Tariq Kipemba amewakosea nini wanadamu mpaka wameamua kumpa adhabu kali namna hii?

Tariq Kipemba amewakosea nini wanadamu mpaka wameamua kumpa adhabu kali namna hii?

Expensive life

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2020
Posts
2,971
Reaction score
9,437
Nimeiona hii habari kupitia Millard ayo nikaona ni vyema niilete humu jamvini huenda akapata chochote.

Kijana Tariq Kipemba amemwagiwa kitu kinachohisika kuwa ni tindikali huko mkoani Kilimanjaro wakati akiwa katika matembezi ya kawaida.

Tukio hili limempa majeraha makali mwilini mwake na kumpelekea kupoteza uwezo wa kuona.

Kijana Tariq bado anaendelea kupatiwa matibabu katika hospital ya KCMC mkoani Kilimanjaro, kutoka na hali yake kuzidi kuwa mbaya, familia imeshauriwa ni vyema wakampeleka kijana wao India kwa matibabu zaidi.

Kutokana na gharama za matibabu za kwenda India kuwa kubwa familia imeomba wasamaria wema waweze kuwasaidia kwani wao wameshindwa kuzimudu gharama hizo. Ni zaidi ya milion 30 zinaitajika kwa ajili ya matibabu.

Kama unachochote unaweza kumsaidia Tariq kupitia namba hizi, 0764510774 Jina Tariq kipemba au kupitia account number equity bank 3012111594790.

Screenshot_20220505-092041.jpg
 
Haya ya wachaga na visa vya kidwanzi tu


USSR
Acha upumbavu wako,zee Zima hadi leo 21st century bado unaongelea ukabila, mimi ni mndendeule na nipo huku lingusenguse, huyu aliyepatwa na janga hili ni binadamu mwenzangu, kwangu sio mchaga..halafu unakwenda nyumba za ibada na kuomba wakati umejaa ushetani mkubwa, sometime learn to shut up
 
Ukimsikiliza mwenyewe kwenye hizo onlinetv anasema ni jamaa yake jirani walikuwa haziivi na hawasemeshani na akasema atamlaza kitandani miaka ...sababu wanazijua wao wenyewe Kama ni dhuluma etc

Waebrania 12:14-15
Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, .....
15 Angalieni sana mtu ye yote asishindwe kupata neema ya Mungu, na muwe waangalifu pasizuke chuki ambayo, kama mmea wenye sumu, inaweza kukua ikaleta matatizo na kuwachafua wengi
 
Ni kweli jamaa hali yake ni mbaya....nimewah kumhudumiia yupo pale wodi ya macho ana kama miezi mitatu wodini.
Vijana tujichunge sana na zaidi tumsaidie bila kujali kipi amefanya, kama mungu ni mwingi wa rehema na huruma sisi ni akina nani?
Nilifikiri limetokea juzi kumbe miezi mitatu! Rais anakwenda kubembea Marekani, raia kupelekwa India haiwezekani!
 
Back
Top Bottom