Tanzanian actor Steven Kanumba reported dead

Tusiwe wepesi kuhukumu jamani, sbb wote tunatenda dhambi na tumepungukiwa na utukufu wa Mungu. Kila kitu ni neema tu. Pia sisi tuna dhambi ambazo wengi hawazijui na hatujui lini zitatuumbua na kwa style ipi.

So, lulu ni mmoja wa watenda dhambi km sisi, na kanumba safari yake ya mwisho imeshatimia, hata tuseme nini hawez rudi. Hivyo tuache kuwa judgmental kihivyo. Msiba huu na hatima ya Lulu itusaidie kujifanyia self assessment ya jinsi tunavyoenenda, na kubadilika ili kujiandalia maisha ya baadae baada ya kifo.

Tumwache Mungu ahukumu mwenyewe.

R.I.P KANUMBA.
 
Makamanda wako Arusha wanashugulikia mustakabari wa taifa letu. Tumeambiwa jamaa atazikwa wiki ijayo kwa hiyo wanao muda wa kutosha kwenda kushiriki msiba na mazishi. Pia haya mambo yanategemeana na MILa, inawezekana wewe KIM kwenu mkipata msiba mnaacha kila kitu na kuanza kulia tu.
 
Ujinga mtupu, Kwanza hakuwa na adabu wala heshima hata kwa wazazi wake (mnakumbuka alivyokuwa najibishana na baba yake mzazi kuwa hakumlea), hivi hiyo ni akili kweli au kupata tujisenti ndo ishu. ukipata mtu wa kukufikisha hata miaka 5 tu ili uweze kuwa angalau ombaomba mtaani ni wa kumshukuru. He wasnt responsible so he he desearved it, ulitegemea aishi miaka mingi ya nini. RIP anyway
 

wa chadema wameiweza hiyo protocal "ndogo" unayoiita,wmaekwenda pale ubalozini au wako busy kushangilia ushindi wa arumeru mashariki na posho kuongezeka chamani na kuota uchaguzi wa ubunge wa arusha mjini?
 

Kwa mila za kichagga mnafanyaje labda mnapofikwa na misiba au ni mbege tu???
 
Una picha yeyote labda?






Acha ku-politicise msiba wa Kanumba. Kanumba ni private person aliyeishi kwa 'public work - Entertainer' Watanzania wote tunaothamini kazi ya Kanumba tumeguswa na msiba huu bila ya kujali itikadi zetu. Huku ni kufilisika kisiasa. Kuna wanaoomboleza kimyakimya. RIP my bro Steve Kanumba
 
Msiba hauzoeleki. Pole sana mama, MUNGU akupe ujasiri ktk kipindi hiki kigumu.
 
mbona watu mnaleta mambo ya kis**** watu waache program zao kwa msiba wa kanumba?mlitaka chadema wote waache mambo yao waje msibani?
 

Na yule mbunge wenu aliyepata ajali je,mbona mlideka sana na ule msiba wake mkitaka taifa zima liingie msibani kisa kafa mbunge wa viti maalum kupitia chadema.Ukweli ni kwamba kanumba alikua mtu maarufu na miongoni mwa wapenzi na mashabiki wake ni wanachadema
 
maneno yako yamenigusa kiongozi,ee mungu niumbie nafsi mpya nikujue,nikuhushimu nikuabudu,nikupende na mwisho nitimize wajibu ulionipa,R.I.P. KANUMBA
 
tusi-conclude kirahisi hivyo kua kauwawa na mpenzi wake.Angefia hospitalini nafkiri mgesema uzembe wa madaktari ndio uliosababisha kifo. Tusiwe wepesi kuwajaza watu taarifa za uongo. wote hatujui exactly kilichotokea,ngoja wataalam(polisi na madaktari) watuambie baada ya uchunguzi.
 
Mwingine ataibuka na swali "Tume ya Katiba imeupokeaje msiba wa Lanumba?"
 
Sina uhakika na hayo usemayo Mphamvu ila naomba unifahamishe. Hiyo title ya thread yako ni kispaniola au kifaransa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…