Tarehe 18 Mei 1985: Shirika la kijasusi la KGB kulikuwa na idara iliyojulikana kama Directorate K

Leo uhakika .. NAMI na majukum ya kulijenga taifa . Ningetype the whole story endapo ningepata laptop sema ndio hivyo natumia simu...na pia jana shamrashamra za gem
 
Majasus umekuja
 
Ila hii tabia ya kuleta story nusu nusu haifai, jitahidi ukiandaa story imwage yote tuache wasomaji tuangaike nayo.

Uko vizuri thou.
Na inabidi iwepo hata kanuni ya kuwapiga ban milele maana ishakuwa utamaduni Sasa wa JF , mtu sio storyteller anachukua sehemu analeta , akiona msimuliaji kakoma kusimulia na yeye anaishia hapo
 
SEHEMU YA 3

Stalin alikufa mwaka 1953.Aliyemfuata baada ya yeye kufariki alikuwa ni Nikita khrushchev. Miaka mitatu tu toka afariki Stalin aliyemfuata alianza kuuponda utawala wake kwa kuwa ulikuwa wa kimabavu akiwa anahutubia mkutano mkuu wa 20 wa chama .Baba yake Oleg alipigwa na butwaa sana na akaamini huenda ndio itikadi za kijamaa zinaenda kufa kutokana na sera za Nikita. Kwani wafungwa wa kisiasa waliachiliwa,masharti ya censorship yakalegezwa n.k. Hiki ni kipindi ambacho mambo ya umagharibi na uhuru ulianza na raia wakaanza kuona hafueni . Kwa upande wa mzee Anton hakufurahishwa( mlinda legacy[emoji1]) lakini kwa mwanaye ilikuwa ni ahueni.
Akiwa na miaka 17 Oleg alijiunga na Moscow state institute of international relations. Huko alivutiwa na maisha ya chuo . Alijihusisha pia na deep discussion kuhusu sera za nchi yake za usosholisti
.kwa kifupi alianza kuamini katika mrengo wa kibepari(hakuonyesha waziwazi).lakini asijue kwamba mle chuoni kulikuwa na spies wa KGB. Akaonywa kiaina na wenzake. Na pia alikuja kugundua mambo hayajabadilika kabisa . Hii ni baada ya urusi kuivamia Czechoslovakia, raia wa huko wakiandamana kupinga kuwepo kwao ndani ya umoja wa Soviet. Lakini maadamano yalizimwa na ikapelekea umwagaji mkubwa wa damu.

Hiki chuo kilikuwa ni chuo Cha hadhi ya juu sana kwa wakati huo kiasi kwamba Henry Kissinger aliwahi kukiri mwenyewe na kusema ni "Russian Harvard". Chuo hiki kilikuwa chini ya wizara ya mambo ya nje ilikuwa ndio tunaweza kusema breeding ground ya wanadiplomasia, wanasayansi,wachumi,wanasiasa na zaidi training center ya majasusi wa KGB.
Akiwa hapo Oleg alijikita kwenye masomo ya historia, geography,uchumi pamoja na mahusiano ya kimataifa,yote ya haya masomo yakiwa yamejikita katika itikadi za kikomunisti. Taasisi hii pia ilikuwa inafundisha lugha 56 zaidi ya chuo chchote duniani kwa wakati huo. Kujifunza lugha chuoni hapo ilikuwa ni njia na sababu ya kupata ajira nje ya nchi kwa mwana KGB. Na pia ni kwa sababu kilikuwa special kwa ajili ya ujasusi.Oleg kwakuwa alijifunza kijerumani tokea akiwa mdogo aliamua kujifunza kingereza,lakini kaka yake akamlazimisha asomee kiswedish ambaye tayari ni mwajiriwa rasmi wa KGB . Kwani alimsisitizia kujifunza lugha hiyo kutampa mwanya wa kufanya kazi nchi za Scandinavia.
Chuoni hapo alikuwa anasoma magazeti ya nje hususan magharibi Japo yalikuwa machache lakini kulimpa mwanga Fulani wa duniani huko.
Akiwa na miaka 19 Oleg na rafiki yake wa chuo kwa wakati huo aliyeitwa stanislav kaplan walianza mazoezi ya kujijenga miili Yao . wakaaanza kufanya cross-country running kama sehemu ya kuweka mwili fiti.hii ilikuwa ni sehemu ya course hapo chuoni. Huyu rafiki yake alikuwa anasoma kozi fupi za kufanya tracking mwenye asili ya Czechoslovakia. Yeye tayari alikuwa na degree yake tayari aliyoipata kwenye chuo Cha Charles mjini Prague. Na kuja kwake hapo chuoni ni kwamba alichaguliwa kama wale the best and gifted students ndani ya muungano wa Soviet.
Kwa kuwa walikuwa ni marafiki walikuwa wanashare baadhi ya mambo na namna gani hawakuwa wanavutiwa na mfumo wa taifa lao kwa maana walihisi kama wamefungwa akili na propaganda za nchi Yao. kwa kuwa walikuwa ni vijana rijali na wenye muonekano wa kuvutia ,walikuwa ni Magnet kwa wanawake wengi hususan walipokuwa wakipata maakuli kwenye mkahawa mmoja kitingoji Cha Gorky park. kwa hiyo kukaa hapo waliweza kujirusha na bebezi.
kaka wa Oleg ,Vasili yeye tayari alikuwa ameajiriwa ndani ya KGB kama illegal ndani ya kundi kubwa la majasusi waliosambazwa duniani.
huyu Vasili alikuwa ni majasusi kwenye kundi la illegal au kwa kirusi ni Nelegal.
Iko hivi wanasema urusi kulikuwa na aina mbili za majasusi .legal na nelegal. Kuna wale wanatumwa kukusanya taarifa za Siri kwenye nchi Fulani wakijifanya wafanya biashara,wafanya kazi kwenye mashirika ya msaada, wahisani,walimu, waandishi wa habari n.k. . Na wanakuwa na majina feki, passport feki na utambulisho batili. Hawa ikitokea wamekamatwa ina kula kwao mazima na nchi inawakana kama raia wao endapo wamekamatwa . Kwa kifupi wanakuwa hawana formal cover na ni sleeper agents. Sasa Kuna wale ambao ni legal , Hawa wanakuwa na diplomatic cover. Hawa ni wale ambao ni wafanyakazi wa ubalozini (consular staff) akiwemo na balozi mwenyewe [emoji1]. Hawa ikitokea wanahusishwa na ujasusi/uhaini kwenye nchi Fulani mara nyingi hawawezi kushtakiwa wanakuwa declared persona non grata na kufukuzwa na nchi hiyo ndani ya masaa 24 au 72. Hawa Sasa wanakuwa na formal/diplomatic cover .
Kwa hiyo bwana Vasili yeye alikuwa ni illegal aliyeajiriwa mwaka 1960 na FCD (First chief directorate). ndio aliyemshauri bwana mdogo asomee lugha ya kiswedi. Na ndie aliemtambulisha mdogo wake kitengoni kwa mabosi wake wa kitengoni FCD. Hichi kitengo ndani ya KGB kilikuwa kinajihusisha na ujasusi wa nje ya urusi.
Mwaka 1961 bwana Oleg Gordievsky alipata mwaliko wa ghafla na akapewa maelekezo aende kwenye jumba Moja karibu na makao makuu ya KGB lililoko mitaa ya Dzerzhinsky.



Bwana Oleg kwenye miaka yake akiwa chuoni.

Oleg akiwa kwenye sare za KGB
 
Na inabidi iwepo hata kanuni ya kuwapiga ban milele maana ishakuwa utamaduni Sasa wa JF , mtu sio storyteller anachukua sehemu analeta , akiona msimuliaji kakoma kusimulia na yeye anaishia hapo
Kwanini unaniombea kupigwa ban?
 
Tamu nene ila fupi.....
 
Kitasa cha tatu bado tunakikumbuka, natumaini utarudisha kule kwenye muendelezo wakati ametoka Uingereza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…