Tanzania tuna matatizo mawili makubwa: (a) tunapenda sana kuiga mambo ya nchi za nje hasa marekani, (b) tunawaogopa sana viongozi wetu kiasi kuwa wakitoa tamko hata kama ni wazo lao binafsi tunalichukulia kama ni sheria.
Swala la umiliki wa silaha za moto (bunduki) ni jambo ambalo siamini kuwa liliwahi kujadiliwa kwa kina na bunge letu bali lilitolewa kama agizo kutoka kwa Waziri mkuu (Sumaye) wakati ule. Matokeo ya umiliki hovyo wa bunduki, na hasa bastola, umesababisha mambo mengi ya ukiukwaji wa amani kwa raia wa kawaida, hasa yakiwahusisha watu wa ngazi za juu katika jamii: viongozi na wafanya biashara.
Marehemu Mzuzuri anakumbukuwa sana kwa hili, ila kuna watu wengi sana kama watoto wa wanasiasa wakongwe Kingunge na Mungai, na viongozi wengine mbalimbali pamoja na wafanya biashara wa viwango tofauti kama vile Mbilinyi Hartmann na steven Kanumba.
Umiliki wa silaha za moto kwa nchi kama Marekani ni swala tete sana ambapo makampuni ya utengenezaji wa bunduki yanatumia nguvu kujihakikishia soko la bidhaa zao hizo. Hata hivyo, Marekani bado wamegawanyika kuhusu umiliki wa silaha hizo ingawa vile vile wana sheria ngumu sana kuhusu utumiaji wa silaha za moto. Kuna mlolongo wa background check kabla mtu hajaruhusiwa kununua bastola, na state nyingine , kwa mfano Florida, wana sheria inaitwa 10-20-life kama
inavyoelezwa hapa. Chini ya sheria hiyo, kutoa vitisho kwa kutumia silaha ya moto kunampeleka mtu jela miaka kumi na zaidi. Halafu kama ataua basi ajue naye atanyongwa bila cha swaleh mtume. Florida ni state ya pili kwa unnyongaji huko Marekani. Pamoja na kuwepo kwa hatua hizo, Marekani wamekuwa wansumbuliwa sana na mauaji ya hovyo ya utumiaji wa bunduki zinazonunuliwa mitaani, kwa mfano yale mauajia ya Virginia Tech na yale yaliyofanywa na
Major Nidal Malik Hasan huko Texas hivi majuzi.
Kinachonifanya nianzishe thread hii, ni ukuaji wa vitisho na matumizi ya silaha za moto nchini kwetu kwa ubishi mdogo tu kama eti kugombea "demu."
Jana niliongea na ndugu yangu mmoja kule Tabora akaniambia kuwa mtoto wa Profesa Kapuya aliua kijana mwenzie kwa kumpiga risasi kwa bastola eti wakigombea DEMU: sijapata data zaidi kuhusu tukio hilo, ila hiyo ni trendi inayoonekana kuwa ya kawaida kwani wiki chache zilizopita kulikuwa na uvumi wa mwana sinema Hartmann kuwatishia mahasimu wake kwa bastola kwa vile eti walimnyang'anya DEMU.
Swali langu ni kuwa je Tanzania tulinogewa wapi na uzuri wa bunduki hadi kuwa na sheria za kuwaruhusu watu kumiliki bundukuki kiholela? Kwa utaratibu wa sasa tuna mwanya mdogo sana wa kujua tofauti kati ya jambazi na raia mwema tukiwaona wakiwa na bunduki.
Tulizoea bunduki kubwa (shortgun+ rifle) kama silaha za kuwindia tu. Bastola ni silaha ya kuua mtu, siyo silaha ya kuacha kila mtu ajibebee mfukoni na kwenda nayo kwanye vilabu.
Naomba Bunge letu liangalie tena sheria yoyote inayohusu umiliki holela wa silaha za moto kama bastola. Ningefurahi kama wataweka sheria ya kusimamia matumizi ya silaha hizo kama ile ya 10-20-life inayotumika Florida