Tanzania yazindua Noti Mpya toleo la 2010 zenye Saini ya Waziri Mwigulu Nchemba na Gavana Emmanuel Tutuba

Sawa, Noti mpya za Fedha tayari zimechapishwa, lakini waTanzania hatujaelezwa sababu hasa za msingi na zenye mashiko zilizopelekea kuchapishwa kwa Noti hizo mpya.
1. Zopi hasa sababu za msingi kabisa za kuchapishwa kwa Noti hizo mpya ikiwa Noti za awali zilizopo kwenye mzunguko bado zipo imara Sana hazijachakaa wala haziijachoka? What are the Motives behind for printing of these new Banknotes?
2. Kwa nini wameamua kuingiza kwenye mzunguko Noti hizo Mpya kwenye kipindi hiki kibaya wakati nchi ikiwa kwenye mzigo mkubwa zaidi wa Bajeti ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025? Kwa nini hasa wameamua kuwaongezea Wananchi mzigo wa Kodi ili kugharamia mchakato mzima wa uchapishaji wa hizo Noti Mpya? Je, kulikuwa na ULAZIMA sana wa kufanya hivyo katika kipindi hiki cha Bajeti ya Uchaguzi Mkuu?
3. Je, Gharama kiasi gani ambazo zimetumika kwenye mchakato mzima wa kuzalisha hizo Noti mpya?
Hivi kweli kulikuwa na ULAZIMA wa kufanya hivyo kweli??

Naona kama kuna mashaka makubqa sana kuhusiana na Mchakato wa Uchapishaji wa hizo Noti mpya. Hapakuwa na uwazi kabisa kwenye utekelezaji wa suala hili. Habari ya kuwepo kwa Noti mpya ilikuja kama shambulizi la kushitukiza "ambush". Wananchi hatukuwahi kutaarifiwa kabla kuhusiana na suala zima la uwepo wa Zabuni au kuwepo kwa nia ya kutaka kuchapisha noti Mpya.
Isije ikawa zoezi hilo limefanywa kwa nia ovu ya kupata Fedha zisizo haliali za kugharamia zoezi la uchaguzi Mkuu ujao wa Oktoba 2025. Kwa sababu Wahusika wanajua ni vigumu Sana kwa Wananchi kuweza ku-detect ufisadi kuhusiana na Fedha Mpya ambazo bado hazijawahi kuingia kwenye mzunguko wa Fedha unaodhibitiwa na Benki Kuu kwa sababu Fedha hizo Mpya zinakuwa bado hazijawa discounted na Benki Kuu.
Gharama na sababu za kuchapisha zitajwe, waache kupeleka kigizagiza , aah ! Hao ni ma PhD' s wajameni. . .
 
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba amesema kuwa Noti Mpya za Tanzania zenye Saini ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb) na yeye mwenyewe, za toleo la mwaka 2010, zitaingia kwenye mzunguko kuanzia tarehe mosi Februari mwaka huu.

Gavana Tutuba amesema hayo wakati akimkabidhi Mhe. Dkt. Nchemba, Noti kifani za shilingi elfu kumi, elfu Tano, Elfu Mbili na Shilingi Elfu moja, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam, kwa mujibu wa Sheria na Taratibu zinazosimamia masuala ya fedha nchini.

“Mheshimiwa Waziri, ninayofuraha kukujulisha kuwa zoezi letu la uchapaji upya wa Noti kwa marejeo ya toleo la mwaka 2010, limekamilika na tayari tumewajulisha wananchi kupitia taarifa niliyoitoa kupitia Gazeti la Serikali” alisema Bw. Tutuba.

Gavana Tutuba alifafanua kuwa Noti hizo zitatumika sambamba na Noti zilizopo hivi sasa, zinamwonekano wa Noti zinazotumika hivi sasa zilizotolewa Mwaka 2010, ikiwemo alama za usalama, ukubwa, rangi na mambo mengine, isipokuwa ina marekebisho kwenye saini ya Waziri wa Fedha, na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania.

“Saini ya aliyekuwa Waziri wa Fedha ambaye hivi sasa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango imebadilishwa na kuwekwa Saini yako Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba na Saini ya aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania aliyestaafu, Prof. Florens Luoga, imebadilishwa na kuwekwa Saini ya Gavana wa Benki Kuu wa sasa, Bw. Emmanuel Tutuba” aliongeza Bw. Tutuba.

Akizungumza baada ya kupokea sampuli za Noti hizo mpya, Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, alimshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu jambo hilo kufanyika na kumpongeza Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, kwa kusimamia mchakato wa uchapaji wa Noti hizo kwa weledi na uadilifu mkubwa.
View attachment 3210129

“Mpaka kufikia hatua hii ni heshima kubwa kwa Taifa letu na inaendeleza heshima ya wataalam wetu mnavyoweza kusimamia kwa umakini mambo yenye maslahi mapana kwa nchi yetu” Alisema Dkt. Nchemba.

Mhe. Dkt. Nchemba aliridhia Noti hizo ziingizwe kwenye mzunguko na kuanza kutumika kama ilivyopangwa tarehe moja Februari mwaka huu.
View attachment 3210142
Ufisadi na upumbavu wa kawaida.
 
View attachment 3210129

“Mpaka kufikia hatua hii ni heshima kubwa kwa Taifa letu na inaendeleza heshima ya wataalam wetu mnavyoweza kusimamia kwa umakini mambo yenye maslahi mapana kwa nchi yetu” Alisema Dkt. Nchemba.
Sijaelewa nukuu hii ya Mwigulu. Kuweka Saini zenu kwenye noti na kuondoa zilizokuwepo, kinaleta vipi heshma kwa Taifa letu na kusimamia maslahi ya Taifa letu?
 
Inaumiza sana kwa nchi masikini kuendelea kuwa na fikra za kimasikini, hivi kulikuwa na ulazima gani kubadili noti kisa saini ya waziri na Gavana? aliyeturoga sisi ni nani? mbona Marekani picha ya Dola na hizo saini ndio hizohizo miaka nenda rudi na thamani ya dola inakua siku hadi siku? sijaelewa sie watu weusi uwezo wetu wa kufikiri ukoje.
 
Mkuu kuna nn embu tueleze kwa kina
 
Mh! hivi wanabadili noti ama wanafungua bunda jengine la noti nakuanza kuzi print..?
Hivi unahabari noti zipo bank kuu ambazo hazijapewa namba na hazina sign!, hizo hauwezi hata kuzitumia mpaka zitiwe sign na zipewe number.
Mi nafikiri taarifa haijaeleweka vyema.
 
Ww hujui Mh moja ya ndoto zake tangu anasoma sign yake ikae kwenye fedha na ndoto imetimia namkubali sana watu na maono yao
 
Ujinga umaskini maradhi
Ujinga umaskini maradhi
Ujinga umaskini maradhi
Narudia
Ujinga umaskini maradhi
Ujinga umaskini maradhi
Ujinga umaskini maradhi
 
Inaumiza sana kwa nchi masikini kuendelea kuwa na fikra za kimasikini, hivi kulikuwa na ulazima gani kubadili noti kisa saini ya waziri na Gavana? aliyeturoga sisi ni nani? mbona Marekani picha ya Dola na hizo saini ndio hizohizo miaka nenda rudi na thamani ya dola inakua siku hadi siku? sijaelewa sie watu weusi uwezo wetu wa kufikiri ukoje.
Hapa utaitwa mchochezi na mpinga maendeleo ya Saini.
 
Inaumiza sana kwa nchi masikini kuendelea kuwa na fikra za kimasikini, hivi kulikuwa na ulazima gani kubadili noti kisa saini ya waziri na Gavana? aliyeturoga sisi ni nani? mbona Marekani picha ya Dola na hizo saini ndio hizohizo miaka nenda rudi na thamani ya dola inakua siku hadi siku? sijaelewa sie watu weusi uwezo wetu wa kufikiri ukoje.

Background kaka, mtu kakulia kuchunga ng'ombe mkimpa madaraka showoffs lazima, ndo maana wanataka magari ya 600m wawakoge maskini wa kule walipotoka bila kujali siku akipigwa chini atarudi kwenye ist japo wanaiba sana na kutunzia Dubai na Jersey au Mauritius na Swiss
 
Mkuu kuna nn embu tueleze kwa kina
avana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba amesema kuwa Noti Mpya za Tanzania zenye Saini ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb) na yeye mwenyewe, za toleo la mwaka 2010, zitaingia kwenye mzunguko kuanzia tarehe mosi Februari mwaka huu.

Back
Top Bottom