Tanzania yasitisha vibali vya usafirishaji wa mahindi nje ya nchi

Tanzania yasitisha vibali vya usafirishaji wa mahindi nje ya nchi

Tiss imefeli kumshauri hili mama kwa wakati hadi kupanda kwa mchele kuwa 2800 Tsh, na debe la mahindi kuwa 25,000Tsh ni kutokana na kuwa na uhitaji mkubwa kwa soko la nje hasa Kenya na Congo. Maafisa wetu walipaswa kuingilia hili mapema coz hali ya chakula haikuwa nzuri toka mwaka jana isitoshe na mazao yalikuwa duni.
 
Serikali za Africa mashariki Zina Fanya uzembe mkubwa kutowekeza kwenye kilimo Cha ndani. Yaani uwekezaji haswa. Matumizi ya technologia ya kisasa katika kilimo ndio njia pekee ya wananchi wake kupata chakula Cha kutosha. Kilimo tegemezi kilishapitwa na wakati, yaani kusubiria mvua tu ili mazao yawepo. Viongozi waamke, Hali so Hali tena. Dunia ya Sasa haina mda na wazembe!
 
Shida ya nchi yetu tunapenda sana mapambio badala ya kufanya kazi ona Sasa wanashtuka kumekucha
 
Huyu Bashe hata mwezi haujaisha alijinasibu kuruhusu wakulime wauze popote wanapotaka ila waache akiba ya chakula.

Sasa inakuaje tena, tukumbuke mazao ya chakula sasa ni biashara kwa sehemu kubwa.

Tunahitaji kuyalinda masoko pia kwa kuhakikisha supply haipotei.

Sasa hizi tabia za kuwapangia pangia wakulima wafanye nin na chakula chao sio afya.

Serikali inawajibu wa kununua chakula cha kutosha na kuhifadhi katika maghala yake. Itakapofikia upungufu na bei kwenda juu sana iweze kuyatoa sokoni.

Kama haina fedha ikope tu.
 
Ila hii sio haki, NFRA ilitakiwa inunue akiba ya kutosha wakati mahindi ni mengi na bei ni ya chini, sasa wamezembea halafu mnatakq kuja kupora haki ya mkulima kuuza chake anapopataka
 
Uganda na Rwanda wana mahindi ya kutosha kutoka Tanzania maana serikali iliwapa wafanyabiashara wao mabilioni wanunue Tanzania, watu kama akina bashe wakielezwa haya hawajui na naimani mawaziri wengi hawajui mchezo wa kagame na museveni na kenyata wao wanawapa mabilioni watu wao watafute mazao kokote kule hawa wa kwetu wao wanacheka tu
Hayo mabilioni wakulima wa Tz waliouza mahindi huko wamefanyia nini? Kama waliweka benki wakayatoe sasa waagize na wao
 
Ndiyo maana nafaka zilipanda bei May-July. Ila kwa sasa bei inaanza kushuka.

Suluhisho kwa TANZANIA ni kuzalisha mahindi ya kutosha, Serikali iboreshe skimu za umwagiliaji na upatikanaji wa zana za Kilimo, mbolea na dawa.

Hapa Serikali inawadidimiza wakulima, Kila mwaka wanalima kwa hasara, ni lini watapata faida? Muda kama huu ndiyo neema kwa mkulima!
Mahindi yakiwa ya kitosha NFRA wanayaacha yaoze kwa wakulima, maana beixinakuwa ndogo sana na waliopewa jukumu la kuyanunua na kuyahifadhi hafanyi hivyo, matokea yake wanakula hasara kubwa, ikifika wakati wa kulipiza ile hasara waliyopata kwa bei kuwa nzuri eti tunawazuia tena wasiuze kwenye bei nzuri, is this fair?!
 
Hii ni kumyanyasa mkulima,

Halafu kenya walivyo wajanja wanasaga unga na kupack vizuri wanaprint made in Kenya wanauza congo bei mara kumi
Sisi tuna millers wadogo maelfu kwa maelfu, hata soko la ndani tu hatujalitosheleza, si rahisi kuuza unga nje
 
Hii kitu niliandika humu watu wakaja juu eti ni mda wa mkulima kunufaika. Hakuna mkulima anayepeleka mahindi Kenya ni wafanya Biashara tu ndo wenye uwezo huo tu. Nilipenyezewa za ndani kua mama tozo ameambiwa bohari kuu ya chakula ya serikali Haina chakula.

Ndo kashituka akaagiza na kuzuia kimya kimya tangu wa 7 katikati. Ila Leo ndo wameamua kutangaza. Usalama wa nchi yoyote Ile hua ni utoshelevu wa chakula. Na Bahat mbaya viongozi wetu wa ccm Hilo hawalijui wanawazia matumbo Yao tu
Hao NFRA ni kwanini hawakununua kipindi kile mahindi yanaozea majumbani kwa wakulima kwa kukosa soko na nei kuwa mbovu? Walikuwa wapi?!
 
Ila hii sio haki, NFRA ilitakiwa inunue akiba ya kutosha wakati mahindi ni mengi na bei ni ya chini, sasa wamezembea halafu mnatakq kuja kupora haki ya mkulima kuuza chake anapopataka
Hakuna mkulima mwenye mahindi hadi Sasa hivi
 
Back
Top Bottom