Analyse
JF-Expert Member
- Jan 19, 2014
- 17,637
- 47,413
Binafsi simfahamu na sikuwahi kusikia habari yake before hujampost. Ila naomba niwe general tu katika maoni yangu bila kuyaelekeza kwake. Ktk kila tukio, Kuna hidden story behind. Sisi wanadamu tukiwa na afya njema, tunakuwa na dharau Sana, na hatujali maumivu ya wengine. Ni jambo la kawaida mtu kukudhulumu alaf akakuletea utemi. Ni kawaida mtu kutembea na mke wa mtu au kuchukua demu wa mtu alaf akaenda kutangaza as if ni jambo zuri.Nimeiona hii habari kupitia Millard ayo nikaona ni vyema niilete humu jamvini huenda akapata chochote.
Kijana Tariq Kipemba amemwagiwa kitu kinachohisika kuwa ni tindikali huko mkoani Kilimanjaro wakati akiwa katika matembezi ya kawaida.
Tukio hili limempa majeraha makali mwilini mwake na kumpelekea kupoteza uwezo wa kuona.
Kijana Tariq bado anaendelea kupatiwa matibabu katika hospital ya KCMC mkoani Kilimanjaro, kutoka na hali yake kuzidi kuwa mbaya, familia imeshauriwa ni vyema wakampeleka kijana wao India kwa matibabu zaidi.
Kutokana na gharama za matibabu za kwenda India kuwa kubwa familia imeomba wasamaria wema waweze kuwasaidia kwani wao wameshindwa kuzimudu gharama hizo. Ni zaidi ya milion 30 zinaitajika kwa ajili ya matibabu.
Kama unachochote unaweza kumsaidia Tariq kupitia namba hizi, 0764510774 Jina Tariq kipemba au kupitia account number equity bank 3012111594790.
View attachment 2212157
Kipindi hayo yote yanatokea, wakishauriwa huwa wanashupaza shingo. In a real sense, ni ngumu mtu kuja kukudhuru bila sababu. Anyway, pole Sana kwake.