Taratibu za kufuata ili kumiliki Silaha ya Moto Tanzania

Taratibu za kufuata ili kumiliki Silaha ya Moto Tanzania

Ukiona urasimu bongo mkubwa kama ilivyo jadi,sema nikupe bastola ya kijadi.Haina usajili,leseni haina wala hakuna atakayejua kama unayo.Bastola hiyo ni kwa ajili ya kuzuia wezi tu si kuua wala kwenda kuibia.

Ni kimti fulani unaweka home kwako basi,wezi wakija nyumba hawaioni basi,kama una mshiko mkubwa,basi unanusa kijiti chako,vibaka/wezi hawakuoni.Hizo za kisasa balaa.

ha ha ha
 
We unajua ofisi ya RPC ina watu wangapi ambao wanaweza ku sign off kibali cha kitu kwa niaba ya RPC??? Wanatosheleza kuprocess maombi yote nchi nzima au ndo kuunda urasimu tu ili kutengeneza mazingira ya rushwa? RPC and his signers hawana ulazima wa kuwa kwenye huu mchakato, kufuatilia ombi la kuwa na silaha nchi za watu hii ni kazi ya mid level detective mmoja tu per application.

Eti maombi yapitie kwa mwenyekiti wa kijiji sijui wa kata, mimi natokea Manzese Darajani, Mwenyekiti wa mtaa hapa hajui background ya binadamu yeyote hapa maeneo jinsi palivyo na nyomi la kila aina, Mwenyekiti wa Mtaa au Kamanda Kova apitie maombi ya silaha atasaidia nini? Kazi ya detectives hii.

1. Nimekushauri fuatilia utajua zaid, kwanza huyo RPC hata hutomuona kwa hili wapo watu assigned for this duty!!! Wanatosheleza sana tu, kama mwalimu can handle a class of 50 students at a Uni level hawa watashindwa nini????!!!! Nilikuuliza RPC ni ofisi au mtu??!! Jukumu la RPC kwenye kamati ya ulinzi na usalama mkoani unaijua????!!! Can you connect the process na hiyo role huko???!!!

2. Umeongelea detectives; halafu unahoji umuhimu wa wakuu wa mitaa na kata na kwa taarifa yako wanaita wajumbe na lazima kuwe na muhtasari na sahihi za wajumbe waliohudhuria???!! Umewahi kuiona fomu ya maombi??!! Unajua inataka mpaka Box # na mtaa na nyumba namba???!!! Unajua ukihama unatakiwa kutoa taarifa ya anuani mpya????!!! Bila ya hizi tarifa huyo detective ataota au ni malaika????!!!!

Nakushauri badala ya kubisha kwa nadharia tafuta muda nenda kituo cha polisi mkoa nenda ofisi husika omba maelezo na fomu utajua zaidi halafu urudi hapa mkuu!!!!!
 
Nakushauri ununue silaha kali kuliko yote ni Biblia.Hapo hakuna wakukudhuru
 
Jamani kwa mnaojua hii kitu hebu nipeni ufahamu, hivi sheria ya kumiliki silaha ya moto inaruhusu pia hata kwa wanawake kumiliki?

maana jana kuna mwanamke mmoja nimemuona na bastola wakat sio askari polisi, polisi jamii, askar magereza wala JWTZ na hata kwenye ulinzi shirikishi hayumo
 
Ni mwanamke wa nchi gani huyo ? Kwa Tanzania ni ruksa kwa mtu mzima yeyote mwenye akili timamu na tabia njema katika jamii, tena sasa hivi katiba pendekezwa imeongeza wigo kwa maana kwamba katika eneo husika kama wanaume 5 mnamiliki hiyo kitu ni lazima na wanawake 5 nao wamiliki.
 
Refer yule mama wa bagamoyo aliyeua jambazi kwa kutumia bunduki anayoimiliki kisheria

Jamani kwa mnaojua hii kitu hebu nipeni ufahamu, hivi sheria ya kumiliki silaha ya moto inaruhusu pia hata kwa wanawake kumiliki?

maana jana kuna mwanamke mmoja nimemuona na bastola wakat sio askari polisi, polisi jamii, askar magereza wala jwtz na hata kwny ulinzi shirikishi hayumo
 
Ni mwanamke wa nchi gani huyo ? Kwa Tanzania ni ruksa kwa mtu mzima yeyote mwenye akili timamu na tabia njema katika jamii, tena sasa hivi katiba pendekezwa imeongeza wigo kwa maana kwamba katika eneo husika kama wanaume 5 mnamiliki hiyo kitu ni lazima na wanawake 5 nao wamiliki.

Ni Mtz huyo na kwa kweli nilikuwa cjui kama sheria inaruhusu nikajua tunakaribia kupigishwa magoti
 
Ni Mtz huyo na kwa kweli nilikuwa cjui kama sheria inaruhusu nikajua tunakaribia kupigishwa magoti

Inaruhusu Mkuu na wengi wanazo ila kwa kuwa wanawake huwa hawapendi kujionyesha kama wanaume na hawavai mikanda ya kuzipachika kama Mhe. Rage, ndio maana huzini kwa wingi, kumbuka yule wa Bagamoyo aliyemtwanga jambazi nje ya nyumba wakatik walipovamiwa. Aidha ifahamike kuwa wanawake wanaopewa ni wale wenye staha na heshima katika jamii sio vicheche kama ilivyo kwa wanaume.
 
Mkuu wewe upo Tanzania kweli? Au unaishi moja ya nchi zifuatazo Afghanstan, Somalia, Saudi Arabia, nk
 
"Hamsini kwa hamsini", sijui upande wa sheria lakini kwa nini asiwe na haki ya kuimiliki?
 
Kiudhati haswa hawa binadamu hawakustahili !
Piga picha mkeo anamiliki cha-moto then una mpango wa kuoa mke wa pili , siku chache kabla hujaoa unaona mara kaitoa anaifanyia usafi ! Utaoa ?
 
Back
Top Bottom