Taratibu za kufuata ili kumiliki Silaha ya Moto Tanzania

Kaburu gani unayemtafuta umuue? Im sorry muuaji!
 
Du..kaz kwelkwel mpk kupata iyo ki2
 
wadau
Naomba kwa mwenye ufahamu juu ya vigezo vinavyo tumika ili mtu wa kawaida aweze kumiliki silaha[bunduki] kwa raia wa Tanzania


Unaanza kutafuta bunduki yenyewe, unapewa invoice na kampuni inayokuuzia, unaomba kibali cha kununua hiyo bunduki polisi. Baada ya hapo, (kwa kufuata utaratibu halali wa kisheria ) polisi wataitisha mikutano ya kamati za ulinzi na usalama (kuanzia mtaa/kijiji/kata hadi wilaya) ili kujadili ombi lako na wajithibitishie kuwa una akili timamu na sababu isiyotiliwa mashaka ya wewe kumiliki bunduki. Ukipita hapo unapewa kibali cha kumiliki hiyo silaha lakini baada ya kupitia mafunzo ya namna ya kuitumia na hifadhi yake.

Angalizo: Kwa kuwa siku hizi kuna policcm kuna uwezekano ukaipata bila kufuata utaratibu nilioueleza (na ndio maana kuna watu wanaporwa SMG - ambo kisheria hairuhusiwi mtu binafsi kuimiliki - na machangudoa hotelini).
 

asante kwa maelezo mazuri,mimi nadhani utaratibu ulioueleza ndio mzuri na je wapi natakiwa kupata mafunzo ya jinsi ya kuitumia?
 
Mkuu umemaliza, hoja yangu ya awali ilikuwa ni ya kuchamgamsha bunge tu. Si unajua current issues zinazogonga vichwa vya magazeti.
 
Lazma uwe umepitia jeshi

Acha uongo. Sio Lazima.
Taratibu ziko hivi, Unaenda kwanza kwenye Maduka ya Silaha, Mzinga au Tanganyika Riffle, (haya yapo kikanda i guess, Mzinga wanalo Dar, Moro, Moshi na Arusha, Tanganyika Riffle iko pale Clock Tower Arusha na pia Dar wana Duka i guess) unanunua silaha yako unayoitaka, either Pistol, Bunduki za uwindaji au Bunduki za kulindia mashamba (with Lower Caliber i mean) then ukishanunua, unaenda kwenye serikali ya mtaa unaoishi, kamti ya ulinzi ya mtaa wako itakuandikia barua ambayo utaenda nayo kwa OCD wa kituo cha polisi cha wilaya yako, ukiambatanisha na barua yako ya maombi ya kumiliki silaha tajwa na sababu za kutaka kumiliki ukiziweka wazi.

Pale utapewa Form 4, utazijaza utaambatanisha na Picha 4 (passport size) then na ile barua ya kamati ya ulinzi ya mtaa na kopi ya risiti ya kununulia silaha yako.
ukimaliza utawasilisha kwa OCD na wao watayapitia maombi yako kwenye kikao cha kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya, kisha yakiita yatapelekwa kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa then yakipita yataletwa DSM kwa msajili wa silaha, ambaye atakupatia leseni/kibali cha kumiliki silaha yako.

ukishapata kibali unaenda na original receipt yako kwenye lile duka ulilonunulia silaha yako nao wanakupatia unarudi zako home.hope umenielewa japo nimeelezea kwa kifupi, kama una swali unakaribishwa pia.
 

Kuna uwezekano wa maombi yako kukataliwa? ikitokea maombi yamekataliwa huwa inakula kwako au unarudishiwa fedha zako zote!! Baada ya kukataliwa unaweza kufanya maombi tena baadaye?
 
Kuna uwezekano wa maombi yako kukataliwa? ikitokea maombi yamekataliwa huwa inakula kwako au unarudishiwa fedha zako zote!! Baada ya kukataliwa unaweza kufanya maombi tena baadaye?

hawawezi kukurudishia fedha zako,(maana silaha umenunulia dukani na sio polisi) kama yamekataliwa unaweza ku-apply tena na kwenye ile fomu utakayopewa polisi ina sehemu unatakiwa kujazwa kama ushaomba silaha na kukataliwa ama la. kwa hivo ukikataliwa utakuwa umepewa sababu na may b utaitwa kwenye kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya wakuhoji.
 

shukrani,nadhani wengi wamepata kilichobola na sasa ni kuanzisha harakati ya kuipata hii kitu
JOTO HASIRA
 
Wewe ukija tutakumilikisha kisu manake nna wasiwasi utaanza kuua paka na mbwa
 
asante kwa maelezo mazuri,mimi nadhani utaratibu ulioueleza ndio mzuri na je wapi natakiwa kupata mafunzo ya jinsi ya kuitumia?

Ukipewa kibali cha kuinunua utapewa na mafunzo na polisi kabla hujakabidhiwa bunduki yenyewe.
 
kwa tanzania mtu anatimiza miaka 50 hajui ata matumizi ya silaa wenzetu wanazaliwa nazo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…