Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Majaliwa anazunguka kama waziri mkuu hazunguki kama Raia wa kawaida bado anatumia magari ya Serikali
Sasa hoja iwe kutumia rasilimali za serikali kufanya kampeni za kisiasa, Hoja siyo eti kwa kuwa ni mgombea ubunge wa Ruangwa basi eti hana haki ya kuzunguuka nchi nzima kumpigia kampeni mgombea mwingine wa chama chake!.
Mbona wagombea ubunge wa Chadema wanasaidiana kampeni kwenye majimbo yao?, kwa mfano Msigwa alienda Kilosa kumpigia kampeni Profesa J?
Mbona Zitto anazunguuka nchi nzima kuwapigia kampeni wagombea wa chama chake?
Hoja ya Lissu katika hili suala haina mashiko, labda aijenge juu ya kutumia rasilimali za serikali kupiga kampeni, lakini si kwa mtu individually kupiga kampeni kwa niaba ya mtu mwingine mahali popote nchini!