Tanzania yasitisha vibali vya usafirishaji wa mahindi nje ya nchi

Wasiwasi mpya wa upungufu wa unga wa mahindi umeibuka nchini Kenya baada ya Tanzania ambayo ni msafirishaji mkubwa wa mahindi nchini humo kufungia vibali vya kuuza nafaka hiyo nje ya mipaka yake.
Kinana anasemaje
 
Wapi nimesema wapate hasara? Nilikujibu kuwa hao sio wakulima Bali wafanyabiashara ndio ukaanza kuleta pumba zako, alafu Sasa hivi unageuka tena
Kwahiyo wafanya biashara ndio wanastahiki kupata hasara? Kwamba ingekuwa ishu kama ingekuwa ni wakulima, ila sababu si wakulima basi its okay.., hiyo ndio logical implication ya response yako katika mazingira husika. Milango ifunguliwe regardless wanaoweza kupata hasara ni wakulima au wafanyabiashara, hiyo ndio hoja ya msingi.
 
We jamaa hii id yako nishaijua, huwa nasoma hoja zako mwanzo tu nacheka halafu siendelei kutaka kujua umeandika nn.....Una tatizo la kuanza na Unnecessarily harsh tones.
Nilijua akili ya kuendelea zaidi ya hapo huna. Ni sawa na uanzishe hotel mbugani kwa ajili ya wazungu, wakati watalii wanaweza kuja waarabu au wahindi wakalipa same price.
 
Wewe una matatizo ya akili, wapi nimesema wafanyabiashara wanastahiki kupataa hasara?

Nilichikueleza ni kuwa hakuna mkulima anayeweza kupeleka mahindi yake Kenya. Mkulima anauza bei ya soko ilivyo kwa muda husika, atayenunua Kama atayaacha hapa au atapeleka Kenya hiyo ni juu yake
 
Huku kilindi na handeni wakivuna tu wanauza gunia elf30 mpaka 25 unaweza pata alafu baada ya hapo ndoa zinakua nyingi watu wanaongeza wake tu.
.
Saiv wachaga wanauza unga kg1 1500 wanawauzia wakulima
Hapa nilipo kilo 1 ya sembe Tshs. 1,700

Sent from my Nokia 3.2 using JamiiForums mobile app
 
Nilijua akili ya kuendelea zaidi ya hapo huna. Ni sawa na uanzishe hotel mbugani kwa ajili ya wazungu, wakati watalii wanaweza kuja waarabu au wahindi wakalipa same price.
Ubongo wako una condition ya kujudge literary ya binadamu wengine wakati wote. Ukisoma hoja all you think is " huyu mtu ni mjinga".
 
Je Ukraine nao wagome kuwaletea ngano kwa sababu wako vitani?? Acheni sababu zenu za kindezi.. Niko huko vijijini Tanganyika wakulima wengi tuu wamehifadhi mazao yao ya chakula... Wanauza ziada..
 
Ubongo wako una condition ya kujudge literary ya binadamu wengine wakati wote. Ukisoma hoja all you think is " huyu mtu ni mjinga".
Ujinga ni kama pembe la ng'ombe, haujifichi.
 
Nakumbuka ule uzi na vilaza wa chama wakaja kupinga eti tunafungua nchi
 
Upuuzi mtupu. Mimi nimeplan kuuza yangu niliyolima ifikapo december na january na nitauza popote ninapotaka. Hakuna aliyenisaidia kulima.
Mkuu mimi ni mkulima.. Kwa zaidi ya miaka 7 ni mwaka huu tuu ndiyo nimeweza kuuza mahindi kwa bei ya sh 120,000 yakiwa shambani, yaani nimevuna na kupukuchua kwa mashine Mteja anakuja shambani unapima debe 7 kwenye gunia anakupa laki moja na elfu ishirini hapo hapo. Nimeuza nusu ya mzigo na mengine yako stoo. Kiukweli hata machungu ya kununua mbolea mfuko kwa sh 120,000 yameisha kabisa. Huyu Waziri Bashe Mungu amlinde na Mama aendelee kumuacha kwenye hiyo wizara maana kilimo sasa kitakuwa ajira inayolipa kama ajira nyingine tuu. Mpunga pia Nimeuza bei nzuri sanaaaaa, kiujumla wakulima wengi sana wako vizuri kimapato, wameweka akiba ya chakula (ni mkulima asiyejitambua tuu ambaye atauza mavuno yootee aliyopata na kuitesa familia yake kwa njaa. Na kumbuka mkulima kama huyu hana tofauti na mfanyakazi ambaye akipokea mshahara wake anaupeleka Bar au kwa mchepuko na kuacha familia yake ikiteseka).
 
Hapa Tanzania [emoji1241] uzalishaji wa mazao utaongeza endapo tuu tuna soko la kutosha na bei nzuri kama sasa, mengine ni mbwembwe tuuu. Yaani mwezi uliopita nilikuwa Mpanda maeneo ya jirani na Railways station nikakuta semi kibao za wafanyabiashara kutoka Kenya [emoji1139] wananunua mahindi sh elfu 16 mpaka elfu 18 kwa debe. Hivi mtu akijua kwamba akivuna gunia 200 atapata milioni zaidi ya 25 (ndani ya kipindi cha miezi 4) nani ataacha kulima mkuu?
 
Wewe ni mjinga kabisa. Tumelima kwa gharama zetu halafu kwenye kuuza mnatuletea upumbavu.
Kabisa mkuu, kuna watu wa ajabu sana aisee... Yeye akiongezewa mshahara hakuna anayempangia namna ya kutumia..
 
Acha kudanganya watu hapa, wakulima wengi wenye akili wameweka akiba ya chakula kwa sababu wana familia zao na wanajua hata ikitokea njaa nchi nzima hakuna mtu wa kuwapa chakula cha bure (nitajie mwaka ambao kulitokea njaa na serikali ikagawa chakula bure nchi nzima? Unakumbuka JPM aliwaambiaje kule Kagera baada ya kutokea tetemeko la ardhi??). Of course wapo wakulima wachache malofa, kama tuu ilivyo kwa wafanyakazi au wafanyabiashara, ambao watauza mazao yote na kwenda kulewa au kuhonga, kama ambavyo mfanyakazi anapokea mshahara wake na badala ya kununua mahitaji yake ya familia ya mwezi mzima, anaamua kuutapanya mshahara wake wote na kutesa familia. Nenda huko Katavi vijijini ndani ndani utakuta vihenge vimejaa mahindi, mipunga mpaka viazi vilivyokaushwa.
 
Wewe sio mkulima wala mfanyabiashara ni mtu wa hovyohovyo tu
Sasa kama huna pesa ya kununua mchele mzuri Supa kwa elfu 3 si ukachemshe hata mihogo au viazi vitamu fungu ni 500?? [emoji12] [emoji12] Acheni kulia lia hapa, kama vipi msimu ujao kalime na wewe... Wewe na Waziri Bashe na baraza zima la mawaziri nani kwenye akili na ambaye ni well informed??
 
Sasa ukiisha na bei kuwa hata 5000 wewe inakuuma nini hasa? Kuna ambaye amekuja kwako kukuomba chakula? Kama mimi nimevuna magunia 300 nikaona sasa bei ni nzuri nikauza magunia 250 na kubakiza akiba ya gunia 50 nyumbani kwangu wewe utaweza kujua kweli??
 
Japo wamechelewa lakini walau itasaidia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…