Tarehe 29 Oktoba, piga kura yako mapema na nenda nyumbani

🙄🙄🙄🙄............!!!
 
Hujasema mbadala wako ni upi, kama ni kuandamana, halafu baada ya kuandamana itakuwa ndo unapata kiongozi mpya?
Unampataje katika maandamano?
Tujifunze civics na kuelewa kuwa mtu hudai haki tu lakini una wajibu wa kikatiba vile vile.
Wajibu wa kwanza wa kikatiba kwa kila mwananchi mzalendo, ni yeye binafsi kutokubali kushiriki jambo lolote ovu. Kinachoitwa uchaguzi kwa mwaka huu ni uovu unaolenga kubariki ushenzi unaoendelea wa kuteka na kuua watu, kupora rasilimali za nchi, na kupoka haki za watanzania. Ni watnzania maharamia pekee ndio watakaoshiriki tendo hili la kishenzi ambalo wahuni wamelipa jina la uchaguzi.

Wajibu wa pili wa mwananchi mzalendo, kama anaweza, ni kuzuia au kushiriki jitihada zozote zile zinazlenga kuzuia uovu. Hivyo kila mwananchi mwenye mapenzi mema kwa Taifa hili, kishiriki kikamilifu katika jitihada zozote za kuzuia au kubatilisha mipango ovu ya kuhalalisha uovu kupitia uhuni uliopangwa kufanyika Oct 29. Kama huwezi kuuzuia huo ushetani, basi usishiriki kwa namna yoyote ile.

Siku kutakapokuwepo uchaguzi wa kweli, hakuna mwananchi atakayesubiri kuhubiriwa akapige kura, kwani kila mwananchi anajua kuwa ni wakati wake wa kushiriki kuuweka uongozi wa nchi.

Kwa sasa, tukio la Oct 29 liendelee kubakia maalum kwa wahuni, wauaji na watekaji, wadhulumaji haki za wananchi, na wale washenzi wote waporaji wa rasilimali za Tanganyika.
 

Katika andiko lako tumepata thibitisho moja kuwa mtu mmoja anaweza kuwa mjinga mnafiki wa kiwango cha juu, akafundishwa na watu wengi, lakini akaamua kubakia na ujinga wake, na akaondoka anatamba kuwa ni yeye ni mwerevu, na kwamba wote waliokuwa wakimfundisha ndiyo wajinga!!

Illiteracy yako umeifanya literacy, na literacy ya wengine wote umeifanya ni illiteracy. Hiyo haishangazi, hasa kama mhusika amefikia kiwango cha kuanza kuondoka kutoka kwenye illiteracy na kuanza kuelekea kwenye brain disability.
 
Hatuwezi kunywa sumu, kwa sababu tu tunasikia kiu..!
 
Upige kura kisha uende nyumbani si bora ungeendelea tu kulala au uende kwenye mishemishe zako....TZ hakuna uchgaguzi bali ni uhuni uhuni tuj...kwa Tume hii iliyounganishwa na SISIEMU makao na NIDA ni kupoteza muda tu.
 
 
Nitakachofanya mimi ni juu yangu cha msingi ni kwamba usinishauri cha kufanya tarehe 29 kiwe cha tofauti au sio.
Fanya haki yako ya kikatiba nenda katulie kwako.
Utakachofanya tarehe 29 we na Lamomy ni kupika ugali wenu na matembele kuweka bundle kujificha juu ya dari na kuchungulia kwa millardayo kuona kama kuna mtu kaandamana
 
Utakachofanya tarehe 29 we na Lamomy ni kupika ugali wenu na matembele kuweka bundle kujificha juu ya dari na kuchungulia kwa millardayo kuona kama kuna mtu kaandamana
Wewe sisi sio soft km wewe hata kukata ugali huwezi..!!
 
Utakua wapi nikupitie nikufundishe kupangua mabomu ya machozi 😹
Kigwangala anasema alishawahi kukusanya wananchi elfu 5 kuwahamasisha waandamane na wakakubaliana ila walivyoskia sauti ya bom 1 tu wote walitokomea kusikojulikana akajikuta kabaki peke yake.

Usikute na wewe ulikua miongoni wa wale elfu 5
 
Utakachofanya tarehe 29 we na Lamomy ni kupika ugali wenu na matembele kuweka bundle kujificha juu ya dari na kuchungulia kwa millardayo kuona kama kuna mtu kaandamana
Tusiongee sana tusubiri tarehe 29 ndio utaona. Mimi binafsi nitatoka sio kwa ajili yangu bali kwa ajili ya kizazi ninachokiacha.
 
Kigwangala anasema alishawahi kukusanya wananchi elfu 5 kuwahamasisha waandamane na wakakubaliana ila walivyoskia sauti ya bom 1 tu wote walitokomea kusikojulikana akajikuta kabaki peke yake.

Usikute na wewe ulikua miongoni wa wale elfu 5
Sasa kuna mtu mwenye akili timamu anaweza akamsikiza Kigwa? 😹😹
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…