Uchaguzi 2020 Tarehe 28/10/2020: Siku ya kuweka Historia kuu Tanzania

😒😒😒 Nafikiria MITANO TENA halafu vile namna vyuma vitatunyonga tukufe dah!
Ukiona mtu anasema mitano tena ujue tayari Ccm waneshachukua akili yake. Huwezi kumpigia kura Magufuli aendelee kuwa Raisi wa Tanzania kama umepewa akili timamu na Mungu.
 
Usifanye uamuzi kwa hasira,fanya ukiwa umetulia. Huyo unayempigia debe unadhani atatuajiri wote?! Uongo,hata Nchi zilizoendelea haziwezi kuajiri raia wake wote! Kodi wanalipa ili kupata mapato ya serikali, afya, elimu pia wanachangia. Uamuzi wa hasira siyo wa busara!
 
Hapana hawezi kutuajili wote Ila ataweka mazingira mazuri ya sekta binafsi kuja kwa wingi nchini Tanzania na kuajili watu wengi kuliko huyu magufuli wako ambaye ameharibu ukuaji wa sekta binafsi na kufanya wawekezaji kukimbia na maelfu ya watu kupoteza na kukosa ajira
 
Katika kipindi cha mitano ya awali ya JP amejenga misingi ya ukuaji wa uchumi, mitano ya sasa itatumia misingi hiyo kuleta ukuaji wa uchumi na ustawi wa jamii.
 

umejitahidi kuandika sana lakini ushindi haukwepeki kwa JPM: wewe ruka lala amka lia cheka
 
Wapiga kura huwa hawaamui wa kuwa madarakani, bali wahesabu kura.

Ni Ukweli ulio wazi CCM kupitia kikaragosi chao NEC(National Election Criminals) ndio wanao waamulia Watz Nani awatawale!!!
Ni ukoloni ulioje......!!!!
 
umejitahidi kuandika sana lakini ushindi haukwepeki kwa JPM: wewe ruka lala amka lia cheka
Mpaka kwa akili yako ya ukilaza umeona nimeandika kitu basi ujue huyo Magufuli wako hapaswi kuendelea kuwa Raisi hata kwa dakika 10 zaidi. Nakushauri na wewe fanya maamuzi magumu manaake najua hapo ulipo huna ajira ya kudumu wala huna uhakika wa pensheni endapo ikitokea umeezeka.

Nenda kapige kura kesho, kura ya ukombozi na mchague Tundu Antiphas Lissu kuwa Raisi wa Jamhuri ya Tanzania 2020-2025 ili aweke mfumo bora wa kukuhakikishia maisha bora wewe na uzao wako!!

ukipiga kura yako usiondoke bila kuilinda
 
Sote kwa pamoja tukamchague Lissu kwa kishindo, Tuifagie kabisa CCM na kero zake za kufukarika wananchi! Tarehe 28.10.2020 itakuwa ikiadhimishwa kama tarehe ya ukombozi wetu kila mwaka!
 
Katika kipindi cha mitano ya awali ya JP amejenga misingi ya ukuaji wa uchumi, mitano ya sasa itatumia misingi hiyo kuleta ukuaji wa uchumi na ustawi wa jamii.
Msingi upi aliojenga wa ukuaji uchumi??? Kuzuia wahaya wasiuze kahawa nje ya nchi na kuwa masikini??? Kupora korosho kusini na kusababisha umasikini mkubwa??? Au kuteka watu, kuua na kubambikia watu makesi???
 
Kesho nitaenda kibaha nikitokea chanika kumpigia tundu lisu
Safi sana. Hamasisha pia ndugu zako, jamaa na marafiki wakampigie kura Lissu hapo kesho. Waambie pia wasikae mbali na vituo vya kura kusubiri matokeo
 
Sote kwa pamoja tukamchague Lissu kwa kishindo, Tuifagie kabisa CCM na kero zake za kufukarika wananchi! Tarehe 28.10.2020 itakuwa ikiadhimishwa kama tarehe ya ukombozi wetu kila mwaka!
Amina. Lazima tarehe 28/10/2020 tutaiweka kama siku kuu ili kuashiria ukombozi wa Taifa letu na mwanzo mpya wa maendeleo ya nchi yetu.

Tuhamasishane tukapige kura kwa wingi kesho na tulinde kura zetu!
 
Msingi upi aliojenga wa ukuaji uchumi??? Kuzuia wahaya wasiuze kahawa nje ya nchi na kuwa masikini??? Kupora korosho kusini na kusababisha umasikini mkubwa??? Au kuteka watu, kuua na kubambikia watu makesi???
Inawezekana jich lako limeona hayo ambayo mimi siwezi kuyathibitisha! Lakini ninaona miradi ya kimkakati kama usafirishaji (ndege, barabara, viwanja, reli), umeme wa uhakika, formalization ya biashara, vituo vya kutolea huduma za jamii kama afya, elimu, kuingia uchumi wa kati, hisa kwenye madini, masoko ya ndani ya madini, kuboresha ushirika, uwezo wa Serikali kujitegemea kimapato, raslimali watu nk.
 
Mradi wa ndege una business plan ipi ya kutengeneza faida??? Ndege zetu zinasafiri wapi na wapi???

Barabara kajenga barabara ngapi magufuli??? Au fly-over ya mfugale ambayo mvua ya masaa 5 tu inasababisha ifurike maji???

Masoko ya madini yamefanya nini cha ziada??? Au unasikiliza takwimu zao za kupika izo na unaziamini???

Ushirika gani umeboreshwa??? Huo ambao haujalipa pamba kanda ya ziwa??? Huo ulioshindwa kwenye korosho na mbaazi??? Au huo uliofeli kwenye tumbaku na kahawa na wakulima wamekuwa wasikini wa kutupwa???

Unasema serikali inajitegemea kimapato, kivipi???? Wakati kila siku tunaona katibu mkuu wizara ya fedha akipokea fedha za misaada kutoka kwa wazungu???
 
Ni siku ya mapinduzi ya kweli ya kumwondoa Mkoloni mweusi kuitawala nchi yetu ki mabavu.
 
Ni siku ya mapinduzi ya kweli ya kumwondoa Mkoloni mweusi kuitawala nchi yetu ki mabavu.
Amina, na Mungu atutangulie katika kufanikisha hili. Abariki na afanikishe hili kwa Jina la Yesu
 
Iwe! Pole sana, ninaona una hasira, Nchi hii ni yetu hatutaijenga kwa hasira bali kwa Busara kubwa na utulivu,wala tusifanye majaribio. Ninakushauri chagua maendeleo usichague maneno! Umeuliza maswali mengi sana nitayajibu hata kwa hatua. Naanza na Idadi ya Flyovers msikilize Mwenezi kwenye vidio iliyoambatishwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…