Tarehe 18 Mei 1985: Shirika la kijasusi la KGB kulikuwa na idara iliyojulikana kama Directorate K

Nimemchana anachofanya sio poah angekua anakupa credit aisee ...... Kwa hyo hapo anaenda kujivutia pesa kiulain kwa kila kichwa 2500 telegram[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Hajakutukana, maana yule bwana ni mtata sana kama ukiingia anga zake [emoji28][emoji28]
 
Everyone has a price tag Ulimakafu kuja huku
 
Huyo buyoye ni nyoko na mwizi hafu Huwa analipishwa watu kwanini asirepotiwe Kwa copyright infringement Hana haya kweli, hata story ya yoga aliiba pia
Ni swala la muda tu.
 
Ni swala la muda tu.
Inabidi watu waanze kumu report Kwa copyright infringement maana huo ni wizi wa kazi na nguvu za wengine pia aweke source. Mange kimambi kawakomesha wote waliokuwa wanatumia habari zake Tena huko Twitter au Instagram uki report inafanyiwe kazi, haiwezekani mtu atumie nguvu and energy yeye aibe bila kutaja hata source this isn't fair huku yeye akauze hizo habari
 
Daah
 
19

Hili faili la Michael foot a.k.a agent BOOT lilifunua mambo mengi kidogo kwa upande wa bwana Oleg. Report mbalimbali zinasema kwamba huyu Michael foot alikuwa anapokea baadhi ya taarifa na majasusi wa urusi azitumie katika kampeni zake , hususan kuishawishi uingereza kuachana na kusitisha matumizi ya nuclear (. Nuclear disarmament ) . Kumbuka huyu bwana alikuwa ni mwanachama wa mrengo wa kushoto hivyo sera zake kipindi Cha kampeni aligusia kuitoa uingereza katika matumizi ya nuclear. Sera hizi alikuwa anapewa na urusi ,Kwa maana urusi au Soviet haikutaka nchi za magharibi kujizatiti katika kujijenga na kujilinda kupitia silaha za nuclear. Kwao waliona kama ni tishio. Repoti iliendelea kudokeza kwamba foot alitoa list ya wanasiasa ambao ni pro- Soviet kwa Russia na hivyo wangekuwa wanapewa fund na urusi ya kujiimarisha kisiasa na pia kuwapa Hela za matanuzi kipindi Cha holiday. Lengo la hizi fund lilikuwa ni kuwashawishi viongozi hao wawe na ushawishi katika kupinga matumizi ya nuclear ambao nchi za magharibi zilikuwa zimejikita katika kujiimarisha kiulinzi kutokana na tishio la umoja wa kisoviet enzi ya vita baridi. Pia bwana foot alitoa taarifa za maoni ya chama chake Kwa KGB kuhusiana na mtazamo wa uingereza kwenye maswala tata yaliyokuwa yanagonga vichwa kwa wakati huo ,kama uvamizi wa marekani nchini Vietnam,mauaji ya Kennedy na athari za kisiasa, na pia agenda kuu za mkutano wa Geneva kuhusu vita ya Korea 1954 . Nao KGB wangemtumia bwana foot katika kuyaeleza haya yote kwenye vikao vya chama na kitaifa kwa mtazamo ambao ungeegemea upande wa Russia. Kwa kifupi foot hata baadhi ya hotuba kuhusiana na maswala mtambuka wakati huo alikuwa akiandikiwa kwa msaada wa KGB. Alikuwa akitumika kueneza propaganda za Russia pasipo yeye kufahamu.
Mwaka 1967 bwana foot aliwapinga Russia hadharani kwa kitendo Chao Cha kuivamia Czechoslovakia. Russia wakaacha kumtumia na kuamua kumpuuzia. Lakini baadaye Russia wali resume tena mahusiano na foot baada ya kuchaguliwa na labour party kama kiongozi mkuu wa upinzani na ambaye alitarajiwa atapambana thatcher kwenye debe la kuwania u prime minister uchaguzi uliotarajiwa kufanyika. Ripoti mbalimbali baadaye zilisema kwamba endapo hizi taarifa za foot kuwa na mahusiano na KGB zingejulikana na mahasimu wake wa kisiasa hususan wa conservative , wangetumia kama fimbo ya kumchapa na kumpoteza kisiasa mazima . lakini bahati aliangushwa kwenye uchaguzi mkuu uliofuata wa 1984.
Kumbuka hili file bwana Oleg Gordievsky alilisoma mwaka 1981.



Tarehe 2 April 1982, nchi ya Argentina ilivamia visiwa vya faulkland vilivyokuwa chini ya uingereza kusini mwa bahari ya Atlantic. Huyu bwana foot alitaka hatua zichukuliwe za haraka kuhusiana na uvamizi huo wa Argentina. Margaret thatcher alituma kikosi kazi kudili na wavamizi huo. Hili tukio liliwachukiza sana Urusi hususan KGB na kupelekwa mwanamama huyu kuchukiwa na Urusi (Hadi Leo hii), kwa hatua zake za kuzima uvamizi huo. Kwani Moscow waliamini uingereza wangekuwa defeated katika kuuzima uvamizi huo. Russia walipanick sana katika tukio hili ,kwa maana hata Michael foot aliafiki kwa mpinzani wake wa kisiasa mwanamama thatcher kuchukua jitihada za kuzima uvamizi huo.
Ni kwamba uingereza au Britain kwa wakati huo ilikuwa katika vita baridi . Oleg alikuwa ameshachagua upande wake tayari [emoji39].





Baada ya Moscow kufanya clearance kwa Bwana Oleg , hatimaye mwaka tarehe 28 June 1982 alikwea pipa la shirika la ndege la Aeroflot Hadi London akiwa na mkewe Leila na wanao wawili. Ni kwamba akili ilikuwa inawaza mambo mengi ikiwemo taarifa za kijasusi alizozikusanya miezi minne akiwa anasubiri approval ya kusafiri.
Kifupi alikuwa amebeba kichwani mwake taarifa nyeti sana kwa wakati huo ikiwemo za agent boot au Michael foot . Na pia taarifa za majasusi wote walioko Jiji la London.
Lakini wanasema msaliti anakuwa na msaliti wake .



Tuachane na Oleg kidogo.tusonge Hadi marekani.


Aldrich Ames alikuwa ni afisa wa CIA ,mwenye maisha ya kawaida Lakini asiyekuwa na furaha kutokana na pandashuka ndani ya ndoa yake.
Huyu bwana kazi aliyopewa ya kuwaajiri na kuwatumia majasusi wa Soviet ndani ya mexico haikuwa na matokea yaliyotarajiwa na maboss wake ndani ya Langley Virginia makao makuu ya idara hiyo.Hakuthaminiwa ,na pia malipo hayakuwa mazuri na ndio ilifanya hata ndoa yake kuingia matatizoni. Alikuwa mzembe na careless sana kiasi Cha maboss wake kutomzingatia sana.
Huyu bwana alizaliwa huko river falls , Wisconsin mwaka 1941. Baba yake alikuwa ni academian na baadaye akawa anafanyia CIA kazi huko Burma.
Huyu Ames alikuwa ni mtu intelligent na pia Mtu mwenye ndoto kubwa za kuwa mbali kimaisha. Alijiunga na chuo Cha Chicago ila baadaye akaacha ,na kuanza kufanya part-time kama muigizaji. Baadaye alirudi na kupata degree yake ya kwanza na kujiunga na junior officer training course ndani ya CIA kwa kupitia connection ya mshua wake. Hii course ililenga kuongeza idadi ya majasusi kutokana na uhitaji mkubwa uliokuwepo wakati huo.
Alitumwa huko uturuki ambapo ndio palikuwa ndio center ya vita ya kijasusi kati ya west na east. Hii ni kwa sababu pia hapo uturuki palikuwa na military base ya marekani . Karibu na urusi kabisa .
Huko kazi yake ilikuwa ni kupandikiza majasusi wa Soviet na kukusanya taarifa kupitia wao. Pia kipindi Cha uvamizi wa Czechoslovakia na Russia , alikuwa na kazi ya kuchapisha vipeperushi vilivyoandikwa " Remember 68" lengo la hivi vipeperushi ni kuvimwaga kwenye dustbin kuwakumbusha waturuki kwamba nao wanaweza kuwa huenda nao watavamiwa na urusi kama walivyofanya kwa Czechoslovakia .
Mwaka 1972 alirudi Washington na akatumia miaka nne zaidi kujifunza ki Russia na kufanya kazi kwenye idara ya Soviet-east European department. Hii idara haikumvutia hata kidogo.
Hii ni kutokana kwamba kipindi hiki CIA ilikuwa inapigwa msasa kutokana na kashfa zilizokuwa zinaandama kitengo kwa wakati huo.
Kashfa zilizokuwa zinaandama shirika hili ni kwamba , ilisemekana Richard Nixon kwa wakati huo alipanga kuitumia CIA kuvuruga uchunguzi wa serikali kutokana na skendo maarufu wakati huo iliyomwandama ya WATERGATE SCANDAL. Pia serikali ya marekani ilikuja kubaini kazi chafu za taasisi hiyo ya usalama na kutaka kufanyike uchunguzi wa kina, tuhuma ikiwemo kupanga mauaji , matumizi ya binadamu kwenye kufanya tafiti (human experimentation), tuhuma za CIA kushirikiana na mafia,na vilevile tuhuma za kuwadukua watu pasipo ridhaa Yao. Sasa hizi kashfa ziliandama CIA kwa miaka 20 baadaye. Hii ilifanya mkurugenzi wake kwa wakati huo kujiuzulu aliyejulikana kama bwana James angleton pamoja na top staff wa shirika Hilo. CIA ndio kipindi ilianza kupoteza mvuto sana . Na hiyo tumbua tumbua ilikuwa ni bumpyride kwa maafisa wengi lakini haikumgusa Ames . Ilisemekana kwamba CIA ingetengamaa baada ya Miaka kumi baadaye ili iweze kurudi kwenye mstari na kupambana na KGB Ili liweze kuwa na ushawishi duniani.
Mwaka 1976 alipelekwa kikazi huko new York na baadaye akatumwa kikazi huko mexico 1981.
Wakuu wa CIA walianza ku notice tabia yake ya ulevi kupitiliza ,na kulalama kila wakati. Ila hakukuwahi pendekezwa aachishwe kazi.
Baadaye alimwoa Nancy segebarth. Kama Oleg tu ,ndoa yake ilikuwa na mvutano sana.
Akiwa meksiko kikazi hakuambatana na mkewe. Alikuwa akijihusisha na mahusiano na wanawake wengi .
Mwaka 1982 alikutana na mwanadada Rosario casas dupuy wa miaka 29 mwenye asili ya Colombia na ufaransa. Alikuwa mfanyakazi wa ubalozi wa Colombia hapo Mexico city.na ndipo walikutana na Ames kwenye diplomatic dinner party.
 
Nimemwona yaani we acha tu ,mpaka picha za humu kazipeleka kule yaani..dah...kwamba waende wakaisome telegram [emoji28][emoji28]
kwa jina naitwa Fortunatus Buyobe au ukipenda niite ndimu mkata shombo.

Kwanza naomba nijibu hoja yako moja kwa haraka sana bila kuikawiza

1. Kwamba nimekukopy na hadi nimechukua picha zako. Swali ni, ni wewe ndiye umezipiga picha hizi? Kama sio unajimilikishaje hakimiliki?

2. Kwa msisiti mkubwa ni kwamba sijakunukuu, siwezi kukunukuu na uwezo wangu wa kuandika tayari upo dhahili (mnyonge mnyongeni haki yake mpeni) ni kwamba members humu humu watapika consistency yako ya uandishi. Wataangalia chapisho lako la jana, la leo na la keshokutwa kisha kila kitu kitakuwana baina yako nami.

3. Hapa ndio pa muhimu zaidi. Bwana Oleg Gordievsky habari zake zimeandikwa sehemu nyini sana.

Naomba niseme wewe Story yako umeicopy hapa na kuitafsiri kwa kiswahili 👇


So hii ni open source document don’t own any rights na mbaya zaidi hukuwa mbunifu bali umecopy neno hadi neno.

Mimi bwana Oleg nimemsoma kulitia mwandishi BEN MACYNTYRE aliyefanya naye mahojiano. Hata hizo picha unazodai kuwa ni zako umezitoa kwenye hints za kitabu chake cha A SPY AND TRAITOR hivyo HUNA CHOCHOTE KILICHO CHAKO.

Mimi nina vyangu. My flow, Mpangilio wa matukio, na haya hayajionyeshi kwenye hii stotu tu bali na nyingine nyingi.

Karibu Telegramm utakuta story hii inaitwa THE MOLE, mle ndani imeanza na kina Aimes, Hanssen na ikaishia na Oleg. Sasa jiangalie. Ungekuwa na Identity ya kueleweka ningekushitaki
 

Mwanaume anajiitaje ndimu mkata shombo[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Wanaumeeeee hapa kuna mwenzenu kweli?[emoji2094][emoji2094][emoji2094][emoji2094]
 

Boss tuendelee usijibu negative comments
Watu tunafatilia tuwekee vitu leo weekend muda wa kusoma upo
 
Broo punguza vitisho,alaf pia na wewe umezidi nakumbuka kuna story kama sio ya UMUGHAKA sijui n nani nayo uliitoa humu ukawa unairusha kule kwako,alaf pia umshtak mtu kwa kipi kaka?hii kuburudika tuu au kuna kingine?

Ukweli n kwamba umeona jamaa anatoa hii story ukaamua kwenda kuitafuta ukaipa kichwa kingine ili watu watoe 2.5k per monthly,na naimani hakuna mwenye hati miliki ya hii story kwan hata wewe mwenyewe umeikopi mahali,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…