipindi cha JpM walikiwa wanasifu na kumuita majina yote ya Utakatifu. Alipoondoka wakamuita majina yote ya Uzandiki. Mtu kama huyo hafai lkn leo yupo
 
Back
Top Bottom