Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hatari hii Mimi nasubiria tu updates niendelee kujifunzaKuchomeshwa..kuchomeshana.wao kwa wao .. tutaona huko mbeleni
Nilikuwa fasta Jana before sleeping story naisubiria ka msosiNakuona umeiwahi shemela cariha
Nipo nipocariha njoo huku.
Hahahaha 🤣🤣Nilikuwa fasta Jana before sleeping story naisubiria ka msosi
Emdelea na story hawajui flashback hawaMnaosema sijui niende kwenye kitasa nilipoishia .. someni post namba 83 amejibu .. unless otherwise story hii haitakuwa na maana .
Interesting story kazi nyingine zinahitaji usmart wa hatari Yani unaishi roho juu juu.SEHEMU YA SITA
Kama afisa yoyote wa KGB ,bwana Oleg alikata shauri na kuamua kuoa licha ya kazi iliyokuwa na majukumu mazito na hatarishi. Alimuoa Yelena Akopian mwanadada aliyekuwa na umri wa miaka 21 , mwalimu wa lugha ya kijerumani. Alikuwa ni nusu mwa Armenia na nusu mrusi na walikutana na oleg kwenye harakati za majukumu ya kazi za ujasusi. Kama tu Oleg, mwanadada huyu alikuwa anapenda maisha ya umagharibi na alikuwa ni wale akina dada wenye itikadi za ufeministi.
Kuoa kwa afisa wa KGB kwa wakati huo ilikuwa pia ni kigezo Cha kupanda ngazi ya cheo. Na ndivyo ilivyokuwa.
Baada ya kufunga ndoa ,mwishoni mwa mwaka 1965 ilikuwa ni siku iliyosubiriwa kwa hamu kubwa . Ilitoka post ya kufanya kazi ya ubalozini nchini Denmark. Ilitarajiwa kazi official ilikuwa ni ku deal na visa na pasi za kusafiria,usajili wa ndoa ,na kazi zingine official kama afisa wa ubalozini . lakini kazi yake Hiyo ilikuwa ni Kama cover kwa juu , majukumu yake kama JASUSI ilikuwa ni kupandikiza majasusi ndani ya nchi ya Denmark,kupokea infos,kutoa fund kwa majasusi na vilevile kuajiri na ku register majasusi. Kwa kifupi alikuwa na majukumu ya kusimamia shughuli zote za ujasusi nchini Denmark.
January 1966 majira ya kuanguka kwa barafu ndio siku bwana Oleg na mkewe Yelena walitua ndani ya Copenhagen. Kwao Jiji Hilo waliona kama wameingia kwenye ulimwengu wa kubuni wa fairy tales. Kwa kifupi Copenhagen lilikuwa ni Jiji safi, la kisasa na la kitajiri. Waliona kama wameingia mbingu nyingine ukilinganisha na Jiji lao la nyumbani la Moscow. Vilabu, maduka ya pombe,vyakula vya kila aina,bendi za miziki,maktaba na bustani za maua ya kila rangi yaliwavutia . Na ni Jiji ambalo everyone minds his/her own business . Na likiwa na polisi wachache mitaani na visa vichache vya uhalifu.
Walifika kituo chao Cha kazi . Ubalozi wa Soviet ndani ya Copenhagen kilichokuwa chini ya mwakilishi /ambassador Leonid yetsev ulikuwa kwenye kitongoji Cha kristianiagade kaskazini mwa Jiji .ilikuwa ni jengo la kisasa lenye bustani za kuvutia,kwao waliona ni kama villa park au aina ya resort ya kisasa . Sehemu ya uwanja wa michezo pamoja na social club. Aliishi yeye na mkewe kwenye apartment ya kisasa na kukabidhiwa Volkswagen beetle pamoja na euro 250 cash kila mwezi kama advance.
Ndani ya ubalozi huo kulikuwa na wafanyakazi 20 Maafisa sita tu kati ya hao walikuwa ni wanadiplomasia na wafanyakazi wa kawaida ila wote waliobaki walikuwa wanafanya kazi kwa niaba ya KGB,GRU. Yaani walikuwa ni majasusi.
Ndani ya ubalozi huo bwana Leonid yetsev ambaye ndie balozi mwakilishi alikuwa anajua kabisa asilimia kubwa ya wafanyakazi wake hapo walikuwa ni incompetent, hawakuwa serious na kazi na wavivu. Wengi wao walitumia pesa vibaya kulewa,kujirusha na totozi n.k kuliko kuzifanyia shughuli za kijasusi.Lakini kwa bwana Oleg alimuona mfanyakazi anayejituma,mchapakazi na pia alikuwa ni mwelewa wa lugha ya ki danish. Bwana Oleg majukumu yake yalikuwa ni kuprocess visa ,kuandaa nyaraka mbalimbali n.k .ila shughuli ujasusi yeye alianza kuzifanya muda wa lunch.Hii Ina maana kwamba wakati wa chakula siyo rahisi kushtukiwa kwa maana wakati mnakula huku mpo mnapiga stori na marafiki zako mnapeana na kubadilishana infos za kijasusi pasipo kushtukiwa kiurahisi.
Majukumu yake makubwa yalikuwa ni kusimamia mtandao mzima wa majasusi waliotapakaa pasipo pia kukutana nao USO kwa USO ,na pia asiwafahamu sura Wala Majina yao kabisa. Kwa mfano Oleg na majasusi wenzake walikuwa wanawasiliana kwa njia ambazo ni ideal zisizoweza kutambulika kiurahisi. Jasusi anaweza kuacha Ganda la chungwa kwenye Yale mabenchi sehemu za umma akimaanisha nipo hatarini, nafuatiliwa.Au unaweza kukuta mbegu za apple zimeachwa mahali ikiwa na maana jasusi huyo anaondoka nchi hiyo. Kwa mfano bwana Oleg siku Moja aliacha msumari uliokunjwa kwenye dirisha la choo Cha umma ,akiwa na maana jasusi Fulani akiuona akachukue kifurushi cha fedha kilichofichwa kwenye dustbin sehemu Fulani ya mji. Na labda jasusi huyo baada ya kupokea fedha hizo ,Ili kuonyesha amepata mzigo ,angeacha kizibo Cha bia kilichokunjwa kwa meno hapo kwenye dirisha la chooni. Hivyo ndivyo mambo ya kijasusi yalivyokuwa Yana operate.
Kwa kuwa bwana Oleg kazi yake kubwa ilikuwa ni kupandikiza majasusi ndani ya Denmark alihitaji pia kupata access ya registration ya raia wa nchi hiyo.
Ni kwamba nchini Denmark ,rekodi za vizazi na vifo vinasajiliwa na kanisa la kiprotestant la nchini humo . Hivyo Oleg aliamua kufanya forgery ya majina kuingizwa kwa ajili ya kazi za kijasusi. Hivyo alianza urafiki na kuwashawishi makasisi wa kilutheri Ili aweze kuwa na access na daftari la rekodi za usajili la kanisa Hilo. Hivyo alifanikiwa kufoji na kuingizwa kwa majina ya raia wa ki danish ambao kiuhalisia hawakuwahi kuwepo . Hii ni kwa sababu majina hayo angeyatumia kwenye ku process visa na kutengeneza alias hapo ubalozini kwa ajili ya majasusi aliokuwa anawajibika kuwasimamia.
Kiukweli mbali na kuwa mfanyakazi hapo ubalozini ,Oleg alionja ladha halisi ya uhuru wa magharibi. Alipenda miziki,watu wake,na pia zaidi uhuru kwenye swala Zima la mapenzi. Ikumbukwe nchi ya Denmark ndio nchi ya kwanza duniani ku legalize homosexuality miaka ya 1960s. Nchi hii swala la ngono lilikuwa ni kipaumbele kwao kama Huku kwetu kipaumbele ni kutafuta Hela .kwao ngono ilikuwa kama ibada na chakula kwao.
Kwa mfano Siku Moja aliwahi nunua majarida mawili Moja likiwa la mapenzi ya jinsia moja kwenye duka kubwa la bidhaa za ngono, kwa ajili ya kwenda kumuonyesha mkewe. Kiukweli haya mambo yalipigwa marufuku nchini mwao . Ni kwamba Oleg alipata a real taste of liberty.
Lakini wanasema ukiwa ugenini ni ugenini tu.
Shirika la ujasusi la Denmark PET( Politiets Efterretningstjeneste) lilikuwa ni shirika dogo Japo lilikuwa effective na vigilant. Majukumu yake yalikuwa ni Yaleyale kama mashirika mengine ya kijasusi duniani . Walianza kumuweka huyu bwana mdogo kwenye radar zao kufuatilia nyendo zake kimya kimya .
Kutokana na itikadi za kikomunisti ni kwamba wa danish yaani hao PET walikuwa na utaratibu wa mara kwa mara wa kufuatilia nyendo za maafisa wa ubalozi wa urusi.Na pia baadhi ya simu za hapo ubalozini zilikuwa zinasikilizwa kwa Siri kwa kuwa zilikuwa tayari zimefanyiwa bugging. Lakini pia ma technician wa KGB nao walikuwa wamefanikiwa kupenyeza mitambo Yao ya kunasa mawasiliano ya pET. Kwa kifupi kila mmoja alikuwa anamwinda mwenzake bila kujua wanawindana.
Oleg na mkewe walikuwa wanasaidizana kusikiliza mawasiliano ya Siri kutoka kwenye ofisi za PET na kuzi decode na kuzitafsiri Hadi kwenye lugha ya kirusi na kuzituma home.
Kwa kuwa bwana Oleg naye alikuwa tayari alikuwa ameshakuwa suspect na idara ya PET, alipewa jina la uficho Ili asisanuke kama naye yupo kwenye radar za majasusi. Alipewa jina la uncle gormsson. Hili lilikuwa jina la mfalme Harald gormsson mfalme wa Denmark wa Karne ya kumi.
Ni kwamba PET walikuwa na mashaka kiasi kama kweli uncle gormsson au Oleg jasusi wa KGB anayefanya kazi chini ya formal diplomatic cover. Wakaamua kuweka mitego ......
Jioni Moja bwana Oleg na mkewe walipokea mwaliko kuhudhuria kupata chakula Cha jioni kwa rafiki yake mmoja aliyekuwa afisa polisi wa kawaida . Wakiwa wametoka kikosi Cha majasusi wa PET waliingia kwenye apartment Yao na kupandikiza vipaza sauti sehemu mbalimbali ndani ya nyumba hiyo. Lakini kwakuwa jasusi ni jasusi bwana Oleg kabla ya kutoka alitilia mashaka huo mwaliko na akaamua kuchukua tahadhari. Kwenye Mlango wa kutokea nje ya nyumba Yao sehemu ya chini kabisa ya mlango alibonyeza matone kadhaa ya super glue . Yaani tone likawa limeshikana na mlango sehemu ya chini na sakafu. Hii ni kwa majibu ya mafunzo aliyopata SCHOOL 101.Wakati aliporudi alikuta ile glue imeachana .Hivyo akajua ndani kwake Kuna watu waliingia na kufanya Yao. Tangia siku hiyo akawa makini na kila atakachokisema na kuongea na mkewe wakiwa nyumbani.
Wanasema taaluma ya ujasusi ni kama mchezo wa paka na panya ,mchezo wa kuviziana na kuwindana.
Ingawaje maafisa wa KGB walikuwa na uwezo wa kukwepa kufatiliwa(dry -cleaning) na majasusi wa PET ,nao pia PET hawakuwa wachache ku target na kuwafuatilia maafisa wa ubalozi wa urusi hapo Denmark hususan kwa target Yao bwana Oleg.
PET ilikuwa inamfuatilia Oleg Hadi mitaa aliyokuwa anatembelea hususan maduka ya kuuza bidhaa za ngono. Kilichowapa alama ya taa nyekundu ni kwamba inakuwaje kwa afisa wa kiurusi anapendelea kusoma majarida ya mapenzi ya jinsia Moja /gay magazine. Kila nyendo za bwana Oleg zilikuwa noted kwa umakini wa Hali ya juu kwenye file lake. Na kwa mara ya kwanza jina lake lilileta question mark.
Hiyo sentensi ya mwisho.. hahahaha.Interesting story kazi nyingine zinahitaji usmart wa hatari Yani unaishi roho juu juu.
Hivi na intelligence yetu Ina vitu amazing kama hivi [emoji2][emoji2] au inteligensia ya police?[emoji28]
Ranatuchelewesha au kutafsiri ndiko kunamchelewesha
Kutafsiri KIRUSI balaa,..lazima unywe VODKA za kutosha,..Usikute jamaa kazidiwa na Alcohol 😂😂anatuchelewesha au kutafsiri ndiko kunamchelewesha
Kwa madini ya hii thread ukilinganisha na uhuni wa mapolisi na vyombo vingine naona tuko weupe mno aisee na hapo ilikuwa enzi za vita baridi kupamba moto [emoji28][emoji28] Sasa uki compare inachekesha mnoHiyo sentensi ya mwisho.. hahahaha.