Taratibu za kufuata ili kumiliki Silaha ya Moto Tanzania

mkuu GAZETI,

naomba kufahamu kuhusu hizi silaha ambazo zinatumiwa na kampuni za ulinzi, hizi zenyewe bei zake zikoje?

Masharti na vigezo vya kupata hizo silaha ni zipi?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu hebu itolee maelezo kidogo!
Niliuliza hili swali nikajibiwa kama ifuatavyo na IDIMI

Ni pilipili iliyo katika hali ya kimiminika ambayo imefungashwa kwenye kopo kama la dawa ya mbu. Mtu akikuletea za kuleta unampulizia usoni kama unavyopuliza dawa ya mbu.
 
ahaaa!!! kama nimeikumbuka vile!
iko kwenye kikopo cheusi hivi kidogo dogo, kinawasha sana aisee!
sikujua kama hilo ndio jina lake!

Wazazi wanakosea sana matunzo ya vitu hatari kama hivi, kuna siku kaka mkubwa alikaacha chumbani hapo akaenda kunawa uso nje, mtoto mdogo hivi akaingia ndani akaanza kukashangaa kale kachupa!

masikini mtoto, akakashika akajipulizia akidhani perfume!

Duh! baada ya hapo.. kilio chake sikupata ona! kwanza mwathirika hakuwa yeye tu, mpaka waliokuwa karibu na chumba waliathrika!

Nadhani ndo hiyo mkuu!
 
Last edited by a moderator:
Angalizo: SNIPER sio silaha ni mtu mwenye shabaha hata akiwa umbali mkubwa, kimsingi swali lako nadhani lime-base kwenye silaha za moto sio baridi kama viwembe na baadhi ya alizotaja mchangiaji wa kwanza,

mi nakushauri nenda maduka ya silaha kama Tanganyika arms, silaha zote za moto utazozukuta pale maana yake raia anaruhusiwa kumiliki!!
Na utaziona bei zake!!

Pia wanaweza kukupa utaratibu wa kufuata ili uweze kumiliki silha ambapo lazima upitie ngazi mbalimbali za uongozi wakuudhinishe
mkuu na biashara ya ulinzi, wenyewe wanaruhusiwaje kumiliki silaha?
bei za bunduki zile (sijui hata zinaitwaje! loh!) zikoje?
 
Mmmmhhh watu wamekupotosha mno aisee:

Nenda pale Wizara ya Mambo ya ndani kuna kitengo kinaitwa AMARD ulizia mtu anaitwa National Focal Point on Small Arms, ni kitengo kinachoshughulikia maswala yote ya silaha ndogondogo. Eg Small Arms Marking, Small Arms Destruction, Arms Licence etc kwa maelezo zaidi gonga hapa About Us - The Regional Centre on Small Arms in the Great Lakes Region, the Horn of Africa and Bordering States (RECSA) GAZETI kwa maelezo zaidi ni PM
aisee!.. mkuu vipi kuhusu na kampuni za ulinzi?
wenyewe umiliki wake wa silaha ukoje na bei zikoje?
 
Niliuliza hili swali nikajibiwa kama ifuatavyo na IDIMI

Ni pilipili iliyo katika hali ya kimiminika ambayo imefungashwa kwenye kopo kama la dawa ya mbu. Mtu akikuletea za kuleta unampulizia usoni kama unavyopuliza dawa ya mbu.

Hio kitu noma sana. Kuna kipindi Dully Sykes alipuliza na kuchafua hali ya hewa ukumbini pale hotel Travertine Magomeni na kusababisha taharuki kubwa. Alilala lupango.
 
aisee!.. mkuu vipi kuhusu na kampuni za ulinzi?
wenyewe umiliki wake wa silaha ukoje na bei zikoje?

Kila kitu na maelezo yote vinapatikana hapo ndo maana wameweka kitengo maalumu cha silaha ndogondogo na center yao iko Nairobi kwa nchi 15 na nimekupa website wacha uvivu wa kusoma
 
Mkuu nimepitia hiyo web ila sijaona relevant information kwa Tanzania kuhusiana na silaha za ulinzi,
nisaidie basi kwa ufafanuzi mkuu!

Availability and price..
 
Hio kitu noma sana. Kuna kipindi Dully Sykes alipuliza na kuchafua hali ya hewa ukumbini pale hotel Travertine Magomeni na kusababisha taharuki kubwa. Alilala lupango.
Haha ha ha ha ha sio kamba hizi mkuu?
 
Mmmmhhh watu wamekupotosha mno aisee:

Nenda pale Wizara ya Mambo ya ndani kuna kitengo kinaitwa AMARD ulizia mtu anaitwa National Focal Point on Small Arms, ni kitengo kinachoshughulikia maswala yote ya silaha ndogondogo. Eg Small Arms Marking, Small Arms Destruction, Arms Licence etc kwa maelezo zaidi gonga hapa About Us - The Regional Centre on Small Arms in the Great Lakes Region, the Horn of Africa and Bordering States (RECSA) GAZETI kwa maelezo zaidi ni PM
Nashukuru DENA huu ni msaada tosha kabisa.
 
ahaaa!!! kama nimeikumbuka vile!
iko kwenye kikopo cheusi hivi kidogo dogo, kinawasha sana aisee!
sikujua kama hilo ndio jina lake!

Wazazi wanakosea sana matunzo ya vitu hatari kama hivi, kuna siku kaka mkubwa alikaacha chumbani hapo akaenda kunawa uso nje, mtoto mdogo hivi akaingia ndani akaanza kukashangaa kale kachupa!

masikini mtoto, akakashika akajipulizia akidhani perfume!

Duh! baada ya hapo.. kilio chake sikupata ona! kwanza mwathirika hakuwa yeye tu, mpaka waliokuwa karibu na chumba waliathrika!

Nadhani ndo hiyo mkuu!

Ha ha ha haaa watu mnaweka vitu hatari kama hivyo bila uangalifu
 
Haha ha ha ha ha sio kamba hizi mkuu?

Ndugu GAZETI, mie ni mtu mzima mwenye staha zangu kabisa. Hii habari ni ya kweli kabisa na iliandikwa na magazeti yenye heshima zake. Inasemekana chanzo cha Dully kupuliza hiyo pepper spray ni kugombea demu na jamaa. Sasa alipozidiwa ndipo alipopuliza hiyo hiyo kitu na kuharibu hali ya hewa pale ukumbini Travertine (kulikuwa na show ya Zanzibar Modern Taarab)
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom