Acha uongo. Sio Lazima.
Taratibu ziko hivi, Unaenda kwanza kwenye Maduka ya Silaha, Mzinga au Tanganyika Riffle, (haya yapo kikanda i guess, Mzinga wanalo Dar, Moro, Moshi na Arusha, Tanganyika Riffle iko pale Clock Tower Arusha na pia Dar wana Duka i guess) unanunua silaha yako unayoitaka, either Pistol, Bunduki za uwindaji au Bunduki za kulindia mashamba (with Lower Caliber i mean) then ukishanunua, unaenda kwenye serikali ya mtaa unaoishi, kamti ya ulinzi ya mtaa wako itakuandikia barua ambayo utaenda nayo kwa OCD wa kituo cha polisi cha wilaya yako, ukiambatanisha na barua yako ya maombi ya kumiliki silaha tajwa na sababu za kutaka kumiliki ukiziweka wazi. Pale utapewa Form 4, utazijaza utaambatanisha na Picha 4 (passport size) then na ile barua ya kamati ya ulinzi ya mtaa na kopi ya risiti ya kununulia silaha yako.
ukimaliza utawasilisha kwa OCD na wao watayapitia maombi yako kwenye kikao cha kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya, kisha yakiita yatapelekwa kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa then yakipita yataletwa DSM kwa msajili wa silaha, ambaye atakupatia leseni/kibali cha kumiliki silaha yako.
ukishapata kibali unaenda na original receipt yako kwenye lile duka ulilonunulia silaha yako nao wanakupatia unarudi zako home.hope umenielewa japo nimeelezea kwa kifupi, kama una swali unakaribishwa pia.