Sehemu ya Kwanza
Tarehe ya kuzaliwa uwa inabeba taarifa zote muhimu kuhusu maisha ya muhusika na hii ni kwa mujibu wa elimu ya namba (Numerology). Katika hatua ya mwanzo nitaanza kwa kuzungumzia kitu muhimu ambacho kinapatikana kwa kukokotoa tarehe, mwezi na mwaka wa kuzaliwa, kitakachopatikana katika ukokotozi huo kitaitwa Mzunguko wa maisha (Tafsiri Binafsi). Kuna mambo muhimu ya kuzingayia katika ukokotozi wa mzunguko wa maisha ambayo ni namba mama na namba kiongozi.
Namba Mama
Namba mama ambazo zitakuwa zikitumika katika uchambuzi ni 1,2,3,4,5,6,7,8,9, namba yoyote baada ya 9 inaweza kurudiswa katika namba mama. Zingatia mfano unaofuata
10=1+0= 1
27= 2+7= 9=
389= 3+8+9=20=2+0=2
Kila namba mama kuanzia namba 1 hadi 9 inakuwa imebebe nguvu maalum, na hiyo nguvu inakuwa imegawanyika katika pande mbili, nguvu chanya na nguvu hasi.
Namba Kiongozi
Namba kiongozi ni namba ambazo zina sifa maalumu, nazo ni 11 na 22, namaba hizi zinapojitokeza wakati wa kukokotoa uwa zinabaki kama zilivyo, zingatia mifano ifuatayo;
155= 1+5+5=11
949=9+4+9=22
Namba hizi zinakuwa zimebeba sifa za Namba Mama na Namba Kiongozi, zingatia mfano ufuatao;
155= 1+5+5=11=1+1=2
949=9+4+9=22=2+2=4
Wakati mwingine hizo Namba Kiongozi uwa zinaandikwa 11/2 na 22/4.
Sehemu ya Pili
Mzunguko Wa Maisha
Mzunguko wa maisha ni funguo ya kufungua kile ambacho mwenyezi Mungu amekiweka ndani yako wakati wa kukuumba. Hii ni namba ya kudumu katika kipindi chako chote cha uhai, daima haitabadilika kwa kuwa inatokana na tarehe yako ya kuzaliwa.
Mzunguko wa maisha utakuwezesha kutambua mambo unayotakiwa kuyatimiza katika kipindi chako cha uhai kwa kuzingatia fursa na vipaji ambavyo Mungu amekuumba navyo. Mzunguko wa maisha utakuwezesha kwa urahisi kufanya maauzi kuhusu;
Uelekeo wa maisha
Kupanga na kutimiza Malengo
Mahusiano
Mipango ya mbeleni
Kazi ambayo itakufikisha katika kilele cha mafanikio
Hivyo basi Mzunguko wa maisha utatuwezesha kutambua mazingira ambayo yataambatana na fursa ambazo Mungu ameziumba kwa ajili yako.
Mzunguko wa maisha ni namba inayopatikana kwa kuzipunguza tarehe, mwezi na mwaka wa kuzaliwa hadi kufikia katika Namba Mama au Namba Kiongozi, mfano wa kwanza unahusu Namba Mama na wa pili unahusu Namba Kiongozi
Mfano wa kwanza 21/04/1990
Tarehe 21= 2+1 = 3
Mwezi 04= 0+4= 4
Mwaka 1990=1+9+9+0=19=1+9=10=1+0= 1
Baada ya kupata hizo Namba Mama kutoka katika tarehe ya kuzaliwa, mwezi na mwaka unazijumlisha zote;
3+4+1=8
Mfano wa pili 14/01/1985
Tarehe 14= 1+4 = 5
Mwezi 01= 0+1= 1
Mwaka 1985=1+9+8+5=23=2+3=5
Baada ya kupata hizo Namba Mama kutoka katika tarehe ya kuzaliwa, mwezi na mwaka unazijumlisha zote;
5+1+5=11
Sehemu ya 3
MZUNGUKO WA MAISHA 1
Mzunguko huu unahusika na wale wote ambao ukokotozi wa tarehe zao za kuzaliwa unaleta jibu la 1. Kitovu cha mtu wenye mzunguko wa maisha 1 ni kujitegemea, mtu mwenye huu mzunguko lazima ajifunze na kuweza kusimama kwa miguu yake miwili ili kutumia vipaji vyake katika kuzitumia vizuri fursa atakazokutana nazo katika kipindi cha uhai wake. Bila kujitegemea malengo yako hayawezi kufikiwa.
KAZI
Mwanasiasa
Mtaalamu wa maabara
Msanii
TABIA CHANYA
Afya njema
Uongozi
Utawala na usimamizi
Kujiamini
Ubunifu
Ugunduzi
Shahuku
TABIA HASI
Majivuno
Ubinafsi
Kutopenda ushirikiano
Kiburi
Unyanyasaji
Ukatiri
Hofu
Kukosa uvumilivu
Woga
Kukosa hamasa/Kutojikubali
Maelezo/Ushauri
Mtu mwenye mzunguko wa maisha 1, katika hatua za awali za mzunguko uwa rahisi kwake kuwa tegemezi kuliko kujitegemea. Mtu yoyote mwenye mzunguko wa maisha 1, kama atatumia vema tabia chanya ambazo Mungu ameziweka ndani yake ana uhakika wa kufikia kitovu chake ambacho ni kujitegemea.
MZUNGUKO WA MAISHA 2
Mzunguko wa maisha namba 2 una maana ya Mahusiano na Ushirikiano, Mtu mwenye mzunguko huu ni muhimu kutumia uwezo aliojaliwa na Mungu kwa maslahi mapana ya umma, ingawa mara chache mchango wake utajulikana kwa umma wote. Mambo ambayo wengine watatumia nguvu kuyakamilisha yeye ataweza kuyakamilisha kwa urahisi, mara nyingi uwezo wa mtu mwenye mzunguko huu uwa unatumiwa na watu wengine. Pia ni muhimu kujifunza namna ya kuweza kufanya kazi na watu tofauti, furaha ya mtu huyu ni kuona kazi inafanyika hata kama sifa watapata watu wengine.
KAZI
Katibu Muhktasi,
Msanii,
Mfanyakazi wa Viwandani,
Mwanadiplomasia,
Mwanamuziki,
Muimbaji.
Mfanyakazi katika sekta ya elimu
Mfanyakazi wa Umma.
VIPAWA
TABIA CHANYA
Kujali Hisia
Machale/Maguto
Ushirikiano
Dilpomasia
Kupangilia Mambo
Uaminifu
Urafiki
Ulezi
Mikakati
Mvuto wa Kimapenzi
Upole
Uwakilishi
Kujali
TABIA HASI
Kuona Haya
Kutojali
Woga
Utegemezi
Kutopenda ushirikiano
Kuficha/Kukosa hisia
Kuendeshwa na hisia
Kujifanya mjuaji
Kutokutimiza maono
Kulaumu
MAELEZO/USHAURI
Mtu mwenye mzunguko wa namba 2 ili aweze kufanikiwa anatakiwa kudhibiti hisia zake, lazima afanye shughuli ambayo haitakuwa na madhara katika hisia zake kali ivyo kutokuwa anaumizwa. Muhimi kujifunza kukabiliana na hisia za watu wengine ivyo kupunguza uwezekano wa kuumizwa. Hisia zake kali anaweza kuzitumia katika kujenga urafiki, mahusiano au shughuli za kidiplomasia.
Itaendelea............