TANZIA: Aliyewahi kuwa Rais wa pili wa Zanzibar, Mzee Aboud Jumbe afariki dunia

Mzee Aboud Jumbe amefariki dunia muda si mrefu. Ni baada ya kuugua muda mrefu.

=======
UPDATE:

JamiiForums imethibitisha kutokea kwa msiba huu.

View attachment 381455
View attachment 381456
View attachment 381457
Inalilah wainailaihi rajiuun. Pole maalim Seif, hukupta nafasi ya kumuomba radhi kwa maovu uliomtendea. Hajakusamehe na huna radhi nae amoja na watu wa Zanzibar. Tulikuomba ukamuombe msamaha sasa ndio kaburi ya maisha ya siasa zako. HUKUBALIKI TENA ZANZIBAR
 
Tutasikia, alikuwa mtu wa watu, mchapa kazi, mwadilifu mchango ni mkubwa na ameacha pengo kubwa ambalo sio rahisi kuzibika

RIP Mzee Abdul Jumbe Mwinyi.
 
Huyu mzee Jumbe ni muislam, naamini taratibu za mazishi zitazingatia imani yake i.e azikwe leo leo.

Serikali isijipendekeze.

RIP Aboud Jumbe.
Nenda ukale ugali na malaika
Mchonga akikuzingua mpe za mbavu.
 
Upumzike kwa Amani..!! Alikuwa silent sana, sikujua kama alikuwa hai au alikuwa Rais wa Znz... sbb alipotea sana ktk vyombo vya habari au
mambo ya kitaifa... sijawahi muona..!!

Ukifika huko Jumbe.. waambie Mwalimu Nyerere na Mzee Karume, watuombee, tunapambana huku duniani, tuko tunakuja huko...!!

Mungu mpokee na mtakase mzee wetu Jumbe.. Amina..!!

 
RIP mzee wetu , umri uliofikisha yapata kupewa tuzo hapa duniani.....yaani ulizaliwa 1920? Mungu akuangazie mwanga wa milele.
 
Ningekuwa mwana familia nisingemruhusu hata kiongozi mmoja wa nchi hii asogee....ubaya ubaya TU bora
mkuu,umesahau ya kabwe na makonda?ukileta fyokofyoko watakufyokoa!hata mie ningependa waheshimu wosia wa marehemu,ila hofu yangu ni je:wosia wa marehemu utaheshimiwa?
 
Kwa mujibu wa wosia wake amekataa kuzikwa Kitaifa au Kiserikali. Anataka familia yake ndio imzike...
 

Aliyemfunga Jumbe kule mjimwema alikuja kumalizwa na 'mwanawe' aliyemtegemea kwa kumsimamia 'apite'. alimfyeka kama majani pamoja na kuwa mgumu kama 'ndago'
 
mkuu,ni nini kilicho tokea ktk kikao icho cha n.e.c?
 
Alipo apa kuwa Rais/Makamu wa Rais alipoteza haki hizo zote. Haki hizo kwa sasa ni za Taifa, na taifa litaamua kama alivyojikabidhi kwa taifa kipindi anaapishwa.Full stop.

duuuuuuuuu, mbona hasira mkuu? hata kwenye msiba unapandisha mori? kiapo chake kilikoma alipoonekana anataka kuleta uasi, akafungwa, uhuru wake ni umauti huu uliomfika, hapo sasa anahaki yakuchagua nini kifanyike baada ya kifungo kuisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…