Tanzania yazindua Noti Mpya toleo la 2010 zenye Saini ya Waziri Mwigulu Nchemba na Gavana Emmanuel Tutuba

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba amesema kuwa Noti Mpya za Tanzania zenye Saini ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb) na yeye mwenyewe, za toleo la mwaka 2010, zitaingia kwenye mzunguko kuanzia tarehe mosi Februari mwaka huu.

Gavana Tutuba amesema hayo wakati akimkabidhi Mhe. Dkt. Nchemba, Noti kifani za shilingi elfu kumi, elfu Tano, Elfu Mbili na Shilingi Elfu moja, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam, kwa mujibu wa Sheria na Taratibu zinazosimamia masuala ya fedha nchini.

“Mheshimiwa Waziri, ninayofuraha kukujulisha kuwa zoezi letu la uchapaji upya wa Noti kwa marejeo ya toleo la mwaka 2010, limekamilika na tayari tumewajulisha wananchi kupitia taarifa niliyoitoa kupitia Gazeti la Serikali” alisema Bw. Tutuba.

Gavana Tutuba alifafanua kuwa Noti hizo zitatumika sambamba na Noti zilizopo hivi sasa, zinamwonekano wa Noti zinazotumika hivi sasa zilizotolewa Mwaka 2010, ikiwemo alama za usalama, ukubwa, rangi na mambo mengine, isipokuwa ina marekebisho kwenye saini ya Waziri wa Fedha, na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania.

“Saini ya aliyekuwa Waziri wa Fedha ambaye hivi sasa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango imebadilishwa na kuwekwa Saini yako Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba na Saini ya aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania aliyestaafu, Prof. Florens Luoga, imebadilishwa na kuwekwa Saini ya Gavana wa Benki Kuu wa sasa, Bw. Emmanuel Tutuba” aliongeza Bw. Tutuba.

Akizungumza baada ya kupokea sampuli za Noti hizo mpya, Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, alimshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu jambo hilo kufanyika na kumpongeza Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, kwa kusimamia mchakato wa uchapaji wa Noti hizo kwa weledi na uadilifu mkubwa.
View attachment 3210129

“Mpaka kufikia hatua hii ni heshima kubwa kwa Taifa letu na inaendeleza heshima ya wataalam wetu mnavyoweza kusimamia kwa umakini mambo yenye maslahi mapana kwa nchi yetu” Alisema Dkt. Nchemba.

Mhe. Dkt. Nchemba aliridhia Noti hizo ziingizwe kwenye mzunguko na kuanza kutumika kama ilivyopangwa tarehe moja Februari mwaka huu.
View attachment 3210142
Kwa nini hawajaweka picha ya Rais Samia?
 
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba amesema kuwa Noti Mpya za Tanzania zenye Saini ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb) na yeye mwenyewe, za toleo la mwaka 2010, zitaingia kwenye mzunguko kuanzia tarehe mosi Februari mwaka huu.
Utadhani saini zao ndio noti zenyewe.Tanzania hata raisi akiwa mbuzi tutafika TU.Hakuna wanalolijua viongozi wa kitz
 
Baada ya kushughulikia uchumi na upandaji wa dola kiholela wanauza sura
 
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba amesema kuwa Noti Mpya za Tanzania zenye Saini ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb) na yeye mwenyewe, za toleo la mwaka 2010, zitaingia kwenye mzunguko kuanzia tarehe mosi Februari mwaka huu.

Gavana Tutuba amesema hayo wakati akimkabidhi Mhe. Dkt. Nchemba, Noti kifani za shilingi elfu kumi, elfu Tano, Elfu Mbili na Shilingi Elfu moja, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam, kwa mujibu wa Sheria na Taratibu zinazosimamia masuala ya fedha nchini.

“Mheshimiwa Waziri, ninayofuraha kukujulisha kuwa zoezi letu la uchapaji upya wa Noti kwa marejeo ya toleo la mwaka 2010, limekamilika na tayari tumewajulisha wananchi kupitia taarifa niliyoitoa kupitia Gazeti la Serikali” alisema Bw. Tutuba.

Gavana Tutuba alifafanua kuwa Noti hizo zitatumika sambamba na Noti zilizopo hivi sasa, zinamwonekano wa Noti zinazotumika hivi sasa zilizotolewa Mwaka 2010, ikiwemo alama za usalama, ukubwa, rangi na mambo mengine, isipokuwa ina marekebisho kwenye saini ya Waziri wa Fedha, na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania.

“Saini ya aliyekuwa Waziri wa Fedha ambaye hivi sasa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango imebadilishwa na kuwekwa Saini yako Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba na Saini ya aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania aliyestaafu, Prof. Florens Luoga, imebadilishwa na kuwekwa Saini ya Gavana wa Benki Kuu wa sasa, Bw. Emmanuel Tutuba” aliongeza Bw. Tutuba.

Akizungumza baada ya kupokea sampuli za Noti hizo mpya, Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, alimshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu jambo hilo kufanyika na kumpongeza Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, kwa kusimamia mchakato wa uchapaji wa Noti hizo kwa weledi na uadilifu mkubwa.
View attachment 3210129

“Mpaka kufikia hatua hii ni heshima kubwa kwa Taifa letu na inaendeleza heshima ya wataalam wetu mnavyoweza kusimamia kwa umakini mambo yenye maslahi mapana kwa nchi yetu” Alisema Dkt. Nchemba.

Mhe. Dkt. Nchemba aliridhia Noti hizo ziingizwe kwenye mzunguko na kuanza kutumika kama ilivyopangwa tarehe moja Februari mwaka huu.
View attachment 3210142

Kubadilisha Noti za Fedha (Banknotes) kwa nchi nyingi za Magharibi huwa wanafanya pale tu kunapokuwa kuna UMUHIMU au ULAZIMA fulani, lakini katika nchi hizi za dunia ya tatu hasa nchi za Afrika zoezi hilo mara nyingi sana huwa linafanyika kukiwa na sababu za ajenda za Siri nyuma yake, hasahasa ni kwa sababu za wizi mkubwa wa kimtandao na ufisadi. Shuhuda nyingi sana zimethibitisha Ukweli kuhusu suala hili.

Mathalani, nchini Liberia, zabuni ya kuchapisha Noti mpya ilianzishwa wakati fulani hivi ili Watawala wachache walio wezi na Mafisadi wapate nafasi ya kuiba pesa. Makontena manne (4) yaliyobeba Noti mpya zilizochapwa kutoka kiwandani huko Ulaya yaliibwa yakiwa Bandarini katika Mji Mkuu wa nchi hiyo wa Monrovia. Makontena hayo ya Fedha yaliibwa na mpaka leo hajawahi kupatikana
 
Lengo ni kuongeza idadi ya noti kwenye mzunguko maana zitahitajika kwa wingi sana kwenye uchaguzi ujao
 
Ni jambo zuri ila limechelewa kufanyiwa jazi maana October uchaguzi na mambo yatabadilika.
Sawa Ila Halikuwa Na Umuhimu Wowote Zaidi Mlitaka Saini Zenu Ziwepo Tu
Yaani kuweka Saini zenu mnasema ni jambo lenye heshima kubwa kwa taifa? Aseee kwanza nani aliruhusu huu uhuni wa Saini ya waziri wa fedha kuwepo kwenye noti zetu?
Tuna viongozi wa hovyo kupata kutokea duniani,yumkini walishinikiza hili lifanyike haraka hasa huyo mwigulu njemba appearance yake ni mtu anaependa sana sifa.

Sawa, Noti mpya za Fedha tayari zimechapishwa, lakini waTanzania hatujaelezwa sababu hasa za msingi na zenye mashiko zilizopelekea kuchapishwa kwa Noti hizo mpya.
1. Zipi hasa sababu za msingi kabisa za kuchapishwa kwa Noti hizo mpya ikiwa Noti za awali zilizopo kwenye mzunguko bado zipo imara Sana hazijachakaa wala haziijachoka? What are the Motives behind for printing of these new Banknotes?
2. Kwa nini wameamua kuingiza kwenye mzunguko Noti hizo Mpya kwenye kipindi hiki kibaya wakati nchi ikiwa kwenye mzigo mkubwa zaidi wa Bajeti ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025? Kwa nini hasa wameamua kuwaongezea Wananchi mzigo wa Kodi ili kugharamia mchakato mzima wa uchapishaji wa hizo Noti Mpya? Je, kulikuwa na ULAZIMA sana wa kufanya hivyo katika kipindi hiki cha Bajeti ya Uchaguzi Mkuu?
3. Je, Gharama kiasi gani ambazo zimetumika kwenye mchakato mzima wa kuzalisha hizo Noti mpya?
Hivi kweli kulikuwa na ULAZIMA wa kufanya hivyo kweli??

Naona kama kuna mashaka makubqa sana kuhusiana na Mchakato wa Uchapishaji wa hizo Noti mpya. Hapakuwa na uwazi kabisa kwenye utekelezaji wa suala hili. Habari ya kuwepo kwa Noti mpya ilikuja kama shambulizi la kushitukiza "ambush". Wananchi hatukuwahi kutaarifiwa kabla kuhusiana na suala zima la uwepo wa Zabuni au kuwepo kwa nia ya kutaka kuchapisha noti Mpya.
Isije ikawa zoezi hilo limefanywa kwa nia ovu ya kupata Fedha zisizo haliali za kugharamia zoezi la uchaguzi Mkuu ujao wa Oktoba 2025. Kwa sababu Wahusika wanajua ni vigumu Sana kwa Wananchi kuweza ku-detect ufisadi kuhusiana na Fedha Mpya ambazo bado hazijawahi kuingia kwenye mzunguko wa Fedha unaodhibitiwa na Benki Kuu kwa sababu Fedha hizo Mpya zinakuwa bado hazijawa discounted na Benki Kuu.
 
Ni noti ya laki moja 100,000
Habari ndio hiyo.......
Kutokana na sababu za kiuchumi, haishauriwi kwa Mamlaka ya nchi yoyote ile ku-print Noti (Banknotes) zenye denominations kubwa sana namna hii, haifai kabisa hii kiuchumi. Kadiri denominators za Noti za Fedha zinavyokuwa kubwa, ndivyo thamani ya hiyo Fedha inavyokuwa ndogo, and vice versa is true.
Mifano hai kwenye suala hili ni nchini Zimbabwe ambako kutokana na inflation kuwa kubwa sana na Fedha yake kushuka thamani Sana kupita kiasi, Benki Kuu ya Zimbabwe kutokana na influence ya kisiasa kutoka kwa Robert Mugabe iliamua kuzalisha noti za Fedha zenye denominators kubwa sana katika viwango vya kuvunja rekodi ya dunia. Mathalani, walikuwa na Noti ya Fedha ya Zimbabwe Dola Trillioni Moja
(Zimbabwean Dollar 1, 000,000,000 )
 
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba amesema kuwa Noti Mpya za Tanzania zenye Saini ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb) na yeye mwenyewe, za toleo la mwaka 2010, zitaingia kwenye mzunguko kuanzia tarehe mosi Februari mwaka huu.

Gavana Tutuba amesema hayo wakati akimkabidhi Mhe. Dkt. Nchemba, Noti kifani za shilingi elfu kumi, elfu Tano, Elfu Mbili na Shilingi Elfu moja, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam, kwa mujibu wa Sheria na Taratibu zinazosimamia masuala ya fedha nchini.

“Mheshimiwa Waziri, ninayofuraha kukujulisha kuwa zoezi letu la uchapaji upya wa Noti kwa marejeo ya toleo la mwaka 2010, limekamilika na tayari tumewajulisha wananchi kupitia taarifa niliyoitoa kupitia Gazeti la Serikali” alisema Bw. Tutuba.

Gavana Tutuba alifafanua kuwa Noti hizo zitatumika sambamba na Noti zilizopo hivi sasa, zinamwonekano wa Noti zinazotumika hivi sasa zilizotolewa Mwaka 2010, ikiwemo alama za usalama, ukubwa, rangi na mambo mengine, isipokuwa ina marekebisho kwenye saini ya Waziri wa Fedha, na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania.

“Saini ya aliyekuwa Waziri wa Fedha ambaye hivi sasa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango imebadilishwa na kuwekwa Saini yako Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba na Saini ya aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania aliyestaafu, Prof. Florens Luoga, imebadilishwa na kuwekwa Saini ya Gavana wa Benki Kuu wa sasa, Bw. Emmanuel Tutuba” aliongeza Bw. Tutuba.

Akizungumza baada ya kupokea sampuli za Noti hizo mpya, Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, alimshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu jambo hilo kufanyika na kumpongeza Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, kwa kusimamia mchakato wa uchapaji wa Noti hizo kwa weledi na uadilifu mkubwa.
View attachment 3210129

“Mpaka kufikia hatua hii ni heshima kubwa kwa Taifa letu na inaendeleza heshima ya wataalam wetu mnavyoweza kusimamia kwa umakini mambo yenye maslahi mapana kwa nchi yetu” Alisema Dkt. Nchemba.

Mhe. Dkt. Nchemba aliridhia Noti hizo ziingizwe kwenye mzunguko na kuanza kutumika kama ilivyopangwa tarehe moja Februari mwaka huu.
View attachment 3210142
Zamani waziri wa Fedha alikuwa anaheshimika sana, hadi ukiona sign yake kwenye noti unakuwa "excited "
Njoo saizi sasa, hata kijana mdogo tu haeshimu tena!!
What has gone wrong???
 
Tuna viongozi wa hovyo kupata kutokea duniani,yumkini walishinikiza hili lifanyike haraka hasa huyo mwigulu njemba appearance yake ni mtu anaependa sana sifa.
Kubadili saini Ni kichaka tu.
Lengo ni kuchapisha pesa mpya huenda Kuna hali tete kwenye kibubu hakuna kitu.
 
Back
Top Bottom