KipofuNyani haoni kendezake, mbowe si ni kub ana hadhi ya waziri mkuu kivuli
Majaliwa anafanya KAZI anazotakiwa kufanya wakati wote, swala ilibidi kumhoji alikua wapi siku zote kufanya KAZI zake kwa umahiri huu mpaka anasubiria kipindi cha kampeini!?..Sio sahihi
Soma katiba
Spika bado ni Job Ndugai
Naibu spika bado ni Betina atulie akson
Waziri mkuu ni majaliwa
Mawaziri na manaibu waziri bado wapo kwenye nafasi zao hadi atakapo apishwa rais mpya.
Muwe mnasoma soma basi, msiwe wavivu kama maccm
Hakuna popote ambapo Kasim Majaliwa amejitambulisha Kama waziri mkuu hata media hazimtaji kwa cheo chake zinamtaja kwa cheo Cha chama yani ni mjumbe wa kamati kuu kwa hyo tusikaririshwe vinginevyo angetuambia ni kanuni ipi ya Tume iliyovunjwa ili tuwadai nao Tume waje kutoa ufafanuzi juu ya hili
Huyu mtu wa ajabu kweli; akiwa Musoma amezusha uwongo kuwa wakurugenzi wameitwa Dodoma kupewa maagizo na Magufuli: uongo mkubwa! Sasa leo leo anatamka sheria isiyokuwepo kabisa; yaani ameanza anaonyesha kuwa ni mbabaishaji. Sheria ya uchaguzi inayoruhusu wagombewa kufanya kampeini inasema hivi.
View attachment 1583100
hakuna sehemu inasema kuwa Waziri Mkuu hawezi kuwa agent wa mgombea urais kwenye kampeini.
[/QUOTE
CCM yapo kama matahira,huenda hata halijui kuwa sheria hairuhusu kumfanyia Magufuli kampeni!
Sio tuu wajumbe wa NEC ata wewe Leo hii ukiamua kumfanyia kampeini Hashim Rungwe nchi nzima unaweza Fanya hivyo, Nassari na wasanii wanafanya kampeini bila tatizo lolote, unachotakiwa kufanya ni kuomba ratiba za wagombea udiwani, ubunge au urais na kuhudhuria mikutano Yao na kuwaombea Kura..kama anavyofanya Majaliwa kuhudhuria mikutano ya kampeini ya wabunge na madiwani na kuwaombea Kura wao na Mwenyekiti wao WA Taifa... SIMPLE SANA.Uko sahihi mkuu,hivi huu ni uchaguzi wa ndani ya ccm au ni uchaguzi wa vyama vingi??Eti mjumbe wa NEC kwa hiyo wajumbe wa kamati kuu ya Chadema nao wazunguke nchi nzima kumpigia kampeni Lissu??Kumbe yote waliyofanya kwa miaka mitano na Boss wake wanaona watu hawajawaelewa MLIYEKUWA HAMUMUTAKI KAJA NI YEYE YULEE ALIEONJA KIFO. Hangaikeni nae.
Unatupia vifungu badala ya kutafsiri vifungu?Unaelewa kuwa sheria ni tafsiri na wala siyo vifungu?Wewe ni MATAGA?
Kwanini washirikeshe watumishi watumishi wa serikali kila anapopita!???hii haijakaa sawa kabisaOtherwise Kama anatumia mwamvuli wa uwaziri mkuu. Ila Kama anatumia mwamvuli wa kada na mjumbe wa kamati kuu ya ccm Sheria Wala maadili ya tume hayambani hata kidogo. Endapo anajiamini Hana haja ya kampeni Jimboni kwake Basi habanwi kumwombea kura magufuli popote Tanzania.
Hii ni mada nyingine. Anzishia Uzi wake tutaijadili hukoKwanini washirikeshe watumishi watumishi wa serikali kila anapopita!???hii haijakaa sawa kabisa
Lisu ni mweu Amesahau walivyokuwa wanazunguka na ndege huku Mbowe mkoa ule Slaa na mkoa mwingine Ndesambulo.27 September 2020
Tarime , Tanzania
Tundu lissu akitubia Tarime akimzungumzia Waziri mkuu Kassim Majaliwa kumfanyia kampeni Magufuli kinyume na Maadili ya Sheria ya Uchaguzi inavyomkataza
Tume ya Uchaguzi imehojiwa na Tundu Lissu kwanini haijachukua hatua dhidi ya waziri mkuu wa Tanzania kukiuka maaadili ya Sheria ya Uchaguzi kwa kuzunguka nchi nzima kumfanyia kampeni mgombea wa urais John Magufuli kinyume na taratibu, kanuni na sheria ya maadili ya Uchaguzi.
Kassim Majaliwa ni Mgombea ubunge wa Ruangwa na kwa sheria ya maadili ya uchaguzi sehemu pekee anayoweza kumpigia kampeni mgombea wa urais John Magufuli ni katika eneo jimbo la Ruangwa mkoani Lindi tu.
c.c Erythrocyte
Hapa tatizo ni lugha iliyotumika
Ndio ameliona leo,majaliwa anazunguka Kama mjumbe wa kamati kuu na anafanya kampeni mjumbe na ratiba yake ipo.Uchaguzi una kanuni na maadili ya uchaguzi,ili twende sawa weka kanuni au sheria za uchaguzi hapa ili tujue anabanwa au habanwi, je majaliwa ratiba zake zinapangwa na nani?
Yeye ndio kabisa alikua abanduki mgongoni Kwa lowassa..nilikutana nao Mwanza airport kambebea lowassa briefcase yake wakielekea Kagera kwenye kampeini, alikua anahutubia mikutano yote ya lowassa mpaka wanamaliza muda na kumwachia mgombea dakika Tano tuu.Lisu ni mweu Amesahau walivyokuwa wanazunguka na ndege huku Mbowe mkoa ule Slaa na mkoa mwingine Ndesambulo.
Lisu ni mwanasheria wa kwenye magazeti tu na mitandaoni ila hakuna kitu aliwahi kuongea kikaleta maana.
aibu aibu aibu, MEKO kachanganyikiwa anaokoteza wa kumsemea, wanavunja sheria na hakuna wa kuwagusa.Mgombea Urais kupitia CHADEMA, Tundu Lissu amemuonya Kassim Majaliwa kwa kitendo chake cha kufanya kampeni za Urais kote anakopita , kwa vile kitendo hicho ni kukiuka maadili ya uchaguzi .
Kwa mujibu wa Lissu, Waziri Mkuu Kikatiba hatakiwi kumpiga kampeni mgombea Urais wa chama chake nje ya jimbo lake la uchaguzi ambalo ni Ruangwa tu na ameonya kwamba NEC isipochukua hatua kwenye hili basi itajisimika rasmi kuwa TUMECCM .
Je, Wanasheria mliopo hapa JF hili jambo limekaaje?
we ni mmoja ya mambumbu ya ccm kub ni sawa na waziri mkuu kwa katiba ipi?Nyani haoni kendezake, mbowe si ni kub ana hadhi ya waziri mkuu kivuli
Kwani kuna vitu gani anavyoviongea vya kipekee sana he is just an average lawyer, ila kwa vilaza kama nyie ndio mnamuona kuna la maana analolifanya.Uwezo wako wa kumuelewa ni mdogo sana ndio maana vitu anavyoongea havileti maana kwako,ni kama vile kujaribu kuhamishia maji ya bahari kwenye dimbwi.
Kwani umemwona Mbowe akizunguka nje ya jimbo lake kumpigia Lissu kampeni?Nyani haoni kendezake, mbowe si ni kub ana hadhi ya waziri mkuu kivuli
Sheria hazisemi hivyo bwashweeKwenye hili sidhani kama Lissu yuko sahihi.
Godbless Lema alikuwepo kwenye uzinduzi wa kampeni za Lissu Dar na alimpigia kampeni wakati ni mgombea Arusha.
Lakini, Kassim Majaliwa bado ni mtanzania, kwa mujibu wa katiba ya nchi ana haki ya kwenda mahali popote nchini.
Na kwa mujibu wa katiba ya nchi Kassim Majaliwa ana haki ya kufanya kazi ya kisiasa aliyotumwa na chama chake kwa sababu chama chake ni chama halali kilichosajiliwa nchini.
Kazi ya kuomba kura ni kazi ya wanachama wote, siyo wagombea peke yao!. It is not about individuals, it is about the party
Miaka michache iliyopita Chadema walikuwa wakilalamika kuzuiwa kufanya siasa nchi nzima, yaani mbunge wa Jimbo X kushiriki siasa za Jimbo Y, Leo Lissu anakubaliana na katazo lilelile la Magufuli ambalo walilipinga kipindi kile?
Labda Lissu anukuu vifungu vya sheria tujionee otherwise hoja yake hii naona haina mashiko