Tarehe 29 Oktoba, piga kura yako mapema na nenda nyumbani

Hakuna haja ya kumlazimisha mtu asiende kupiga kura kwa sababu wewe umeamua hivyo. Kupiga kura ni jambo muhimu lakini ni la hiari.

Kama chama chako kimejitoa tulia nyumbani waache wale ambao vyama vyao vinashiriki wakapige kura.

Kama chama kilichojitoa ndio kinapendwa sana basi majibu yatapatikana siku ya tarehe 29/10, tutakapoona vituo vingi vya kupigia kura vikiwa wazi bila watu waliojitokeza.
 
Hujasema mbadala wako ni upi, kama ni kuandamana, halafu baada ya kuandamana itakuwa ndo unapata kiongozi mpya?
Unampataje katika maandamano?
Tujifunze civics na kuelewa kuwa mtu hudai haki tu lakini una wajibu wa kikatiba vile vile.
Usikute na wewe ni PhD hapo lumumba

Kwani baada ya maandamano ya Wafaransa kilitokea nini

Maandamano ya Nepal kimetokea nini?

Mbona maswali yako ya kijinga sana?
 
Hujasema mbadala wako ni upi, kama ni kuandamana, halafu baada ya kuandamana itakuwa ndo unapata kiongozi mpya?
Unampataje katika maandamano?
Tujifunze civics na kuelewa kuwa mtu hudai haki tu lakini una wajibu wa kikatiba vile vile.


Kuna kitu cha msingi unakikosa!

Unatakiwa kujifunza kuanzia leo:

1. Ukijua kuna uovu, cha kwanza kabisa, kama unaweza, ni kuzuia uovu usiendelee.

2. Kama huna uwezo wa kuuzuia uovu, the least you can do, ni kufanya kitu chochote kile cha kuonesha kuwa wewe siyo sehemu ya huo uovilu, na kamwe huwezi kuunga mkono uovu huo.

3. Kamwe kuubariki na kushiriki kwenye uovu, haiwezi kuwa njia ya kuzuia uovu.

Kwa sasa kushiriki uovu huu unaoitwa uchaguzi, ni kushiriki na kubariki uovu. Yeyote asiyeunga mkono utekaji, mauaji, udhulumaji haki za wananchi katika kuchagua viongozi wanaowataka, hastahili kwa namna yoyote ile kushiriki uovu huo unaobariki uovu unaoendelea dhidi ya Taifa na watu wake..
 
OLE WAKE MWANANCHI ATAKAYE ENDA KUPIGA KURA
OLE WAKE MWALIMU ATAKAYE SIMAMIA UCHAGUZI MWAKA HUU
OLE WAKE MGAMBO ATAKAYE SIMAMIA UCHAGUZI
 
Nimeuliza wenzako, what is the end game.
Sasa nikuambie wewe na wengine kama wewe, tangulia uanda ane badala ya kupiga kura, tutakuona kwenye luninga!
 
Kwa ground watu hawataki kusikia kitu inaitwa Uchaguzi 🤣 🤣 🤣, Mamaenu amechokwa mpaka Sebuleni kwakwe ni vile tu hawataki kumuambia ukweli.
 
Umetumwa kupima upepo?
Tupotupo hatueleweki na hatupangiwi ili tusieleweke!
 
Hujasema mbadala wako ni upi, kama ni kuandamana, halafu baada ya kuandamana itakuwa ndo unapata kiongozi mpya?
Unampataje katika maandamano?
Tujifunze civics na kuelewa kuwa mtu hudai haki tu lakini una wajibu wa kikatiba vile vile.
Mbadala ni kutafuta muafaka wa kitaifa kabla ya kwenda kupiga kura. Muafaka at the very least ni kuwa na tume huru, uchaguzi ulio huru, wazi, usawa na wa haki.

Tulipofikia tunahitaji kupata mifumo mipya ya kusimamia haki, utu, wa maisha ya kila Mtanzania, mali zao, haki yao kushiriki uchaguzi, kugombea, kuchaguliwa.

Tanzania inahitaji katiba mpya, mifumo mipya ya haki ili kuzuia umwagaji mkubwa wa damu unaotunyemelea wiki, miezi, miaka michache ijayo.
 
Zamani kulikuwa na ndio na hapana, sasa tunawekewa ndio zote, sasa hapo hatuna fursa ya kuchagua
 
Unapigia kituo gani nijekuhakiki kura yako?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…