Tanzanian actor Steven Kanumba reported dead

Tanzanian actor Steven Kanumba reported dead

Tusiwe wepesi kuhukumu jamani, sbb wote tunatenda dhambi na tumepungukiwa na utukufu wa Mungu. Kila kitu ni neema tu. Pia sisi tuna dhambi ambazo wengi hawazijui na hatujui lini zitatuumbua na kwa style ipi.

So, lulu ni mmoja wa watenda dhambi km sisi, na kanumba safari yake ya mwisho imeshatimia, hata tuseme nini hawez rudi. Hivyo tuache kuwa judgmental kihivyo. Msiba huu na hatima ya Lulu itusaidie kujifanyia self assessment ya jinsi tunavyoenenda, na kubadilika ili kujiandalia maisha ya baadae baada ya kifo.

Tumwache Mungu ahukumu mwenyewe.

R.I.P KANUMBA.
 
Makamanda wako Arusha wanashugulikia mustakabari wa taifa letu. Tumeambiwa jamaa atazikwa wiki ijayo kwa hiyo wanao muda wa kutosha kwenda kushiriki msiba na mazishi. Pia haya mambo yanategemeana na MILa, inawezekana wewe KIM kwenu mkipata msiba mnaacha kila kitu na kuanza kulia tu.
 
Ujinga mtupu, Kwanza hakuwa na adabu wala heshima hata kwa wazazi wake (mnakumbuka alivyokuwa najibishana na baba yake mzazi kuwa hakumlea), hivi hiyo ni akili kweli au kupata tujisenti ndo ishu. ukipata mtu wa kukufikisha hata miaka 5 tu ili uweze kuwa angalau ombaomba mtaani ni wa kumshukuru. He wasnt responsible so he he desearved it, ulitegemea aishi miaka mingi ya nini. RIP anyway
 
Hizi mbio za Urais za CCM zitawapeleka pabaya sana, yaani huo msiba unnataka kugeuzwa Siasa!!......Namsubili Laigwan Lowasa naye sijui anakuja lini kusaini huo msiba. usikute hawa CCM hata protocal ndogo tu ya kwenda kutia saini kitabu cha Maombolezo pale Ubalozi wa Malawi imewashinda, wao wanaota Urais tu Vilaza hawa.

wa chadema wameiweza hiyo protocal "ndogo" unayoiita,wmaekwenda pale ubalozini au wako busy kushangilia ushindi wa arumeru mashariki na posho kuongezeka chamani na kuota uchaguzi wa ubunge wa arusha mjini?
 
Makamanda wako Arusha wanashugulikia mustakabari wa taifa letu. Tumeambiwa jamaa atazikwa wiki ijayo kwa hiyo wanao muda wa kutosha kwenda kushiriki msiba na mazishi. Pia haya mambo yanategemeana na MILa, inawezekana wewe KIM kwenu mkipata msiba mnaacha kila kitu na kuanza kulia tu.

Kwa mila za kichagga mnafanyaje labda mnapofikwa na misiba au ni mbege tu???
 
Una picha yeyote labda?




IMG00214-20120407-0812.jpg


Acha ku-politicise msiba wa Kanumba. Kanumba ni private person aliyeishi kwa 'public work - Entertainer' Watanzania wote tunaothamini kazi ya Kanumba tumeguswa na msiba huu bila ya kujali itikadi zetu. Huku ni kufilisika kisiasa. Kuna wanaoomboleza kimyakimya. RIP my bro Steve Kanumba
 
Msiba hauzoeleki. Pole sana mama, MUNGU akupe ujasiri ktk kipindi hiki kigumu.
 
mbona watu mnaleta mambo ya kis**** watu waache program zao kwa msiba wa kanumba?mlitaka chadema wote waache mambo yao waje msibani?
 
Wewe na akili zako za kujaza kizibo cha bia huwezi kuona mbali. Nenda shule ndio utaelewa zaidi.
By the way huyo kanumba wako alilifanyia nini taifa letu? hamna na kifo chake ni kama maelfu ya watanzania wanaokufa kila siku. Sioni kwanini apewe special treatment na hao wanasiasa wanaoenda hapo usifikirie wameguswa na 'mtu muhimu' aliyekufa. Wako kazini. RIP Kanumba.

Na yule mbunge wenu aliyepata ajali je,mbona mlideka sana na ule msiba wake mkitaka taifa zima liingie msibani kisa kafa mbunge wa viti maalum kupitia chadema.Ukweli ni kwamba kanumba alikua mtu maarufu na miongoni mwa wapenzi na mashabiki wake ni wanachadema
 
maneno yako yamenigusa kiongozi,ee mungu niumbie nafsi mpya nikujue,nikuhushimu nikuabudu,nikupende na mwisho nitimize wajibu ulionipa,R.I.P. KANUMBA
 
Clouds fm live dakika zilizopita mtu aliepo nyumbani kwa marehemu, watu wanazidi kufika ndugu zake bado hawajafika.

Kanumba alikuwa anaoga wanavyodai majirani saa sita usiku alitoka bafuni kuingia chumbani eti akamkuta Lulu anaongea simu ya mapenzi na mwanaume mwingine, wakagombana na akasukumwa na kuangukia kujigonga kichwa na ndio kilichosababisha kifo chake. sasa msemaji amesema kuwa hii ndivyo inavyoelezwa pale na wanasubiri wataalamu watoe taarifa yao, inaelekea ugomvi ulikuwa mkubwa kati yao hadi majirani walisikia.

Kwa hiyo kwa sasa ni kauawa na Mpenzie

RIP
tusi-conclude kirahisi hivyo kua kauwawa na mpenzi wake.Angefia hospitalini nafkiri mgesema uzembe wa madaktari ndio uliosababisha kifo. Tusiwe wepesi kuwajaza watu taarifa za uongo. wote hatujui exactly kilichotokea,ngoja wataalam(polisi na madaktari) watuambie baada ya uchunguzi.
 
Mwingine ataibuka na swali "Tume ya Katiba imeupokeaje msiba wa Lanumba?"
 
Sina uhakika na hayo usemayo Mphamvu ila naomba unifahamishe. Hiyo title ya thread yako ni kispaniola au kifaransa?
 
Back
Top Bottom