Uchaguzi 2020 Tarime: Tundu Lissu ampiga marufuku Kassim Majaliwa kufanya kampeni, Yadaiwa anavunja maadili ya uchaguzi

Uchaguzi 2020 Tarime: Tundu Lissu ampiga marufuku Kassim Majaliwa kufanya kampeni, Yadaiwa anavunja maadili ya uchaguzi

Utawala huu wa awamu ya tano awamu ya penda penda kesi kesi kuwabambikia kesi wapinzani ni utawala usiofuata Sheria na katiba bali unafanya kazi kwa mjibu wa zidumu fikra zisizo sahihi za mtukufu mwenyekiti wa CCM
 
Mgombea Urais kupitia Chadema Mh Tundu Lissu amemuonya Kasimu Majaliwa kwa kitendo chake cha kufanya kampeni za Urais kote anakopita , kwa vile kitendo hicho ni kukiuka maadili ya uchaguzi...


Huyu mtu wa ajabu kweli; akiwa Musoma amezusha uwongo kuwa wakurugenzi wameitwa Dodoma kupewa maagizo na Magufuli: uongo mkubwa! Sasa leo leo anatamka sheria isiyokuwepo kabisa; yaani ameanza anaonyesha kuwa ni mbabaishaji. Sheria ya uchaguzi inayoruhusu wagombewa kufanya kampeini inasema hivi.

1601243825893.png

Hakuna sehemu inasema kuwa Waziri Mkuu hawezi kuwa agent wa mgombea urais kwenye kampeini.
 
Huyu mtu wa ajabu kweli; akiwa Musoma amezusha uwongo kuwa wakurugenzi wameitwa Dodoma kupewa maagizo na Magufuli: uongo mkubwa! Sasa leo leo anatamka sheria isiyokuwepo kabisa; yaani ameanza anaonyesha kuwa ni mbabaishaji. Sheria ya uchaguzi inayoruhusu wagombewa kufanya kampeini inasema hivi...
Wewe ndiyo wa ajabu kwa kukataa ukweli hakuna uzushi bali alisema mapema ndipo mtukufu magufuli akaamua kuahirisha kuepuka Aibu kubwa
 
Bunge likivunjwa na baraza la mawaziri huvunjwa hapo hapo lakini kwenye utawala huu wa kienyeji wameendelea kuwepo kazini kwa njia haramu za kishetani kinyume cha Sheria na katiba
Soma katiba tena mzee wangu; bunge likivunjwa Baraza la Mawaziri na Ofisi ya Spika wa Bunge wataendelea na kazi hadi hapo Rais mpya na Spika mpya watakapopatikana.

Angalia kuhusu Waziri Mkuu kifungu 51(3)

1601245164212.png

Najua unaweza kukimbilia hicho kifungu 51(3)(e), lakini soma katiba tena uone kina maana gani.

Angalia jisni katiba inavyosema kuhusu mawaziri

1601245003559.png
 
Kwa kuwa ccm ni wavunjaji wa sheria wazoefu najua hawatatii na kimajaliwa kitaendelea kufanya kampeni za urais,
Cha kufanya na sisi ni kumchukua Mchungaji msigwa au Lema nao wapite mtaa kwa mtaa wakimpigia kampeni Tundu Lissu, halafu tusikie fyoko fyoko mnavunja sheria za uchaguzi
Wamemwita wenyeee huko ngoja aende na hizi nondo mbona watabroo tu
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Wewe ndiyo wa ajabu kwa kukataa ukweli hakuna uzushi bali alisema mapema ndipo mtukufu magufuli akaamua kuahirisha kuepuka Aibu kubwa
Hakuna ushahidi wowote; alisemaje mapema bila kutoa ushahidi. Kama kweli rais anataka kukutana na watendaji wa serikali ni sheria gani inayomzuiwa.

Halafu rais haihitajui kukutana na wakurugnezi kwani anaweza kutoa maagizo hayo kwa waziri wa tamisemi ndiye akayashughulikai; haya mambo ya kusemasema uwongo ili mradi mtu usikikike na ya hovyo sana kwa mstakhabali wa taifa letu.
 
Ndugu kubali tu lugha ya mama kidogo imekupita pembeni ,unajitutumua tu lakini ukweli ndio huo na kukiri kuwa hujui sio kosa kwani Kiingereza wanaokijua kindakindaki ni wachache na tunajifunza kwa makosa, naamini kwa asilimia mia moja hutaandika tena kama ulivyoandika,kama hujui kitu ukubali kukosolewa au kufundishwa ,hii ni lugha na sio siasa ambayo unageuza maneno kumridhisha Mbowe,unaambiwa umekosea wewe unarukia kwa mwingine,kama hujui,hujui tu na kama unajua unajua tu.
Msalimie Mwakyembe , mwambie sisi Chadema tumefurahishwa sana wapambe wake wanavyoibomoa ccm
 
Toka maktaba video:
23 September 2020
Mwanza, Tanzani

Waziri mkuu akiwa Mwanza kumpigia kampeni mgombea John Magufuli wa CCM Mpya

MJUMBE wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, na ambaye ni Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa, ameendelea na kampeni za kukinadi chama chake na kumuombea kura mgombea wao wa urais, Dkt John Pombe Magufuli..

shukrani mkuu
 
Kwenye hili sidhani kama Lissu yuko sahihi.

Godbless Lema alikuwepo kwenye uzinduzi wa kampeni za Lissu Dar na alimpigia kampeni wakati ni mgombea Arusha...
Huyo anajua anachokizungumza na sidhani kama aliongea bila kujiridhisha.Wacha tusubiri ufafanuzi maana hili haliwezi kupita hivi hivi.

Mikutano ya kisiasa ni tofauti na kampeni za uchaguzi zinazoongozwa na sheria na kanuni za uchaguzi.
 
Mazoea waliyokuwa wanapata CCM ya zamani katika chaguzi zilizopita kujifanyia mambo bila kuzingatia sheria ya Maadili ya Uchaguzi Mkuu, CCM Mpya 2020 wayasahau maana mgombea wetu Tundu Lissu na sisi wapiga kura wenye uelewa mkubwa wa elimu ya uraia ni kubabana nayo CCM Mpya kuwazuia kutumia mazoea ya kufanya mambo shagalabaga mpaka kieleweke Oktoba 28 2020
 
Kwamba Lissu ndiye peke yake anajua tafsiri ya sheria? Kama nawe unaamini hivyo iweje ahamasishe wapiga kura kuingia barabarani iwapo hatatangazwa mshindi?

Akili za kinyumbu tu.
Kwani kuingia barabarani ni wapi imeandikw kama ni kosa,basi magari yasingekuwa yanaingia barabarani
 
Hoja sio uwaziri mkuu bali hoja ni kumpigia kampeni mgombea uraisi wa CCM nje ya Jimbo lake.
Katiba na sheria za uchaguzi hazimzuii; na wala hakuna kipengele chochote kinacholimit watu kufanya kampeini za uraisi katika majimbo yao tu. Watu wanaendeshwa na hisia za uwongo tu bila kusoma sheria na katiba inasemaje. halafu Lisu anajua kuwatumia vizuri watu hao ambao wao ni fuata upepeo tu; anawalisha uwongo wao wanameza tu
 
27 September 2020
Tarime , Tanzania

Tundu lissu akitubia Tarime akimzungumzia Waziri mkuu Kassim Majaliwa kumfanyia kampeni Magufuli kinyume na Maadili ya Sheria ya Uchaguzi inavyomkataza



Tume ya Uchaguzi imehojiwa na Tundu Lissu kwanini haijachukua hatua dhidi ya waziri mkuu wa Tanzania kukiuka maaadili ya Sheria ya Uchaguzi kwa kuzunguka nchi nzima kumfanyia kampeni mgombea wa urais John Magufuli kinyume na taratibu, kanuni na sheria ya maadili ya Uchaguzi.

Kassim Majaliwa ni Mgombea ubunge wa Ruangwa na kwa sheria ya maadili ya uchaguzi sehemu pekee anayoweza kumpigia kampeni mgombea wa urais John Magufuli ni katika eneo jimbo la Ruangwa mkoani Lindi tu.
c.c Erythrocyte
Key word CONSTITUENCY = Jimbo la Uchaguzi. Hivyo ni sahihi na kweli Kassim Majaliwa ukomo wake ni jimboni. Hakuna jimbo linalojulikana kama Taifa.

Hivyo mgombea John Magufuli siyo mgombea wa jimbo lolote la uchaguzi ndani ya Tanzania na hawezi kumteua mtu kumuwakilisha kumfanyia kampeni ya urais.

Maana yake waziri Mkuu, mawaziri, wakuu wa mikoa , wilaya hawaruhusiwi kumfanyia kampeni ya Urais John Magufuli .

Wakuu wa mikoa na wilaya walioingia kuomba ubunge waliachia nyadhifa zao ili washiriki kugombea ubunge jimboni.

Waziri Mkuu yeye anaruhusiwa tu kufanya kampeni za kisiasa ktk jimbo lake tu la Ruangwa alikoombea ubunge na huko Ruangwa ndipo pekee anaweza kumnadi mgombea wa urais John Magufuli
 
Kwamba Lissu ndiye peke yake anajua tafsiri ya sheria? Kama nawe unaamini hivyo iweje ahamasishe wapiga kura kuingia barabarani iwapo hatatangazwa mshindi?

Akili za kinyumbu tu.
Hivi akili zenu zimefikia mahali hata lililo semwa mchana peupe hamuelewi? Nani kasema hivyo? Lissu kasema AKISHINDA KIHALALI na kisha ASITANGAZWE ndio patachimbika! Mnaogopa nini kauli hiyo? Kwani ndio mpango wenu kuwa hata akishinda hamumtangazi?

Lissu kasema wazi kabisa, kura zake zisipotosha kihalali hana shida maana ndio demokrasi nyie mnageuza maneno!
Hapo mnatia mashaka makubwa!
 
Hakuna kiingereza cha "Lissu The Greatest", ni "Lissu The Great", ukiandika Lissu The Greatest lazima umalizie na sifa yake yoyote. Mfano ungeandika: "Lissu The Greatest Politician". Au "Lissu The Greatest Lawyer"
Kila siku mnakandia watu hawajui kiingereza kumbe na nyie Grammar ni ZERO.
Mkuu umenikuna kisawasawa. Wa bongo wajuaji. Ukimwambia hapo umekosea au improve kidogo wanakukejel kwani hujaelewa?! Badala wajifunze.
Binafsi hapo umenifunza kisawasawa na nimeelewa
 
Back
Top Bottom