Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 9,189
- 16,128
Wewe ndiye unazungumza mambo usiyoelewa. Vitu ulivyokaririshwa na wanasiasa. Fahamu lengo kuu la serikali kupiga marufuku uuzaji wa mazao ya chakula nje. Lengo si kuzuia wewe usife njaa, lengo ni ili serikali yenyewe isianguke. Moja ya mambo yanayoingiza watu barabarani ni bei ya chakula kuwa juu kwa watu wa mijini. So serikali zinazuia kupanda kwa kufunga mipaka na kuhakikisha bei ya nafaka ipo chini. Hili limefanyika tokea enzi za WaromaTatizo lenu mnaongelea kitu msicho kuwa na elewa nacho.Nchi zote duniani huwa kuna mazingira ambayo yanaweza fanya kuwepo na zuio la muda la kupeleka chakula nje ya nchi, hasa vyakula vikuu, ili kuwapa nafuu wananchi wake.Na ndio maana hapa kwetu kuna maghala ya NFRA, kila kanda, ili kuhifadhi chakula, wakati wa mavuno na kukiuza panapokuwa na upungufu.suala la kilimo huwezi ukasema eti serikali iliache tu, ndio maana huwa wanatakiwa kuwapa ruzuku za pembejeo.Mfano kwa sasa Wakenya wanaingia nchini kununua mahindi tena kwa bei ya juu sana, kwani kule kwao unga upo juu sana kuliko hapa kwetu, ni wazi wafanya biashara wa ndani watashindwa tu kununua, haya wananchi wako utawafanya nini?!!kwani lazima tu utawapa msaada,
Na mwaka huu mavuno yalikuwa kidogo, karibu nchi zote, kwani miaka kama 4 yote huko nyuma mipaka si ilikuwa wazi lakini watu walikuwa wanalia hakuna masoko?!!
Hili linamuumiza nani? Mkulima anayelima. Matokeo yake anashindwa kulima. Matajiri wanaacha kulima. Benki zinaacha kopesha wakulima na njaa inatokea, tena kubwa. Na hili si nadharia. China walikuwa na sera kama hizi zetu. Matokeo yake ni njaa iliyoua mamilioni. Mwisho wake wakaja na mpango. Mkulima anaiuzia serikali sehemu fulani ya mazao yake. Labda 10% yanayobaki yote anauza anakotaka na kwa bei anayotaka. Matokeo yake uzalishaji ukakua kwa mara kadhaa zaidi, leo China njaa ni historia.
Huo utaratibu mnaotaka ufanyike unaleta njaa badala ya kuzuia.