Tanzania yasitisha vibali vya usafirishaji wa mahindi nje ya nchi

Tiss imefeli kumshauri hili mama kwa wakati hadi kupanda kwa mchele kuwa 2800 Tsh, na debe la mahindi kuwa 25,000Tsh ni kutokana na kuwa na uhitaji mkubwa kwa soko la nje hasa Kenya na Congo. Maafisa wetu walipaswa kuingilia hili mapema coz hali ya chakula haikuwa nzuri toka mwaka jana isitoshe na mazao yalikuwa duni.
 
Serikali za Africa mashariki Zina Fanya uzembe mkubwa kutowekeza kwenye kilimo Cha ndani. Yaani uwekezaji haswa. Matumizi ya technologia ya kisasa katika kilimo ndio njia pekee ya wananchi wake kupata chakula Cha kutosha. Kilimo tegemezi kilishapitwa na wakati, yaani kusubiria mvua tu ili mazao yawepo. Viongozi waamke, Hali so Hali tena. Dunia ya Sasa haina mda na wazembe!
 
Shida ya nchi yetu tunapenda sana mapambio badala ya kufanya kazi ona Sasa wanashtuka kumekucha
 
Huyu Bashe hata mwezi haujaisha alijinasibu kuruhusu wakulime wauze popote wanapotaka ila waache akiba ya chakula.

Sasa inakuaje tena, tukumbuke mazao ya chakula sasa ni biashara kwa sehemu kubwa.

Tunahitaji kuyalinda masoko pia kwa kuhakikisha supply haipotei.

Sasa hizi tabia za kuwapangia pangia wakulima wafanye nin na chakula chao sio afya.

Serikali inawajibu wa kununua chakula cha kutosha na kuhifadhi katika maghala yake. Itakapofikia upungufu na bei kwenda juu sana iweze kuyatoa sokoni.

Kama haina fedha ikope tu.
 
Ila hii sio haki, NFRA ilitakiwa inunue akiba ya kutosha wakati mahindi ni mengi na bei ni ya chini, sasa wamezembea halafu mnatakq kuja kupora haki ya mkulima kuuza chake anapopataka
 
Hayo mabilioni wakulima wa Tz waliouza mahindi huko wamefanyia nini? Kama waliweka benki wakayatoe sasa waagize na wao
 
Mahindi yakiwa ya kitosha NFRA wanayaacha yaoze kwa wakulima, maana beixinakuwa ndogo sana na waliopewa jukumu la kuyanunua na kuyahifadhi hafanyi hivyo, matokea yake wanakula hasara kubwa, ikifika wakati wa kulipiza ile hasara waliyopata kwa bei kuwa nzuri eti tunawazuia tena wasiuze kwenye bei nzuri, is this fair?!
 
Hii ni kumyanyasa mkulima,

Halafu kenya walivyo wajanja wanasaga unga na kupack vizuri wanaprint made in Kenya wanauza congo bei mara kumi
Sisi tuna millers wadogo maelfu kwa maelfu, hata soko la ndani tu hatujalitosheleza, si rahisi kuuza unga nje
 
Hao NFRA ni kwanini hawakununua kipindi kile mahindi yanaozea majumbani kwa wakulima kwa kukosa soko na nei kuwa mbovu? Walikuwa wapi?!
 
Ila hii sio haki, NFRA ilitakiwa inunue akiba ya kutosha wakati mahindi ni mengi na bei ni ya chini, sasa wamezembea halafu mnatakq kuja kupora haki ya mkulima kuuza chake anapopataka
Hakuna mkulima mwenye mahindi hadi Sasa hivi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…