Friends and our enemies,
Naanza na maaskofu,nyinyi maaskofu baadhi yenu mna kiburi sana..
Mnataka serikali iwapigie magoti kwani inawajibika kwenu au kwa wananchi?
Tambueni kazi yenu ya kuwa viongozi wa dini ni kazi ya wito na kumtumikia mungu,ikiwemo na kuongoza waumini wenu.
Ni kazi yenu sawa kukemea mabaya na kuhimiza mema na mazuri,lakini mnajisahau na kudhani kuwa nyinyi ndie wenye mamlaka na dola ya kuongoza nchi hii.
Maaskofu mnasahau kuwa mnachukua fedha nyingi sana za kodi zetu kwa kupitia MOU kati yenu na serikali kwa minajili ya huduma za afya,hapo hapo huduma hizo bado hazieleweki na sisi walalahoi tukija huko hospitalin bado tunalipishwa.
Leo mnakuja na matamko ambayo hayana kichwa wala miguu na kusema kwamba eti hamtaruhusu viongozi wa serikali kutoa neno kwenye nyumba zenu za ibada,aliewaambia kuwa serikali ina haja sana ya kutoa neno kwenye mimbari zenu ni nani?
Serikali haina dini,viongozi wa serikali ni waumini wenu,ni hiyari yenu kuwaalika au kutowaalika,sisi haitupunguzii wala kutuongezea chochote,kwahiyo mikwala yenu haina maana.
Wengine mfano kama Gwajima na wenzake kama Kitima,wameacha moja kwa moja kazi yao ya kuchunga kondoo wao wamegeuka kuwa allies wa vyama vya upinzani kwenye kueneza ajenda zao,serikali wakisimama kwenye haki na utaratibu wanageuka na kutoa vilio vya udini,eti ya kwamba wanataka uhuru wa kufanya ibada.
Sasa,kama uhuru wa ibada mnapewa kisha mnageuza platforms za makanisa kuwa sehemu ya kuhubiri minyukano ya kisiasa dhidi ya serikali why msichukuliwe hatua ikiwemo na kuyafuta hayo makanisa?
Sasa,tusionane wabaya...nchi hii ina taasisi nyingi za dini,nyinyi TEC na wakolole hamna uspecial wowote wa kutaka kuipa amri au masharti serikali.
NCHI HII HAINA DINI,KAMA MNATAKA UHURU WA KUIPANGIA SERIKALI NENDENI VATICAN.