Tanzania's GDP: Hivi tunajua hili?

Tanzania's GDP: Hivi tunajua hili?

Mwalimu Agustine naheshimu sana mawazo yako, lakini naomba urudie tena bandiko la BOB hapo juu. Linajieleza.

Hivi mwalimu nchi yenye informal sector ni Tanzania tuu? Somalia, Uganda, Burundi, Liberia, Papua New Guinea, Cape Verde na kwingineko..hawana hiyo sector isiyo rasmi? au sisi kama Tanzania tuna vigezo vyetu spesheli? WHY WE?????? NOT CAMEROON AU MAURITANIA?

Kama alivyosema BOB. ni kweli uchumi wetu mwingi uko informally (Mkapa aliliona hili mpaka akamleta De Soto wa Peru..na akaanzisha Mkurabita..kurasimisha mali zisizo rasmi). Kwa hiyo unless una datas nyingine..kwa hili tukubali tuu pato letu ni $600!.

By the way hiyo $600 inafanya assumptions... lakini hakika nakuambia kuna mamilioni ya watanzania wanakata hata mwaka hawajapata hata $50! NADHANI UNANIELEWA...

Huwezi ukalima mpunga ukategemea mahindi! Leo watanzania tunaiba mpaka hela ya ukimwi iliyotolewa na Bush..harafu tunasema kwamba World Bank wanataka kutufanya inferior? Tumeshindwa kabisa kutumia mali asili zetu kujikomboa...

Hapana mkuu. World Bank haina kosa. Hiyo hali tumejitakia wenyewe (viongozi na wananchi). Viongozi kwa kushindwa kutekeleza wajibu wao na wananchi kwa kushindwa/kuwa wavivu wa kuchagua viongozi bora au kuwawajibisha kwa kuwanyima kura!.


Turudi nyuma, tukae chini, tuanze upya! Hatuna hoja kuilaumu World Bank kwa hili!
 
Hapo viongozi wetu na sisi wenyewe watakapokubali kuwa sisi ni MASKINI wa kutupwa ndiyo nuru itaanza kuingia ndani ya nchi yetu. Watakapokubali na kukasirika kwa nini tumekuwa hivyo ndiyo safari yetu itakapoanza. Leo tunajitetea kuwa informal sekta haijajumuishwa! Kama alivyouliza Masanja, hiyo informal sekta iko Tanzania peke yake? Hivi wenzetu mnasafiri nje ya Dar es Salaam? Na mkiwa Dar es Salaam mnatembelea sehemu mbali ya Masaki?

Watu kandambili ndiyo kiatu cha kutokea. Na ikikatika, inashonwa! Na hawa ndio waliobahatika!
 
Hapo viongozi wetu na sisi wenyewe watakapokubali kuwa sisi ni MASKINI wa kutupwa ndiyo nuru itaanza kuingia ndani ya nchi yetu. Watakapokubali na kukasirika kwa nini tumekuwa hivyo ndiyo safari yetu itakapoanza. Leo tunajitetea kuwa informal sekta haijajumuishwa! Kama alivyouliza Masanja, hiyo informal sekta iko Tanzania peke yake? Hivi wenzetu mnasafiri nje ya Dar es Salaam? Na mkiwa Dar es Salaam mnatembelea sehemu mbali ya Masaki?

Watu kandambili ndiyo kiatu cha kutokea. Na ikikatika, inashonwa! Na hawa ndio waliobahatika!

Mkuu tupo ukurasa mmoja kabisa
Kama mtu unaumwa utajitahidi na ikikushinda mwenyewe utamuona Daktari
 
Kama definition ya GDP, ambayo ni

the total market value of all final goods and services produced in a country in a given year

mnaikubali basi sioni kwanini msione yafuatayo:

Sehemu kubwa ya "goods and services" zinazozalishwa na Watanzania hazioorodheshwi na kupata thamani yake kwani haziko katika uchumi rasmi.

Wakata nywele, mama ntilie, makondakta, watumishi wa ndani, wauza nyama mabuchani vijijini, machinga, etc ni sehemu kubwa sana ya wazalisha mali Tanzania, lakini mchango wao hauko kweye hilo li-GDP lenu.

Please ! ina maana nchi nyingine hawana setor isiyo rasmi
Kwa taarifa yako hizo seka ndio waanadlilishwa kuliko zote uenda kukata leseni TRA
TRA wanataka ulipe kodi kwanza halafu ufanye biashara hii sio fair itabidi tuanzishe thread yake
Yaani TRA wanchukua chao mapema katika mtaji wewe utajijua wakati wafanya biashara wakubwa wana enjoy Tax holiday ambayo unaweza kuitransfer kabla ya miaka mitano mfano Sheraton,to Movenpick and may more
 
Just to put this in perspective

GDP yetu ya 2006 (PPP) ilikuwa some $ 29 billion, deni la Lehman brothers ilipofile chapter 11 lilikuwa $ 613 billion na ilikuwa na assets za $ 639 billion.

Deni la Lehman brothers lilikuwa zaidi ya mara 21 ya GDP (PPP) yetu ya 2006!

Assets za Lehman Brothers zilikuwa zaidi ya mara 30 ya GDP (PPP) yetu ya 2006
 
Just to put this in perspective

GDP yetu ya 2006 (PPP) ilikuwa some $ 29 billion, deni la Lehman brothers ilipofile chapter 11 lilikuwa $ 613 billion na ilikuwa na assets za $ 639 billion.

Deni la Lehman brothers lilikuwa zaidi ya mara 21 ya GDP (PPP) yetu ya 2006!

Assets za Lehman Brothers zilikuwa zaidi ya mara 30 ya GDP (PPP) yetu ya 2006

Au kwa mtazamo mwingine, Bill Gates, Warren Buffet, Slim wote wana njuruku kuliko GDP yetu! Hapo hatujaanza hata kuangalia kampuni zao. Wote hawa wakipoteza kiasi kama GDP yetu, bado watakuwa matajiri wa kutupa. Tusipoangalia, hivi karibuni Oprah na Jay-Z nao watatupita! Watu karibu milioni 40 tunashindwa na mtu mmoja!
 
Au kwa mtazamo mwingine, Bill Gates, Warren Buffet, Slim wote wana njuruku kuliko GDP yetu! Hapo hatujaanza hata kuangalia kampuni zao. Wote hawa wakipoteza kiasi kama GDP yetu, bado watakuwa matajiri wa kutupa. Tusipoangalia, hivi karibuni Oprah na Jay-Z nao watatupita! Watu karibu milioni 40 tunashindwa na mtu mmoja!

hahaha!! fundi mchundo umenifurahisha sana...yani Kijana Jay Z anaweza akatukata ivi ivi..dah! kweli tumechoka..ila sijui kwanini Watanzania tunapenda kulalamika tu na action hamna....sijui ni lini tunazionesha hisia zetu kwa vitendo..? nadhani hapo ndipo tutakapojikomboa..
 
Ndg Mtarajiwa,
Nashukuru kwa kisehemu hicho toka kwenye hiyo module.LAKINI NAPENDA NIKUHAKIKISHIE KUWA MWANDISHI WA MODULE HIYO ALIACHA MAMBO MEEEENGI SANA YA KUZUNGUMZIA JUU YA INDICAROTORS OF ECO DEV na akasite vijisehemu tu vya kuandika ili asambaze module hizo ili watu wasomee somo la GS huko vyuoni hasa Diploma za ualimu.kimsingi alifanya biashara.

Kumbuka kuwa hiyo module ilitokana na ile warsha ya bagamoyo na watu walikaa mwezi mzima.Mimi baada ya kuona kijimodule hicho kidogo nitapike kwani aliandika utadhani ana-account for something.

Nashangaa sana unavyobisha juu ya GDP na kubeza world Bank wakati wewe unatupa reference ya module ya warsha ya Bagamoyo.I cant picture it.

Tukisema vigezo vya maendeleo ya kiuchumi vipo vingi sana lakini baba lao ni GDP.Nikirudi kwako nashangaa huweki hizo indicators unazodai zipo bali unabeza tu.Labda nikukumbushe kuwa ukiwa unajadili usije ukafananisha na Indicators of poverty japo zinashabiana SANA.Sitorudia haya hapa chini:-
-GD
-Life expectanc
-Literacy
-Measures of poverty
-Disease
-Mortarity rate na vifo vya watoto wachanga.

mimi nakubali wazi kuwa Tanzania ni masikini.Nashauri tuache kubisha kwa ajili tu ya siasa bali huo ndo ukweli.Mimi nataka kuangalia baadhi ya sababu zilizo fanya Tanzania tuwe masikini wa kunuka kiasi hiki.

1:WAKATI WA NYERERE
Sababu kubwa iliyotufanya tuwe masikini ni Nyerere na ujamaa wake aliotulazimisha kuuabudu ana kuunga huku ukikinzana na ujamaa nyingine huku akituletea maazimio meengi yasiyo na kichwa wala miguu na kutufanya tumuogope hata kumbishia ama kumwelekeza na kusababisha kuwepo na pengo kubwa kati ya watawala na watawaliwa huku tukiwaogopa kama miungu mtu.kifupi sababu ya kuwa masikini kipindi hiki ni Ujamaa na kujitegemea wa nyerere.

2:WAKATI WA MWINYI:
Serikali haikuwa makini na iliendeshwa utafikiri hapakuwa na wasomi wala watu wa kuongoza.Bra bra nyiiiingi huku mfumko wa bei na kushuka kwa thamani ya hele yetu kukiwa na kasi ya ajabu.

3:WAKATI WA MKAPA.
Serikali ilikuwa MAKINI sana na uchumi wetu ulikuwa SANA tofauti sana na awamu 2 zilizomtangulia.Hapa hakuna ubishi.Uchumi uliimarika na thamani ya hela yetu ilikuwa imara na alidhibiti mfumko wa bei.(Najaribu kumlinganisha mkapa na waliomtangulia pia aliyepo sasa) simlinganishi na waTZ wote tafadhari.Shida inayokuja sasa tumeweka siasa nyiiingi kiasi kwamba sasa hivi mkapa anaonekana kama choo popote litamkwapo jina lake.Lakini ukweli ni kuwa huyu baba wa watu upande wa Uchumi ALIJITAHIDI.

[HTML]4:WAKATI HUU WA KIKWETE.
Hapa hakuna kitu.Sioni hata moja la ku-comment.Silaumu siasa yake kwani hana siasa,wala Ujamaa wake kwani hana ujamaa,wala maazimio yake kwani hana maazimio.USANII TU NA KUCHEKA CHEKA.Inakera sana kuona anapokea nchi ikiwa imara toka kwa Mkapa sasa imekuwa utafikiri danguro.Hivi kwa nini mlimchagua nyie watanzania nyie?????enough is enough.2010 yaja.

[/HTML]
HITIMISHO.
Mambo yote yameongelewa huko juu ila shida ni UONGOZI SAFI ndo hatuna.Tuanazijua indicators zoote za uchumi,indicators zote za poverty na jinsi ya kuzishughulikia.Tuna raslimali nyiingi tu,Watu,Siasa,na Elimu Swafi kabisa.Huwezi kusema sisi ni wajinga wakati tuna mavyuo makuu sijui mangapi tuu na watu kila mwaka wanamaliza pale.Tuchague viongozi imara na thabiti ili watuwekee strategies bora za maendeleo.
Mkishindwa njooni tuvue samaki huku majita


Hapo kwa Kikwete umenifurahisha sana Mkuu......
 
Just to put this in perspective

GDP yetu ya 2006 (PPP) ilikuwa some $ 29 billion, deni la Lehman brothers ilipofile chapter 11 lilikuwa $ 613 billion na ilikuwa na assets za $ 639 billion.

Deni la Lehman brothers lilikuwa zaidi ya mara 21 ya GDP (PPP) yetu ya 2006!

Assets za Lehman Brothers zilikuwa zaidi ya mara 30 ya GDP (PPP) yetu ya 2006

This is shocking....
 
Wakati tunaongelea kuporomoka kwa uchumi wa Dunia na kushuka kwa thamani ya shilingi, kuna hili nimeliona tena kutoka kwa Kikwete ambalo amelifanya kuwa ni shina la maendeleo la Taifa la Tanzania na hata jumuiya za kiuchumi.

Akihutubia mkutano mjini Kampala majuzi, Kikwete katoa kauli kuwa COMESA, SADC na EAC zijiunge na kuwa na mshikamano wa kiuchumi hata kisiasa.

Hilo ni sawa kabisa, linalonitatiza mimi ni kung'ang'ania kwa Kikwete kusema kuwa tuwe na soko huria (free market and free trade) na kuongeza kutegemea sekta binafsi.

Kikwete na hata Mkapa walijijenga kwa kudai kuwa maendeleo ya Tanzania yatatokana na Uwekezaji, Sekta Binafsi na Soko Huria. Hilo si dhambi, lakini ubaya wa Sera zao (Mkapa na Kikwete) ni kukosekana kwa msukumo kutoka Serikali yetu kuhakikisha kuwa Wananchi wa Tanzania wanakuwa washiriki wakubwa na wamiliki wa uchumi na si kukimbilia wageni au bidhaa za kuagiza.


Sasa hapa ndipo kilio changu cha kusema CCM adui wa maendeleo kinapokuja. Badala ya CCM kuhamasisha tija, juhudi na maarifa ili kuboresha uzalishaji mali ndani ya nchi na kupitia Wananchi wake, CCM imeonelea kuwa njia pekee ya Tanzania kufanikiwa ni kuingia katika soko huru na uwekezaji wa kutoka nje.

Namnukuu Kikwete kwenye hotuba yake ya Kampala

Quote:
``A free trade area performs better with a customs union. I appeal to you to reflect the importance of coming together as one after this summit,`` he said.

He explained that good infrastructure served as a bridge to African countries’ development, adding that it was crucial for the regional blocs to decide on ways to make that possible through a fast implementation plan as agreed.

The president also commented on the raging international financial crisis, saying it was now especially difficult for African countries to get outside funding and therefore time for them to devise ways to remain steady and stable without depending too heavily on such assistance.

``We should encourage private sectors, foreign and local, to contribute to the efforts of improving the infrastructure,`` he said.


Anachosahau Kikwete pamoja na nia yake nzuri ni kuwa Tanzania bado haina uwezo wa ndani wa kuzalisha na kujitosheleza, hata zile bidhaa ambazo malighafi zake zinapatikana ndani ya nchi.

Tanzania ya leo ni mnunuzi mkubwa (consumer) na si mzalishaji (producer and supplier) na ndio maana tuna madeni makubwa na kukosekana kwa uwiano wa uuzaji na uagizaji wa bidhaa ambao umekimbilia kuifanya Tanzania ipoteze nguvu ya sarafu yake na hali ya maisha ya Watanzania kuendelea kuwa duni.

Tanzania ya leo haina mpango kabambe wa kuboresha Kilimo, Ufugaji au Uvuvi bila kutegemea Wageni wawekezaji waje kutuokoa. Sasa tutakuwaje na uwezo mzuri kiuchumi ikiwa Kenya, Uganda na Congo bila kusahau Malaysia, Thailand na India ndio watakuwa wakituuzia chakula huku wakulima wetu wakiwa hawana uwezo wa kulima na kujitosheleza au kulisha familia zao?

Ni mfumo gani huu wa Uchumi na kwa utajiri gani Tanzania inakimbilia kuimba kwa sauti kuu kuwa tuwe na Soko huru, huku haina uwezo wa kujitosheleza na inategemea misaada na kuaiza bidhaa?

Watanzania watafaidika nini ikiwa hakuna msukumo wowote wa kubadilisha mfumo wetu wa Uchumi na Uzalishaji kwa kuchochea Tija, Juhudi, Maarifa ili kuunda Taifa linalojitegemea na linalopambana na Umasikini?
 
GDP kisiwe kipimo pekee cha kusema nchi gani ni tajiri zaidi duniani na nchi gani ni masikini wa kutupa.
Watu wa development studies wana kitu wanaita INDICATORS OF DEVELOPMENT,ambayo ina vitu vingi ma hiyo GDP ikiwa ni kasehemu tu ambavyo kwa pamoja ndivyo vinapima uwezo wa kimaendeleo wa nchi tofauti.
Kuna vitu kama huduma za kijamii kwa mfano shule,hospitali,zahanati,maji safi na salama,kuna walimu wangapi katika nchi,uwiano wa madaktari na wagonjwa,vitanda hospitalini nk
Kuna vitu kama miundombinu,barabara,reli,,anga,simu,mzunguko wa pesa,upatikanaji wa ajira,nk nk
Mambo yako mengi.Kwahiyo unaposema GDP pekee ndiyo kipimo cha maendeleo,si kweli.Inabidi uziangalie hizo indicators zote halafu ndiyo utupangie list ya matajiri na masikini.
Halafu hiyo GDP yenyewe inatafutwaje?iko even?Nchi kama Luxembourg ina watu wasiozidi 500,000(laki tano),hiyo population ni kama mara sita ndiyo ifikie population ya watu wa jiji la Dar Es Salaam kwa mfano.Sawasawa na Rwanda na Burundi ambazo nazo zina idadi ndogo ya watu.
Manake kanchi kenye watu wadogo kama Luxembourg,ni sawa na mkoa fulani wa Tanzania au mji fulani wa Marekani au nchi nyingine kubwa.ukikafanyia hiyo GDP ni sawa labda kwa mfano ufanye GDP kwa sehemu nyingine kwa uwiano huohuo.Kwamfano ukifanya GDP ya mkoa wa Dar Es Salaam,utapata nzuri sana zaidi ya hiyo 600.
Kwahiyo point hapa ni hiyo uneven distribution of incomes in different parts of different populations in a big country like Tanzania.
Ndiyo utaona bajeti ya ulinzi ya Marekani ni zaidi ya bajeti ya nchi tano za ulaya lakini kwenye GDP inashika nafasi ya 2/3/5
Kwahiyo usidanganyike na hizo figure mkuu

Usidanganye watu hapa, please FUTA huu huozo!! GDP is a measure of wealth!! Kuna GDP Per Capital, na GDP = Gross Domestic Product. Please go back and learn again!
 
Kama definition ya GDP, ambayo ni

the total market value of all final goods and services produced in a country in a given year

mnaikubali basi sioni kwanini msione yafuatayo:

Sehemu kubwa ya "goods and services" zinazozalishwa na Watanzania hazioorodheshwi na kupata thamani yake kwani haziko katika uchumi rasmi.

Wakata nywele, mama ntilie, makondakta, watumishi wa ndani, wauza nyama mabuchani vijijini, machinga, etc ni sehemu kubwa sana ya wazalisha mali Tanzania, lakini mchango wao hauko kweye hilo li-GDP lenu.
Lo! Hapa ndiyo nachoka kabisa!! my layman answer is GDP (Gross Domestic Production) you divide by population gives you Per Capita; i wud expect 40million population of TZ to produce more than 500,000 of luxemburg; shud be relative!
 
these terms are corelated, without gross production you cannot get per capital; wake up please

Wabongo bwana,kila kitu wao kukariri tu.Sasa nikuulize;40-49%? tunayoongezewa na wahisani kwenye bajeti yetu na misaada mingine tunayopewa nayo inajumlisha kwenye pato la taifa?
 
Wabongo bwana,kila kitu wao kukariri tu.Sasa nikuulize;40-49%? tunayoongezewa na wahisani kwenye bajeti yetu na misaada mingine tunayopewa nayo inajumlisha kwenye pato la taifa?
Ushasema 40 - 49% tunapewa. Pato la Taifa ni ile production (total wealth you produce)
 
Economy - overview: Tanzania is one of the poorest countries in the world. The economy depends heavily on agriculture, which accounts for more than 40% of GDP, provides 85% of exports, and employs 80% of the work force. Topography and climatic conditions, however, limit cultivated crops to only 4% of the land area. Industry traditionally featured the processing of agricultural products and light consumer goods. The World Bank, the IMF, and bilateral donors have provided funds to rehabilitate Tanzania's out-of-date economic infrastructure and to alleviate poverty. Long-term growth through 2005 featured a pickup in industrial production and a substantial increase in output of minerals led by gold. Recent banking reforms have helped increase private-sector growth and investment. Continued donor assistance and solid macroeconomic policies supported real GDP growth of nearly 7% in 2007.
GDP (purchasing power parity): $51.07 billion (2007 est.)
GDP (official exchange rate): $16.18 billion (2007 est.)
GDP - real growth rate: 7.3% (2007 est.)
GDP - per capita (PPP): $1,300 (2007 est.)
GDP - composition by sector: agriculture: 42.5%
industry: 18.9%
services: 38.5% (2007 est.)
Labor force: 20.04 million (2007 est.)
Labor force - by occupation: agriculture: 80%
industry and services: 20% (2002 est.)
Unemployment rate: NA%
Population below poverty line: 36% (2002 est.)
Household income or consumption by percentage share: lowest 10%: 2.9%
highest 10%: 26.9% (2000)
Distribution of family income - Gini index: 34.6 (2000)
Inflation rate (consumer prices): 7% (2007 est.)
Investment (gross fixed): 23.2% of GDP (2007 est.)
Budget: revenues: $3.561 billion
expenditures: $3.594 billion (2007 est.)
Public debt: 19.6% of GDP (2007 est.)
Agriculture - products: coffee, sisal, tea, cotton, pyrethrum (insecticide made from chrysanthemums), cashew nuts, tobacco, cloves, corn, wheat, cassava (tapioca), bananas, fruits, vegetables; cattle, sheep, goats
Industries: agricultural processing (sugar, beer, cigarettes, sisal twine); diamond, gold, and iron mining, salt, soda ash; cement, oil refining, shoes, apparel, wood products, fertilizer
Industrial production growth rate: 9.5% (2007 est.)
Electricity - production: 1.88 billion kWh (2005)
Electricity - production by source: fossil fuel: 18.9%
hydro: 81.1%
nuclear: 0%
other: 0% (2001)
Electricity - consumption: 1.199 billion kWh (2005)
Electricity - exports: 0 kWh (2005 est.)
Electricity - imports: 136 million kWh (2005)
Oil - production: 0 bbl/day (2005 est.)
Oil - consumption: 25,000 bbl/day (2005 est.)
Oil - exports: 0 bbl/day (2004)
Oil - imports: 24,800 bbl/day (2004)
Oil - proved reserves: 0 bbl (1 January 2006 est.)
Natural gas - production: 0 cu m (2005 est.)
Natural gas - consumption: 0 cu m (2005 est.)
Natural gas - exports: 0 cu m (2005 est.)
Natural gas - imports: 0 cu m (2005)
Natural gas - proved reserves: 21.73 billion cu m (1 January 2006 est.)
Current account balance: -$1.856 billion (2007 est.)
Exports: $2.227 billion f.o.b. (2007 est.)
Exports - commodities: gold, coffee, cashew nuts, manufactures, cotton
Exports - partners: China 9.9%, India 9.3%, Netherlands 6.2%, Germany 6.1%, UAE 4.7% (2007)
Imports: $4.861 billion f.o.b. (2007 est.)
Imports - commodities: consumer goods, machinery and transportation equipment, industrial raw materials, crude oil
Imports - partners: China 11.9%, Kenya 7.9%, South Africa 7.6%, India 6.8%, UAE 5.8% (2007)
Economic aid - recipient: $1.505 billion (2005)
Reserves of foreign exchange and gold: $2.91 billion (31 December 2007 est.)
Debt - external: $4.382 billion (31 December 2007 est.)
Stock of direct foreign investment - at home: $NA
Stock of direct foreign investment - abroad: $NA
Market value of publicly traded shares: $587.9 million (2005)
Currency (code): Tanzanian shilling (TZS)
Currency code: TZS
Exchange rates: Tanzanian shillings per US dollar - 1,255 (2007), 1,251.9 (2006), 1,128.93 (2005), 1,089.33 (2004), 1,038.42 (2003)
Fiscal year: 1 July - 30 June
 
Ushasema 40 - 49% tunapewa. Pato la Taifa ni ile production (total wealth you produce)


Unajua kwamba misaada inasaidia sana kuboresha huduma za kijamii kama itatumika ipasavyo na hivyo kuifanya nchi moja kuwa na huduma nzuri za kijamii kuliko nchi nyingine hata kama GDP yake ni ndogo?
 
Masanja,

Asante kwa hoja zako zenye kumfanya mtu afikirie.

Tofautisha kati ya "kuzalisha" ‘goods and services" zenye thamani ya $600 na "kuzipata" $600. Ni Watanzania wepi ambao hawazalishi "goods and services" zenye thamani ya angalau $600 kwa mwaka?

Mfanyakazi wa ndani, gardener, mkulima wa kijijini, muuza kangara, kondakta wa basi la kijijini, muuza duka, etc, wote wanazalisha "goods and services" zenye thamani ya zaidi ya $2000 kwa mwaka! Hawazipati hizo fedha, but that is a different question.

Does the actual value of a good or a service that is produced depend on location? "Thamani" ya service ya kuuza dukani kwa saa moja Marekani inatofautiana na thamani ya kazi hiyo iyo ikifanyika Tanzania? Kwa maoni yangu, ukifanya kazi yenye thamani ya $10 basi umezalisha $10, hata kama unalipwa $1. Unakuwa umenyonywa lakini utajiri wa $10 unakuwa umezalishwa nchini.

Umesema sawa kwamba informal sector ziko sehemu nyingi. Hao wanaohesabu wanokosea, kwa viwango tofauti, katika sehemu zote hizo. Kwetu wanakosea mno! Na kwa upande mmoja, we are supra-informal! Hata mji mkuu wa Dar watu wanaishi na kufanya kazi bila address zozote!

Nahitimisha kwa kusema ukiangalia vizuri, utakuta karibu kila Mtanzania mtu mzima anazalisha "goods and services' zenye thamani kubwa kuliko hiyo average waliyotoa. Unyonyaji ndio unafanya wengi wasiuone ho utajiri wanaozalisha.
 
Just to put this in perspective

GDP yetu ya 2006 (PPP) ilikuwa some $ 29 billion, deni la Lehman brothers ilipofile chapter 11 lilikuwa $ 613 billion na ilikuwa na assets za $ 639 billion.

Deni la Lehman brothers lilikuwa zaidi ya mara 21 ya GDP (PPP) yetu ya 2006!

Assets za Lehman Brothers zilikuwa zaidi ya mara 30 ya GDP (PPP) yetu ya 2006

Kwa hiyo ?

Kwa hiyo nini Pundit ?

Nina assume unataka kulinganisha pato letu na pato la Lehman Brothers, kama ambavyo wengine wameweka stats zako in perspective ya utajiri wa Wamarekani binafsi kulinganisha na Taifa zima la Tanzania. Kama ndio hivyo, basi unaweza kuwa unapotosha.

Kama GDP ni total market value ya goods and service za Taifa basi huwezi kulinganisha utajiri wa kampuni au mtu fulani na na GDP ya Taifa lingine kwa sababu ya tofauti ya market forces za market places tofauti. Hiyo GDP yetu ya $29 billion (assuming, without concluding, kwamba Augustine Moshi is wrong na kwamba hizo GDP figures ni accurate measure ya uzalishaji wetu wote) hiyo $29 bil ni market value ya yote tuliyozalisha kwa market place ya Tanzania. Haimaanishi, sidhani, kwamba Lehman Bothers au Warren Buffet na Jay Z na Oprah walizalisha goods and service nyingi zaidi na walifanya kazi nyingi kuzidi Watanzania wote. Inawezekana kwamba market value ya album mbili za Jay Z zinazidi thamani ya mazao ya biashara ya wakulima wote Tanzania, lakini hiyo ni kwa sababu ya demand ya muziki Marekani in dollar amounts ni kubwa kuliko magunia yote ya mahindi na kahawa ma mazao yote ya biashara yaliyozalishwa Tanzania. But then again, tunapoanza kulinganisha thamani ya vitu katika nchi mbili tofauti in pure dollar amounts tunasahau tofauti ya purchasing power na market forces zingine.

Kikombe kikubwa cha kahawa cha Starbucks Marekani kinaweza kufika dola nne. Tanzania kikombe cha kahawa hakifiki dola nne. Sasa, kwa kulinganisha market value ya bidhaa na huduma utasema mkulima wa kahawa Tanzania au muuza mgahawa kapitwa na mfanyakazi wa Starbucks alieizalishia Marekani dola nne kwa kikombe kulinganisha na Muuza Chai Chapati aliyeizalishia Tanzania shillingi mia kwa kikombe ? Haiwezekani.

Na pia, utajiri wa Lehman Bothers na makampuni mengine ya fedha Marekani ni ya utajiri wa financial instruments za kwenye makaratasi tu. Ikiwemo ku overvalue thamani ya vitu, kama vile mortgages zisizolipika. Lehman Brothers hawakuzalisha tangible goods and services! Na kina Oprah waliokaa kwenye viti ku host talk shows ambazo zina market value ya mabilioni ya hela sidhani kama tunaweza kusema wanatuzidi kwa uzalishaji. Ni kwamba tu Wamarekani wanapenda talk shows na rap music zinazoingiza mabillioni katika market place ya Marekani kuliko bei ya goods and services zetu Tanzania - kwa market place ya Tanzania. Tutofautishe.

Jay Z akiuza mamilioni ya dola za rekodi za rap katika market place ya Marekani haimaanishi amemzidi Bichuka kiuzalishaji, ambae labda hana hata dola nusu milioni, kwa sababu Watanzania hatulipii huduma za muziki kwa mamillioni ya dola -katika market place ya Tanzania. Tutofautishe.
 
Back
Top Bottom