TANZIA: Mkuu wa Uhamiaji mkoa wa Kagera, Pendo Butenghe afariki dunia

TANZIA: Mkuu wa Uhamiaji mkoa wa Kagera, Pendo Butenghe afariki dunia

TANZIA: MKUU WA IDARA YA UHAMIAJI MKOANI KAGERA AFARIKI DUNIA -

Mkuu wa Uhamiaji mkoani Kagera Pendo Butenghe, amefariki usiku wa kuamkia leo, Aprili 29 katika Kliniki ya COSAD kutokana na maradhi ya Shinikizo la Damu na Kisukari - Aidha, inadaiwa marehemu alianza kutumia dawa za kienyeji (kujifukuza) na alipoanza kukosa pumzi na kushindwa kuhema mkewe alimpeleka katika Kliniki hiyo. Aliwekewa drip lakini kupumua ikawa shida zaidi hadi akakutwa na mauti - Kaimu Mkuu wa Uhamiaji Kagera, Thomas Fush, amesema wanasubiria mwongozo wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa na Makao Makuu ya Uhamiaji kujua taratibu za msiba na maziko.

Source : msela tv
 
Kwa spidi hii ya watu maarufu/vyeo wanavyofariki nadhani wananchi wa kawaida tutakua tumepukutika sana, ni vile taarifa zetu haziandikwi kama hawa maarufu
 
Very sad msomi mzima kutumia miti shamba

Na ndio Rais ajue kwamba kauli ya mkuu wa nchi ina nguvu sana.

Yaani mtu unaumwa presha halafu ujiweke kwenye blanket na joto la 100 C halafu usalimike?
 
Mmmh kuugua kwa muda mrefu hii imekaaje?

Bado hatujachelewa kuchukua hatua lakini hali itakuwa mbaya zaidi tukiebdelea kuzubaa.

Tutapoteza watu wengi bila sababu za msingi.
 
Ooooho mambo yanazidi kuaribika wacha liende we are on the right track
 
Imeripotiwa muda mfupi uliopita kuwa Pendo Butenghe ambaye ni Mkuu wa Uhamiaji mkoa wa Kagera amefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Akithibitisha kifo hicho, Kaimu Mkuu wa Uhamiaji Kagera, Thomas Fush, amesema marehemu alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya kushuka sukari mwilini.

Taarifa rasmi za kilichomuua hazijatolewa.

===

Mkuu wa Uhamiaji mkoani Kagera Pendo Butenghe, amefariki usiku wa kuamkia leo, Aprili 29 katika Kliniki ya COSAD kutokana na maradhi ya Shinikizo la Damu na Kisukari

Aidha, inadaiwa marehemu alianza kutumia dawa za kienyeji (kujifukuza) na alipoanza kukosa pumzi na kushindwa kuhema mkewe alimpeleka katika Kliniki hiyo. Aliwekewa drip lakini kupumua ikawa shida zaidi hadi akakutwa na mauti

Kaimu Mkuu wa Uhamiaji Kagera, Thomas Fush, amesema wanasubiria mwongozo wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa na Makao Makuu ya Uhamiaji kujua taratibu za msiba na maziko

Lawama zote kwa Dk .John aka Yohana mbatizaji anayebatiza kwa moto toka Chato

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom