Tanzanialeaks apuuzwe, Hazina haijafilisika

Hauna mzuka wowote njaa inakuuwa tuu nyie ndiyo mkipewa madaraka mnaanza ufisadi wenu hatutak machawa kama nyie
 
ndugu waziri,
Chapa kazi tu,
kama Taifa tuna Imani na Dr. Samia Suluhu Hassan, lakini pia tuna Imani nawe katika kusimamia rasilimali na uchumi wa Taifa letu, kwa maslahi mapana ya waTanzania wote 🐒

daima tutawapuuza wazushi na waongo kama ulivyo shauri..

Mungu Ibariki Tanzania
 
Ndiyo vijana wenu hao halafu kesho kutwa amechaguliwa kuwa kiongoz kisa alikuwa anasifu na kuabudu
Mtegemee ataleta mabadiliko
Hii tabia ya uchawa ni mbaya sana
 
Hizi ni taarabu tu kama za khadija kopa na kina leyla Rashidi, sisi tukuamini vipi sasa...
Nyie wanasiasa mlivyo waongo, leta uthibitisho
 
Mganga wao mkali sana.
 
Watanzania siku hizi Wala hayo hayatuhusu, si tuna focus na yetu, hii nchi si yenu bana, tozo zetu,kikokotoo chetu, ukosefu wa ajira wetu, maisha magumu yetu. Nyie endeleeni kula Bata sisi tupambane na yetu. Kila mtu ashinde mechi yake.
 
😂😂😂 Hapo kwenye Dua mbaya kama kweli vile.
 
Wanatutwisha mizigo ambayo wao wenyewe hawaigusi hata kwa vidole vyao, malipo ya wakandarasi toka mwezi wa tano yamekuwa rejected, wakati huo huo TRA wao wanakaba walipwe, mabosi TRA wanajilimbikizia mali za za kutisha, wanamdanganya raisi wafanyabiashara wanakwepa kodi ili kumpumbaza raisi asiyaone maovu yao, ajabu raisi naye kanasa mtegoni, haya yote hatajibu kwani hayamuumizi yeye, lakini siku zinakuja atayajutia haya yote...😭😭😭😭😭
 
Mbona hamjalipa madeni ya wazabuni miezi 7 sasa
Anayaita madai ya wakandarasi madeni " "MADOGO MADOGO" my brother, munaumiza watu hamlipi, than unatoa kugha za kejeli?! Dharau?! Cha ajabu wapo wakandarasi hususan wa Dar, wanalipwa kiaina sijui wanapita njia/mbinu gani😭😭😭😭
 
Uko vizuri Dk. Waziri.
 
Nilikuwa sijui Mwigulu Nchemba yuko JF.
Nyie ndio watoto wa juzi na mmeharibu sana JF hii. Awali JF ilikuwa uwanja mpana sana wa majadiliano bila woga na kuheshimiana na karibu Mawaziri wote senior walikuwa humu, wanasiana wote mashuhuri na watendaji wa taasisi zote uzijuazo na taasisi zenyewe zikawa na page zake.
Lakini vijana wa kitanzania wa hovyo mkaingia humu na matusi na kejeli hivyo jukwaa likadharaulika.
Kulikuwa kukishushwa nondo zilizoshiba za kina DR Slaa na ma profesa kadhaa hadi unasahau kazi ili usome hoja.
Sasa wamejaa kina Lucas Mwashambwa & company JF imekuwa kikundi cha kwaya ya mapambio na kuabudu utadhani watu tumekatwa vichwa!
 
Hizi ni taarabu tu kama za khadija kopa na kina leyla Rashidi, sisi tukuamini vipi sasa...
Nyie wanasiasa mlivyo waongo, leta uthibitisho
That's very true mkuu. Huyu waziri kwa maelezo yake tunamtofautisha vipi na jamaa wa TanzaniaLeaks? Unapinga uongo kwa kutuletea porojo tena msomi wa PhD, unataka tukuelewe vipi?
 
Hata Raisi wetu Samia Suluhu Hassan ajiunge na JF sio kusoma tu awe anapangua Hoja zetu kuhusu mambo mbali mbali yanalolihusu hil Taifa letu.
Hii ingekuwa jambo jema sana kwake kwa namna alivyozungukwa na wahuni.
Angejiongezea upeo kurahisisha namna anavyopaswa kuongoza nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…