Tanzanialeaks apuuzwe, Hazina haijafilisika

Tanzanialeaks apuuzwe, Hazina haijafilisika

Nyie ndio watoto wa juzi na mmeharibu sana JF hii. Awali JF ilikuwa uwanja mpana sana wa majadiliano bila woga na kuheshimiana na karibu Mawaziri wote senior walikuwa humu, wanasiana wote mashuhuri na watendaji wa taasisi zote uzijuazo na taasisi zenyewe zikawa na page zake.
Lakini vijana wa kitanzania wa hovyo mkaingia humu na matusi na kejeli hivyo jukwaa likadharaulika.
Kulikuwa kukishushwa nondo zilizoshiba za kina DR Slaa na ma profesa kadhaa hadi unasahau kazi ili usome hoja.
Sasa wamejaa kina Lucas Mwashambwa & company JF imekuwa kikundi cha kwaya ya mapambio na kuabudu utadhani watu tumekatwa vichwa!
Si akina Lucas tu. Hata baadhi ya wakosoaji wa watawala wanaandika kichawa.
 
Duuuh kweli watu wana njaa
Kwani umeshindwa nn kumuomba hiyo hela ya kula bila kumsifia uongo wako hapa

Huu uchawa utawamaliza jaji warioba aliwaambia vijana achaneni na uchawa mnaharibu nchi

We jamaa huwa unajitapa sana kule MMU kumbe njaa kali hivii
Unamuomba waziri buku tano ya kula?
Badala ya kazi
Kwani unaumia wapi nikiomba hiyo buku 5 ya maji mkuu...😜
Na ukweli ni kwamba waziri anafanya kazi nzuri na huku mtaani anapendwa kuliko unavyo fukiria, hasa alipo punguza kodi kwa mwananchi na akapndisha thamani ya shilingi..🤣
 
Hahahaha 🤣🤣 yanatoa maziwa?
Halafu unakuja hapa kumuomba waziri buku tano ya kula?

Hakika ningekuwa mimi sikupi hata mia mbovu maana wewe ni mjinga
Unafikir ukiomba kitu bila kusifia uongo hutapewa

Hii ni aibu kuwa na vijana wa ovyo kama wewe
Mnatia kinyaa kabsaa
Tatizo vijana hampendani, punguzeni kumuonea waziri kijana wivu....😜
Waziri oyeeeeeee......🤣
 
Puuzeni taarifa ya “Tanzanialeaks” Serikali haijafilisika, Ameandika hatujalipa Bwawa - Uongo mtupu, Bwawa la Mwl Nyerere hatudaiwi hata Invoice Moja na Wiki jana tumewasha na mtambo wa 7, ( Sasa tumeshawasha 7, 8 & 9 kila mmoja 235MW).

Ameandika kuhusu Yapi, hawa walikuwa na matatizo madogo kama kampuni nayo yanaendelea kutatuliwa, Malipo yameendelea kulipwa kwenye Sekta zote na mengine yapo kwenye hatua za mwisho za malipo. Waongo buana amesahau kwamba ndio tuko wiki ya pili ya mwaka mpya wa Fedha. Puuzeni ni wale wale wenye kututakia mabaya.

Tulimiss hii me X yako kitambo😃😃😃kwakua unaongelea pesa za umma ungeweka na viambatanisho vya malipo ingependeza sana muheshimiwa ili walipa kodi tuwe na uhakika kuliko maneno matupu
 
Nchi hii chadema na wafuasi wao ni wapotoshaji Sana nadhani kwasababu hawajabadilisha mwenyekiti wao kwa muda mrefu.
Wangejiuliza wenyewe kwanza haya maswali;
👉🏿Ruzuku za miaka ya nyuma walizoandika kuomba si walipewa zote bil. 2.73, Jibu ni NDYO
👉🏿Ruzuku si wanapokea kila mwezi ingawa matumizi ndo hatujui🤣🤣 jibu ni NDIYO
Sasa kwann wafuasi wa chadema ni wapotoshaji Sana wanapata nn kupitia upotoshaji wao?
Tumewachoka CHADEMA🚮
Ruzuku ni haki yao sio hisani jibuni hoja zamsingi na hapo CDM wanahusika vipi sasa?
 
Sisi wabongo ni watu wa husda chapa kazi kaka Mwigu, kazi yako imetukuka na Tanzania yote inabubujikwa machozi ya furaha kwa uhodari wenu Mheshimiwa
 
Ndiyo vijana wenu hao halafu kesho kutwa amechaguliwa kuwa kiongoz kisa alikuwa anasifu na kuabudu
Mtegemee ataleta mabadiliko
Hii tabia ya uchawa ni mbaya sana
Ndio maana hili taifa kuendelea itakua ngumu sana.
 
Walidhani ni zamu yao ya kula na kufilisi nchi sasa nchi imefilisika kweli

Wamenunua majumba Dubai na kufungua offshore accounts nje

Wanatamani kukimbia nchi lakini uzuri ni kwamba tutazama wote pamoja

Ndo mjue akili ya mtu mweusi ilivyo
Anaharibu na kunya anapolala

Ccm mmeiharibu nchi beyond repair
 
Mheshimiwa Waziri;

Kwanza kabisa Nafurahi kwamba UPO hapa na uko Verified.Natamani sana Viongozi wote wa Kisiasa wangelazimika/Kuamua kuja hapa Jukwaani na Kuingia katika Mijadala Pale muda unaporuhusu.Pia nimefurahi kwamba Umetumia Jukwaa hili kuweka wazi kwamba Hazina Haijafilisika na kwamba Nchi ina PESA za kutosha.


Natambua kwamba Wewe ni Mchumi wa Daraja la Kwanza na hivyo basi sina shaka nikisema kwamba Hazina Yetu iko kwenye Mikono Salama.

Pamoja na Utangulizi wangu huu sasa naomba nishiriki katika Mjadala huu kuhusu Taarifa Uliyoiweka Hapo inayotokana na Tanzania LEAKS.Niseme tu ukweli kwamba Baada ya Kusoma andiko na kuona kwamba Tanzania Leaks anaonya Kwamba Serikali imefilisika Nikashangaa sana.Nimeshangaa kwa sababu Kwenye Taarifa kuna Contradicting Information kwamba kuna Wakandarasi ahwajalipwa Tangu january na pia akasemakuna Ujambazi unafanywa na TRA(Which Means Wanakusanya Pesa) na mwisho akasema pia kwamba kuna Misafara ya Magari 200 which means Pesa ya kuendesha NCHI IPO maana magari yanaendesha na yote ni Zero Kilomita.

Sasa mheshimiwa.Mimi ni Mchumi wa Daraja la SABA na nina kaulewa kadogo sana Kauchumi wa serikali.Kwa Mfano ninatambua kwamba Serikali Kufilisika Huwa kuna Tafsiri nyingi ili kufilisika kwa Serika ni Ama Imeshindwa kukusanya Mapato kutoka katika Vyanzo vyake vya ndani na Nje au mapato yanakusanywa na Kisha yanaingia kwenye Mifuko ya Wachache.

Mm kama Mchumi wa Daraja la SABA naweza kusema kwamba kwa nionavyo Ninyi kama Serikali Mnafanya kazi yenu kwa kadiri ya UWEZO wenu ila Hamjaweza kufikia Matarajio ya Watanzania.Ninaona Miradi mingi sana ya Miundo mbinu inaendelea ni Jambo ZURI ila mnapoona chokochoko bdo zipo basi ni lazima mtambue kwamba Watanzania wanataka ZAIDI.Usiwalaumu wala kuwasema wala kuwachukia kwa KUTAKA ZAIDI.

Ujumbe wa Tanzania LEAKS unaweza kuwa ni Tahadhari ndogo inayoonesha hatari itakayokuja huko Mbele kama Tusipofanya Spending check.Lakini Pia Ujumbe huo Pia unaweza kuwa unaonesha kwamba Usimamizi wa Matumizi mabaya uko Vizuri kiasi kwamba Watumishi wa Hazina kama huyo mtoa Taarifa wao hawana tena mirija ya upigaji.

Ushauri wangu ni nini?

Kwanza kabisa, Serikali ifanye Explicity Austerity Measures hasa kwa Upande wa Viongozi wa Kisiasa.Pili Tuepuka kabisa hii tabia ya KUZINDUA Mradi wa MILIONI 10 ila gharama za UZINDUZI zinakuwa MILIONI 20.Hii ni moja kati ya tabia ambazo ninaziona bado zipo.Kuliko kufanya Ujinga wa namna hiyo ni BORA Miradi isizinduliwa kwa Mbwembwe.

Kuna Mengi sana ambayo naweza kuandika hapa ila kwa leo niishie hapa.Ukiendelea kuwa mwenyeji Jukwaani naamni kabisa nitaanza kuweka nyuzi ambazo zinachangia zaidi taifa letu kwenda Mbele;


PS.Ongeza Bidii katika kusimamia matumizi Sahihi ya Rasilimali PESA zetu.Msifuje PESA zetu maana Tunawatazama,Tunawaona na Tunawafuatilia.

Mungu Akubariki.
 
Back
Top Bottom