Taratibu za kufuata ili kumiliki Silaha ya Moto Tanzania

Taratibu za kufuata ili kumiliki Silaha ya Moto Tanzania

Taratibu ni hizi.
Maduka yanayouza kama uko dar ni mzinga corp. lilikoko upanga karibu na makao makuu ya Jeshi na Tanganyika Arms liliko stesheni na kama upo mikoani haswa moshi au Arusha Mwanza nk.
Ukifika pale ukishachagua silaha utapewa utaratibu wote na fomu.
Fomu zina sehemu yako ya kujaza, pia ina sehemu ya kujazwa na serikali ya mtaa wako, kata yako, polisi wilaya, mkoa na Taifa.
Kama hujawahi pata mafunzo pia utaelekezwa.
Cha muhimu ni sababu kwanini unahitaji hiyo silaha.
 
Babu nimepita hiyo njia sema aliyenifanyia mimi ametangulia mbele ya baba wa mbinguni. Ukifata watakavyo utamaliza kwa masharti ya leseni utamaliza miaka 5. Sbb inaanzia kwa mjumbe wako huko ngazi za juu baba vikao mara 1kwa miezi 6 saa nyingine hakuna vikao kabisa. Sijuwi labda mwendo wa Magu umebadilisha.
Kama inachukua miaka 5 kupata, hizo wanazotamba nazo huko Bar hao watoto wadogo wanazitoa wapi?!!
 
Juzi imegoma kutoka ikavimbisha mtutu,ilikuwa nimpasue kibaka ya uso mungu wake akamsaidia.

Sasa nataka kujua utaratibu wa kubadilishiwa pistol nyingine,je ni maombi upya au vipi?
 
Wanazotamba nazo watoto ndio hizo short cut ya paper work. Wanamwaga mpunga ndani ya mwezi wanatoa bar kutambiana.
 
Ukienda pale Mzinga au Ta Arms watakupa all details
 
MIE KESI YANGU NI TOFAUTI KIDOGO NI KUWA NINA BUNDUKI NATAKA KUIUZA NINUNUE PISTO HAPO JE TARATIBU ZINAKUWAJE?
 
Taratibu ni hizi.
Maduka yanayouza kama uko dar ni mzinga corp. lilikoko upanga karibu na makao makuu ya Jeshi na Tanganyika Arms liliko stesheni na kama upo mikoani haswa moshi au Arusha Mwanza nk.
Ukifika pale ukishachagua silaha utapewa utaratibu wote na fomu.
Fomu zina sehemu yako ya kujaza, pia ina sehemu ya kujazwa na serikali ya mtaa wako, kata yako, polisi wilaya, mkoa na Taifa.
Kama hujawahi pata mafunzo pia utaelekezwa.
Cha muhimu ni sababu kwanini unahitaji hiyo silaha.
Mzinga corp ndio kwa wapi asee , maana nipo upanga hapa. Au naingia kabisa huku makao makuu kwa davis??
 
Mzinga wapo ukiingia hilo geti karibu na Tumaini hospitali. Ukiwaomba hapo getini watakuelekeza.
 
Kuuza silaha ni issue nyingine na kununua nyingine ni issue nyingine.
Jamaa wa hapo Tanganyika Arms ndio wajuzi zaidi.
 
hata mimi nahitaji sana pistol ila sijajua taratibu za kuipata ni muhimu sana hii kitu kwa usalama binafsi
 
Mkuu mimi ninavyofahamu kama unataka kumiliki kwa mara ya kwanza utaratibu ni huu:

1. Utanunua silaha kutoka maduka ya Mzinga Corporation au Tanganyika Arms Ltd au kutoka kwa mmiliki halali ambapo utakuwa na mkataba wa mauziano na pia kitabu cha umiliki wake (kama umenunua kwa mtu). Hiyo silaha hautapewa ila itabaki mikononi mwa uhifadhi wa Mzinga Corporation, Tanganyika Arms au central police station na wewe kupewa nakala ya Receiving Note kuonyesha kwamba silaha imebaki mikononi mwao kwa utunzaji. Kama ni silaha ya urithi basi kuwepo na muhtasari wa kikao cha wanandugu kilichoridhia wewe kumilikishwa silaha hiyo (wakati huo silaha inayotakiwa kurithiwa ikiwa mikononi mwa moja ya hizo sehemu nilizotaja hapo juu).

2. Utaenda polisi (mfano ofisi ya kamanda wa polisi wa wilaya) na kupewa fomu utakayotakiwa kuijaza maelezo yako kama jina, unapoishi, sababu za kuhitaji silaha, maelezo ya silaha uliyonunua.

3. Fomu yako itatakiwa ipate maoni ya serikali yako ya mtaa, kamati ya ulinzi na usalama ya kata yako (hawa watatakiwa pia kuandika muhtasari kuonyesha kuwa wamekujadili na kukukubalia). Hapa inaweza kuchukua siku chache tu au muda mrefu. Itategemea na UCHESHI wako.

4. Utatakiwa kupitisha fomu yako kwa hakimu au mwanasheria. Hapa ni suala la dakika chache tu na uchakavu kidogo.

5. Utatakiwa uende polisi forensic department kuchukuliwa alama za vidole kupata clearance certificate kuonyesha kuwa hauna kosa lolote la jinai. Kuchukua alama na kupata majibu ni ndani ya kama siku tatu hivi japo kuna uwezekano pia wa kupata majibu siku hiyo hiyo. Na kwa ujumla hapa hapana usumbufu wowote. Kuna malipo kidogo utalipia. Kama sikosei ni Tshs. 3,000/= au 5,000/=.

6. Ukiwa na muhtasari huo wa kamati ya kata, barua yako ya maombi (covering letter), clearance certificate ya Forensic department, fomu yako iliyokwisha sainiwa na ofisi ya serikali ya mtaa, kamati ya ulinzi na usalama ya kata, hakimu au mwanasheria utavipeleka ofisi ya kamanda wa polisi wa wilaya ili nae akusainie covering letter yako na ile fomu yenye maelezo yako na silaha. Hapa ndipo uchukua muda kwani lazima kuwe na kikao cha kamati ya ulinzi na usalama cha wilaya kitakachokaa na kujadili maombi ya watu wengi na wewe kutakiwa kuhojiwa mbele ya hiyo kamati ambayo vikao vyake ufanyika mara moja moja. Ukikubaliwa muhtasari wa kikao utaandaliwa na nakala yake kuambatanishwa kwenye maombi yako. Kama nilivyokwishasema hapa ndipo nyaraka zinaweza kukaa muda mrefu zaidi nadhani kuliko kwingine pote (hata miezi kadhaa) kwa sababu vikao vya kamati ufanyika mara moja moja.

7. Kamanda wa polisi wa wilaya ambaye ndiye katibu wa kamati ata forward hizo nyaraka zako ili zikapitishwe pia na kamanda wa polisi wa mkoa, kamanda wa polisi wa kanda maalumu, na hatimae kwa Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai ambaye ndiye anaetoa kibali cha umiliki wa silaha husika. Huku kwa kamanda wa polisi wa mkoa, kamanda wa polisi wa kanda maalumu na pia kwa Mkurugenzi nyaraka hazikai sana.

8. Kibali hicho uwa valid kwa muda wa miezi mitatu na usipokilipia ndani ya muda huo utalazimika kwenda ofisi ya Mkurugenzi ili kuongezewa muda wa kulipia kibali hicho.

9. Ukishalipia hicho kibali utaenda wizara ya mambo ya ndani makao makuu (kwa watu wa Dsm) ili ukaandikiwe kitabu cha kumiliki silaha kwa jina lako na pia chenye picha yako (Firearm Licence). Zoezi hili linahitaji muda mfupi tu siku hiyo hiyo.

10. Utachukua kitabu chako na kwenda ofisi ya kamanda wa polisi wa mkoa ili uandikiwe kibali cha kukuruhusu kununua risasi (haichukui muda-dakika chache).

11. Utaenda ulipohifadhi silaha yako (Mzinga au Tanganyika Arms au central police station) ukiwa na leseni yako na pia kibali cha kununulia risasi na hivyo kukabidhiwa silaha yako na pia kuuziwa risasi kwa idadi iliyokubaliwa kwenye kibali. Hapa utatakiwa kulipia storage charges za hiyo silaha tangu ulipoiacha hapo hadi siku hiyo unapotaka kuichukua.

12. Baada ya kupata leseni ya umiliki wa silaha kila mwaka (kuanzia Julai hadi Septemba) unatakiwa kulipia leseni yako. Baada ya Septemba utatakiwa kulipa na faini.

Kwa mtu anaebadilisha kunakuwa hakuna mlolongo mrefu kama hapo juu. Ataandika covering letter kwenda kwa kamanda wa wilaya anayoishi akiwa na vielelezo vyote vya silaha mpya na ya zamani. Lakini hakutakuwa na haja ya muhtasari wa vikao vya kamati za ulinzi na usalama vya ngazi ya kata na pia wilaya ambavyo ndivyo vinavyosababisha zoezi zima kuchukua muda mrefu na pia usumbufu usio wa lazima (hasa huku ngazi ya mtaa na kata kwani kama mjuavyo kila mtu anataka nafasi yake imwezeshe kupata mboga ya nyumbani na pia jioni kujenda heshima baa).

Angalizo: Mimi siyo polisi na wala siko ofisi zinazohusika kutoa leseni za umiliki wa silaha. Nilichoandika ndicho ninachofahamu kwa upande wangu kama mdau wa kawaida. Hivyo kunaweza kukawa na masahihisho fulani kwenye maelezo yangu kutoka kwa wenye ufahamu zaidi. Hata hivyo naamini kama masahihisho yapo basi yatakuwa si makubwa sana.
 
Hili la utoaji wa silaha kiholela ni Jipu linalotakiwa kutumbuliwa ,Rushwa ni kitu kibaya sana
 
Anzia kwenye serikali za mitaa unatuma maombi unajadiliwa kwenye vikao vya kamati ya ulinzi na usalama ukipitishwa unapewa kibali unaingia dukani kuchukua mzigo
 
Back
Top Bottom