Uchaguzi 2020 Tarime: Tundu Lissu ampiga marufuku Kassim Majaliwa kufanya kampeni, Yadaiwa anavunja maadili ya uchaguzi

Majaliwa anazunguka kama waziri mkuu hazunguki kama Raia wa kawaida bado anatumia magari ya Serikali

Sasa hoja iwe kutumia rasilimali za serikali kufanya kampeni za kisiasa, Hoja siyo eti kwa kuwa ni mgombea ubunge wa Ruangwa basi eti hana haki ya kuzunguuka nchi nzima kumpigia kampeni mgombea mwingine wa chama chake!.

Mbona wagombea ubunge wa Chadema wanasaidiana kampeni kwenye majimbo yao?, kwa mfano Msigwa alienda Kilosa kumpigia kampeni Profesa J?

Mbona Zitto anazunguuka nchi nzima kuwapigia kampeni wagombea wa chama chake?

Hoja ya Lissu katika hili suala haina mashiko, labda aijenge juu ya kutumia rasilimali za serikali kupiga kampeni, lakini si kwa mtu individually kupiga kampeni kwa niaba ya mtu mwingine mahali popote nchini!
 
Hebu weka hapa hizo kanuni za tume!

Nyie kila kitu anachosema Lisu mnabeba kama kilivyo...

Huyo jamaa yenu pamoja na kujiona anajua kila kitu lakini ndio atapata kura kidogo zaidi kuliko wagombea wote waliowahi kuhombea chadema
 
Huyu jamaa ni noma said ya Corona
 
Kwenye hili ni lazima chakubanga polepole ataitisha press leoleo🤔🤔

Maendeleo yana chama ila udikteta hauna chama
 
CCM yapo kama matahira,huenda hata halijui kuwa sheria hairuhusu kumfanyia Magufuli kampeni!
 
Huu ni mwiba mpya kwa mgombea wa chama kimoja cha siasa. Daktari amemshauri kusimama kwa dakika zisizozidi 20 akiwa anafanya kampeni. Sasa wale right men wake wakipigwa spana sijui atafanyaje kampeni.
Arrested by cardiac arrest!
 
Hebu weka hapa hizo kanuni za tume!

Nyie kila kitu anachosema Lisu mnabeba kama kilivyo...

Huyo jamaa yenu pamoja na kujiona anajua kila kitu lakini ndio atapata kura kidogo zaidi kuliko wagombea wote waliowahi kuhombea chadema
Majaliwa alipokuwa Mwanza alito maagizo kwa taasisi za serikali juu ya kivuko tena akiwa kwenye jukwaa la kampeni

Majaliwa alitoa maagizo kwa wauguzi na hospitali zinazotoza wamama wajawazito tena akiwa kwenye jukwaa la kampeni

Alafu kanuni za Tume zinasema hivi👇
 
sawa kabisa, ni ngumu sana kwa mbongo kupatia English kwa 100% everytime , kuna mahali lazima tunafeli! ni bora tusikosoane , tumuachie malkia lugha yake! kawaida yao kina Rooney adjective hufuatiwa na noun, mf the fastest car, the strongest man, the richest boy, the ugliest girl, the poorest woman, etc
 
Wajinga nyie, mikutano ya kampeni inapangiwa ratiba jee Majaliwa anapangiwa ratiba na NEC?
Hivi kama kila mjumbe wa kamati kuu wa kila chama atafanya mikutano jee haitakuwa fujo hiyo?
Msipende kutetea ujinga!
Kama anajisikia kupiga kampeni aongozane na mgombea wao
 
Kama Mawaziri wengine bado ni Mawaziri vipi PM sio? Au Mkuu, unaamini Mawaziri hawapo sababu bunge limevunjwa.
Hilo la PM kuzunguka nchi nzima sina uhakika na uhalali wake.
 
Aisee mh lissu ni kiboko, kujua sheria ni raha sana
 
Majaliwa anatembelea ratiba ya wagombea ubunge, sio ya Rais, ata Mwanri, Pinda na nassari wanatumia ratiba za wagombea ubunge.
 
Soma Katiba; bunge kuvunjwa haina maana kuwa serikali nayo inakufa! Je una maana kuwa leo hii tukishambuliwa na nchi jirani hatutajibu mapigo kwa vile bunge limevunjwa?
Kwa hyo anazunguka PM kama serkali au kama mgombea na kwanini anatoa ahadi kwa wananchi wakati yy hayupo jimboni kwake.

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…