kina kirefu
JF-Expert Member
- Dec 14, 2018
- 15,188
- 18,583
Hapo pa akijua jambo I think ili aonekane genius no one like him/ her.Na wengine wanaamini anachokijua basi mwingine hakijui. All in all hii thread imekimbiza sana sikutegemea.....tukipata wasaha tuta share nondo... Sema Kuna kitabu Fulani hivi kimendikwa na mwanamama anaitwa Stephanie mayer.. kinaelezea jinsi uingereza ilivyochangia kuwahifadhi wale magaidi walioitingua world trade center na pia kulipuliwa kwa usafiri nadhani kama sio wa basi ni treni za underground nchini uingereza. Japo uingereza ilionywa kuhusiana na sera yake ya kukaribisha wahamiaji wa kila nchi kutakuwa na madhara hapo Baadaye viongozi wa serikali wakakaza kichwa ,matokeo yake ugaidi ukashamiri. Changamoto ya hiki kitabu kwa mujibu wa mwandishi kina utata sana .
Kwahiyo Fortunatus Buyobe ni mchawi??Mkuu hao ni wachawi tu na kama ilivyo desturi mchawi hataki kitu anachokijua yeye basi na mwingine akijue Aaaa Never asee.... Hawa ni wachawi kabisa na ni wachawi wa maarifa ama ujuzi na ni wabinafsi wasikuumize kichwa we endelea kushusha Nondo hii vita tutashinda tu.
Natamani tupate visa vya CIA, MOSSAD, BND na Ofcoz FSB na hao MI6 Hawa ndio inaelezwa kwamba ni wababe wa UJASUSI ijapokuwa tutaambulia za zamani sana ambazo sio CLASSIFIEDS kwa sasa. Hawa wakwetu sidhani ata kama wana issue yoyote ya maana [emoji38]
Hilo buyobe uwa ni lina ufala mwingi na bichwa lake kama tikitiKwahiyo Fortunatus Buyobe ni mchawi??
Another Code?
Tabu ya kusoma juu juu.Umesoma yote lakini????
Salute mkuu, shukran kwa burdan murua kabisa.36
Rumours kuhusiana na kutoweka kwa bwana Jasusi zilianza kusambaa sana ndani ya corridor za makao makuu ya KGB kwenye jengo la lubyanka. Idara ya directorate K ambao walikuwa na jukumu la kumfuatilia Oleg kila mahali waliamini kwamba lazima atakuwa yupo Russia , either amelewa na kufa ,au labda kajiua na kujitupa mtoni. Msako ulianza kwenye maeneo ya mito na maziwa yaliopo jiji la Moscow. Maafisa wengine wakasema labda alitoroka kupitia Iran kwa kutumia passport feki. Nae bwana Budanov akasema atakuwa labda amejichimbia mahali kwenye safe house za uingereza. Mkewe , Leila alifuatwa huko kwa baba yake alikokuwa kwenye mapumziko kwenye fukwe za bahari ya Caspian Hadi kwenye gereza la lefortovo kwa mahojiano zaidi..... Swali alilokuwa akiulizwa mara kwa mara ni MUMEO YUKO WAPI. Lakini huyu mwanamama hakuweza kujibu zaidi aliwaambia kama nyie hamjui afisa wenu Yuko wapi ,basi Mimi sijui alipo huku akilia. Baadaye huyu mama alipokuja kuambiwa na hao wanaomhoji, kwamba mumewe alikuwa anafanya kazi na waingereza hakuamini hizo stori na alikataa katu.
Oleg alishawahi mwambia asiamini lolote atakaloambiwa kuhusiana na yeye [emoji28].
Kiufupi watu wengi waliokuwa na uhusiano wowote wa karibu na Oleg hapo Moscow walihojiwa intensively lakini bado haikujulikana haswa yupo wapi Hadi muda huo...,......
Siku ya jumatatu ,Oleg(Mr. Hanssen muda huo akiwa London) alijikuta yupo kwenye ukumbi wa south ormsby hall kwenye mji mdogo wa Lincolnshire akiwa ameandaliwa hafla fupi ya kumpongeza kama mgeni wa heshima. Hakutegemea kutokana na uchovu aliokuwa nao . Aliwauliza maafisa wa M16 kama anaweza kupiga simu kwa mkewe lakini hawakukubali kutokana na kwamba ingewapa alert KGB.ilikuwa ni mapema sana
Oleg alipelekwa kuhifadhiwa kwenye ngome Moja iliyoitwa fort Monckton kama safe house iliyopo kitongoji Cha Gosport . Na safehouse hii iliitwa Military Training Establishment. .iMTE. Pia ilitumika kama kambi ya mafunzo kwa majasusi wa M16. Hapo alipewa debriefings za hapa na pale na kupewa treatment za hadhi ya juu. Lakini hakusita kuuliza kuhusiana na familia yake . Eneo Hilo la fort Monckton lilikuwa linalindwa maradufu na mara ya kwanza haikuwa rahisi kumtambua huyu mgeni ni nani haswa kwa baadhi ya maafisa wengine wa M16. Lakini baadaye walikuja kumtambua ni nani huyu mgeni mpya waliyenaye.na alipewa jina la uficho la OVATION.
Kutoka SUNBEAM, NOCTON , PIMLICO Sasa ni OVATION. Kwa upande wa CIA wao walimtambua kama TICKLE [emoji28][emoji28].
Case ya Oleg ikawa imeingia rasmi kwenye phase nyingine. Kutokana na information alizowapa mashirika ya kijasusi ya nchi za west, zilisaidia sana kuepusha vita vya nuclear baina ya Soviet na west. Pia info hizi za Oleg zilisaidia kuwafichua Maafisa wa ngazi za juu wa kisiasa waliokuwa serikalini ambao walikuwa kwenye payroll za KGB wakiuza Siri.
M16 wakaanza kujiuliza maswali, Je wawaambie CIA na washirika wengine kuhusiana na hii operation ilivyofanyika na kufanikiwa? Au waitishe vyombo vya habari kwa ajili ya hii taarifa? Na Je baada ya mambo kutokea juu uhusiano wa uingereza na Russia utakuwaje? Uhusiano wa Thatcher na Mikhail Gorbachev utakuwaje? Na kingine M16 Walilopaswa kulifanyia kazi ni familia ya Oleg . Mkewe Leila na watoto wake . Haya maswali M16 Walikuwa wanajiuliza
Baadaye kupitia afisa mmoja wa KGB aliyeitwa vitaly virchenko aliyekuwa anatoa info kwa CIA ,aliwatonya kwamba Kuna jasusi wa KGB anayehusishwa kuifanyia kazi M16 yupo under house arrest akisubiri kesi yake itafikia wapi aliyeitwa Oleg . CIA kwakuwa walimjua kama tickle ,wakawapa info M16. Kupitia hii info M16 walituma maafisa wawili Hadi kwa bill Casey marekani kwenda kumpa A to Z ya Oleg Hadi kutoroshwa kwake. CIA walishangazwa na hizi taarifa zilipotuwa mezani kwao.
Bwana Casey aliamua kufunga safari Hadi fort Monckton kuonana na hii ASSET mpya ya M16 waliyokuwa nayo Ili kupata new infos za Russia kuhusiana na vita baridi na pia kutoa shukran zake binafsi kwa Oleg Kutokana na nondo zake alizokuwa anatoa kwa nchi za west na kuepusha uwezekano wa kutokea vita.... likapita
Miezi kadhaa baadaye Oleg alisafiri Hadi marekani chini ya ulinzi mkali ,Ili kufanya mkutano wa Siri na maafisa wa ngazi za juu wa Baraza kuu la usalama wa taifa la marekani . Maswali yote aliyoulizwa alijibu kwa ufasaha kuhusiana na Russia. Na pia alienda Hadi Langley makao makuu ya CIA kukutana na maafisa wa ngazi za juu wa kitengo kwa ajili ya kikao nao. Alipewa heshima zote alizopaswa kupewa na mambo mengine yakaendelea.....
Kipengele kikawa ni familia yake.
Kwakuwa M16 wanajua baadhi ya maafisa wote wa KGB wanofanya kazi under official diplomatic cover , waliamua kumtokea afisa mmoja wa KGB ambaye alikuwa ni mshauri kwenye maswala ya kisayansi kwenye ubalozi wa Soviet kwenye Jiji la Paris ufaransa. M16 Walimpa ujumbe wa Siri utumwe Hadi Moscow kuhusiana na kuiachilia familia ya Oleg. Mke na watoto wake. Ujumbe ulikuwa unawataka Soviet waiachilie familia la sivyo maafisa wote wa KGB London watimuliwe . Ilikuwa ni ultimatum kwa Russia na walikuwa na wiki mbili za kujibu. Huu ujumbe haukusema kama Oleg yupo uingereza au la .
Huku mkewe Oleg aliendelea kubananishwa kwenye geraza la lefortovo na maswali kuhusiana na alipo mumewe . Wanawe wakiwa shuleni walikuwa chini ya uangalizi wa KGB.Pia rafiki yake Oleg bwana lyubimov naye alitiwa ndani kwa ajili ya mahojiano kuhusiana na alipo mwamba . Majibu ni Yale Yale . Hakuna aliyejua alipo. Kwa kifupi hili sakata liliwatia watu wengi lockup. Je wapi alipo Oleg?
Mke wa Oleg alipoona maswali yanazidi aliwatolea uvivu waliokuwa wanamhoji na kuwaambia . Nanukuu " Look. Let's be clear. I was a wife. My job was to clean,cook ,shop ,sleep with him, have children ,share the bed and be his friend. I was good at it. I'm grateful he didn't tell me anything. For six years ....I was a perfect wife. I did everything for him . You , the KGB, you have thousands of people with salaries whose job was to check up on people . They checked him and cleared him .. And you come to me and blame me ?. Don't you think that sounds stupid? You didn't do your job. It wasn't my job,it yours. You ruined My life".. Huyu mama alikuwa sahihi.
Ujumbe wa siri wa Ultimatum ulipowafikia KGB kuhusu kuiachilia hii familia Lakini wakatia ngumu wakisema huyo ni msaliti na familia yake lazima ibaki Russia.
Ujumbe huu uliporudi uingereza kwa M16 ,wakaamua kuujibu kibabe zaidi.
Ofisi ya wizara ya mambo ya nje wakaamua kutoa info kwa media kuhusiana na Oleg kutoroka Russia,ila info haikuwa na maelezo ya Zaidi kuhusiana na kutoroka huko. Magazeti ya uingereza kama kawaida Yao vichwa vya habari vikawa kama ifuatavyo.. " The biggest fish ever Netted",[emoji28][emoji28][emoji28] lingine likaandika " Friend Oleg, Master Spy" , lingine likasema " Russia's Ace of spy ;the Super-spy who went West". Lingine likaandika kwa mbwembwe "Our Man in KGB"[emoji38]. Na haikupita muda tokea taarifa kwa umma itoke , serikali ya uingereza ikatimua maafisa Zaidi ya ishirini wa Russia Waondoke ndani ya masaa 48.
Nao Russia wakaamua kufukuza maafisa wote wa uingereza waliokuwa wakifanya kazi Soviet ikiwemo akina Arthur gee na mwezake Ascot ambao walimtorosha Oleg.
Ndani ya KGB wakubwa walianza kutupiana Mpira wa lawama . Kila kitengo ndani ya KGB kilitupa lawama kwa mwenzake kutokana na aibu hii ya mwaka kuhusu Oleg aliyewatoroka . Maafisa wote wa KGB kwenye Jiji la Leningrad walilaumiwa pia kutokana na uzembe walioonyesha mpaka jamaa akawatoroka kizembe. Wengi wa maafisa walifukuzwa kazi au kusimamishwa . Na hili varangati lilimkuta Hadi Vladimir Putin akiwa afisa wa KGB kwenye mji wa Leningrad . Wengi wa maafisa wenzake walitimuliwa .
Kutokana na aibu hii KGB wakaamua kutunga uongo kwa ajili ya kuihabarisha umma wa raia kwamba Oleg alitekwa na kutoroshwa na sio kwamba alitoroka mwenyewe kama inavyodaiwa[emoji28][emoji28][emoji28].
Siku mbili baadaye rasmi sasa maafisa wa uingereza kwenye msafara wa magari nane waliondoka Russia chini ya conyoy ya KGB kwenye ulinzi mkali kupitia mpaka wa Vyborg Hadi nchini finland.
Hatimaye tarehe 14 November 1985 kwenye mahakama ya kijeshi ilimkuta Oleg na hatia alisomewa mashtaka ya uhaini na kuhukumiwa KIFO in absentia.
Mwaka 1986 Oleg alialikwa na Margaret thatcher kwenye makazi yake kwa ajili ya pongezi[emoji3578][emoji3578][emoji108]. Na mwaka huo huo Oleg alikutana na Ronald Reagan kwenye oval office marekani..
Huko Russia mke wa Oleg aliendelea kushikiliwa under house arrest kwa kisasi na KGB asije kutoroka kama mumewe.[emoji28][emoji3578]. Pia KGB walimwambia Leila endapo akitoa tamko la kuachana na Oleg au talaka Mali zake atarudishiwa zilizokuwa zimeshikiliwa .
Miaka sita ya mivutano kati ya Russia na uingereza kuhusiana na hii familia ya Oleg iliendelea. Uingereza ilitumia nchi washirika kuishinikiza Russia iachilie hiyo familia. Hata thatcher alipokutana na Gorbachev mwaka 1987 ,bado waliendelea kukaza.
Hatimaye ilipotimia 6 September 1991 Russia waliamua kuiachilia familia hii ya Oleg na kusafirishwa Hadi Heathrow London Kisha wakapelekwa na helcopter Hadi fort Monckton Oleg akiwa anawasubiri kwa hamu. Walifanyiwa homecoming ya kutosha . It was an emotional moment.
Miezi mitatu baadaye muungano wa umoja wa nchi za kisoviet ukavunjika RASMI.
Watoto wa Oleg waliendelea masomo shuleni na hawakutumia jina la Gordievsky kamwe .
Na mwaka 1993 Oleg na mkewe walivunja uhusiano wao wa ndoa RASMI. .......
Chukua maua yako mkuu..!!AFTERMATH.
Baada ya haya yote, kesi ya Oleg imebaki kuwa Case study kwa vyombo vya usalama vya nchi za magharibi Hadi Sasa. Kutokana na hadhi aliyopewa ,ameshasafiri nchi mbalimbali za dunia , ikiwemo New Zealand, South Africa, Australia, Canada, ufaransa, ujerumani, Israel, Saudi Arabia na nchi za Scandinavia Katika kutoa Somo kwa Mashirika ya kijasusi ya nchi hizo. Nchi nyingi duniani zililazimika kubadili muundo wa kiutendaji kwa taasisi za kijasusi za nchi hizo kutokana na hili swala la Oleg.
Maafisa mbalimbali wa M15 na M16 waliohusika na kesi hii ya Oleg wengine ni wastaafu ,na baadhi wametangulia mbele za haki na wengine bado kazini mpaka stori hii ilipowekwa kitabuni. Na wengi wa maafisa walibadilishwa vitengo waliohusika na Hili swala la Bwana Oleg Ili kuficha identity zao .
Na kwa upande wa bwana Aldrich Ames , madhara aliyoisababishia CIA ni kwamba ilipoteza majasusi wake wengi kwa Siri alizokuwa anatoa kwa nchi ya Russia. Na inakadiriwa Bwana Ames alipata kiasi Cha Dola milioni 4.6 kutokana na information alizokuwa anatoa kwa Urusi na wengi wa majasusi wa CIA waliokuwa Soviet walipotezwa mazima.
Yote kwa yote bwana Ames alikamatwa na maafisa wa FBI tarehe 21 Feb 1994 ,akiwa na mpenzi wake Rosario dupuy na kutiwa ndani.
Miezi miwili baadaye alikutwa na kesi ya kujibu kuhusiana na ujasusi na akafungwa kifungo Cha maisha jela . Mkewe Rosario dupuy alikutwa na hatia na kosa la ukwepaji Kodi na kosa la kutaka kufanya uhaini , na alipewa kifungo Cha miaka mitano baada ya plea bargaining. Kwa Sasa Ames ni mfungwa namba 40087-083 na anaitumikia adhabu yake kwenye geraza la federal correctional institution Terra Haute huko Indiana marekani.
Baadaye Ames alipohojiwa akiwa gerezani 1997 Alikiri na kusema aliwasaliti wengi kwa ajili ya pesa na akasema hakuwahi mjua Oleg na hakumsaliti.
Swala la nani aliyemchomesha Oleg mpaka Sasa limebakia kuwa kitendawili au fumbo la imani.
View attachment 2615407
Aldrich Ames akitiwa pingu na makachero wa FBI muda mfupi baada ya kukamatwa 1994. Hii ni baada ya kuvujisha Siri za CIA kwa KGB kwa zaidi ya miaka 10.
View attachment 2615409
Aldrich Ames na mkewe Rosario dupuy wakiwa kwenye arrest photography.muda mchache baada ya kukamatwa . Rosario aliachiliwa baada ya kukamilisha kifungo chake ,ila mumewe Aldrich still yupo jela.
Credit: ziende kwa
1.Ben MacIntyre@The spy and the Traitor.2018
2. Duka la vitabu la Elite Bookstore pale Shoppers Plaza Dodoma
3.wana jf wote na wale wote walionipa maua yangu[emoji39][emoji39][emoji39] Appreciation kwao for their encouragement.
Ya Aldrich pia itaunganishwa hapa hapa tuendelee kuwepo au nyingine mkuuBado hatujamalizana naye😅
Wewe ni muungwana sanaShukrani ndugu..
Hili tatizo la wengi rumekua tukigugumia kimya kimya kwa kufikiri ni uzembe wa simu zetu tu.Futa app ya JF hiyo mpya download hii hapa ya zamani utainjoy https://www.apkmonk.com/app/com.quoord.jamiiforums.activity/
Kwamba ukifuta mpya ndio kila kitu kinaenda sawa mkuu?. Picha zitafunguka moja kwa moja?.Hili tatizo la wengi rumekua tukigugumia kimya kimya kwa kufikiri ni uzembe wa simu zetu tu.
Umetuokoa wengi asante, japo bado changamoto ipo baadhi ya picha hazifunguki mpaka itoke na kuongia tena mara kadhaa.
Nime uninstall app iliyokuwepo ambayo ni latest, nika install hiyo aliyotuma kwy link. Yes, inafungua baadhi ya picha moja kwa moja kuliko iliyokuwepo. Ile kufungua picha ilikua mtihani kama kukombeleza kopo la colgate ikiisha.Kwamba ukifuta mpya ndio kila kitu kinaenda sawa mkuu?. Picha zitafunguka moja kwa moja?.
Sasa wenyewe kwa nini wenye kuhusika wasiyafanye mambo yawe rahisi tu,bila kutafuta tafuta ufumbuzi?
Hakika , Japo wengine wanafanya kwa passionMaisha ya ujasusi Ni full kujistukia kama unasakwa hivi. Halafu kifo nje nje. Ni maisha ya mashaka mashaka tena muda wote wa maisha yako. Hata kama umestaafu hiyo kazi bado unaweza ukawa huna ule Uhuru halisi wa kuamua ukitakacho na muda mwingine kutafutwa kuuawa ksbb unajua siri nyingi za nchi.
Mfano hata kuamua kusafiri,unaweza kufuatliwa au hata kukataliwa kusafiri kwenda nchi fulani. Hata kama umestafu bado huna uhuru