Tarehe 29 Oktoba, piga kura yako mapema na nenda nyumbani

Kupiga kura kwa amani na kuondoka kwa mujibu wa katiba iliyoko ni sawa. Hili limekuwa linafanyika.
Tatizo lipo kwenye kipengele cha matokeo ya kura.
-Wizi wa kura na uhujumu wa chaguzi mambo ambayo yamekuwa yanatoa viongozi ambao kiuhalisia sio chaguo la wananchi, yamefanya watu wachoke kufanya hayo uliyoshauri hapo juu..

Kwa sasa watu WANATAKA haki yao, kipindi walipokuwa wanadai hiyo haki hakikutumiwa vizuri na watawala.

Nikuhakikishie, wasipoipata kwa wakati huu wakati ujao itakuwa mbaya zaidi.
 
😂😂😂afu usikute wew ndio mume wa dadangu 😖😖
 
Nakubaliana 100%
Ila give it enough rope to hang itself.
 
View attachment 3480672
Hongereni wana JF kwa kunipa dislikes nyingi.
Lakini vile vile hilo linaeleza jinsi civics illiteracy ilivyoshamiri, hata uwanja huu wa Great Thinkers.
Watu wanashindwa kufikiri three steps ahead.
Pamoja sana mkuu..!
Muhimu katika hii mada yako umeweza kupata picha ni namna gani watu(bila kujali elimu yao) walivyochoshwa na aina ya uongozi wa ccm kwa sasa.

Hilo la watu kushindwa kufikiri hatua tatu mbele, huo ni mtizamo wako na ninauheshimu ila usitake kila mtu awe na mtizamo wako.
 
Jidu La Mabambasi unampigia nani anayeshindana na nani?
Unakipigia chama gani kinachopingana na kipi?
Tunaomba ufafanuzi.
Is it true kwamba kuna watu hawaoni kwamba hapa hakuna uchaguzi? Mtoto wa darasa la tatu anaweza kuona kinachoendelea inakuwaje mtu mzima asione?
 
Kura hatupigi na nyumbani atukai tukutane barabaran

Na maandamano yakinoga tusiwaone njee mnakuja kutuunga mkono tutawatia madole
 
View attachment 3480672
Hongereni wana JF kwa kunipa dislikes nyingi.
Lakini vile vile hilo linaeleza jinsi civics illiteracy ilivyoshamiri, hata uwanja huu wa Great Thinkers.
Watu wanashindwa kufikiri three steps ahead.
Title yako inasema piga kura yako mapema uende nyumbani. Umeshindwa kabisa kungamua kwamba Tanzania sasa hivi inapitia changamoto kubwa kuliko hiki kiini macho kinachoitwa uchaguzi, ni changamoto kubwa kuliko wakati wowote.

Kuna hatari kubwa nchi kuingia kwenye machafuko makubwa kama hii serikali itangangania kuendelea kukaa madarakani kwa nguvu kutumia ubabe, polisi, usalama, magereza, mahakama, tume. Muafaka wa Kitaifa unahitajika ndio kuwa kipaumbele cha Watanzania wote wenye akili timamu na hata wasio na akili timamu, waliolamba asali, wanaokandamiza wenzao, na kuipa mnada nchi na maki zake zote kuhakikisha Tanzania bado itakuwepo.
 
Karatasi la kura lina choice nyingi, kwamba unayempenda hayupo si mwisho wa zoezi.
 
Vijana wenzangu, nguvukazi ya taifa hili punguzeni kuwajibu watu wanaotoa matamko kama haya. Wapo kupima upepo mpaka sasa zimebaki siku chache sasa wanataka kujua haya maji yanaspeed gani. Tusiwajibu kwa maneno tuwasuprise kwa vitendo. Over
 
Mkuu hata wewe?

..haiwezekani Ccm wapuuze madai ya mabadiliko tangu mwaka 1992 halafu Watanganyika tusichukue hatua.

..suluhisho ni kutokupiga kura, kwa maana nyingine kutowachagua.

..Sasa najua watajitangaza. Lakini kujitangaza katika uchaguzi uliogomewa, ni tofauti na kujitangaza katika uchaguzi tulioshiriki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…