TARURA na TANROADS yale matuta pale kigamboni mnadani yanaumiza sana! Tunaomba yaboreshwe au muweke moja kubwa

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
Kwa nia njema! Tarula/ Tanroad mmeweka matuta ili kupunguza speed!

Lakini aina ya matuta mliyotumia ni mabaya sana na yanaharibu vyombo vya moto!

Pia mbali na kuharibu vyombo vya moto yanatikisa mwili hadi ubongo!

Sasa kwa vile njia hiyo pia inaelekea hospital! Ikipitisha wagonjwa na wenye mishono mikubwa kwa ambulance!

Tunaomba matuta yale yaboreshwe angalau yawe katika mtindo wa tuta moja kubwa (humps) ili chombo cha moto kipite polepole pasipo mtikisiko kama ilivyo sasa!

Aina ya matuta yaliyopo sasa siyo rafiki kabisa kwa usalama wa vyombo vya moto (yanavipepeta vyombo vya moto kiasi cha kuleta uharibifu wa baadhi ya mali).

Wekeni matuta makubwa wala haitaathili lengo la kupunguza speed!
 
Hivyo vituta vidogo vidogo huwa vinakera sana sasa sijui ni bajeti ama kitu gani huwa sielew

Sent using Jamii Forums mobile app
Sizani kama ni bajeji maana hivyo vituta ukiambiwa bajeti iliyotumika utazimia!
Tuwaombe tu wayaboreshe liwe kubwa moja kuliko hivyo vingi vidogo
 
Sometimes unajikuta unakufuru na kuhoji uwezo wa kufikiria wa hawa watu. Matuta yako less than 50m from the round about, nani atapita na speed kubwa kuzunguka round about? Sehemu ambayo ukiikaribia automatically unapunguza mwendo halafu unaweka matuta. Hawana akili.
 
Kwa nia njema! Tarula/ Tanroad mmeweka matuta ili kupunguza speed!
Lakini aina ya matuta mliyotumia ni mabaya sana na yanaharibu vyombo vya moto...
JPM aliliona hili na akalitolea maagizo lakini hakukuwa na sheria inayoelekeza inabidi tusubiri matamko mengine kuondoa hii kero
 
Kwa nia njema! Tarula/ Tanroad mmeweka matuta ili kupunguza speed!
Lakini aina ya matuta mliyotumia ni mabaya sana na yanaharibu vyombo vya moto!

Pia mbali na kuharibu vyombo vya moto yanatikisa mwili hadi ubongo!
Sasa kwa vile njia hiyo pia inaelekea hospital! Ikipitisha wagonjwa na wenye mishono mikubwa kwa ambulance!

Tunaomba matuta yale yaboreshwe angalau yawe katika mtindo wa tuta moja kubwa (humps) ili chombo cha moto kipite polepole pasipo mtikisiko kama ilivyo sasa!

Aina ya matuta yaliyopo sasa siyo rafiki kabisa kwa usalama wa vyombo vya moto (yanavipepeta vyombo vya moto kiasi cha kuleta uharibifu wa baadhi ya mali)

Wekeni matuta makubwa wala haitaathili lengo la kupunguza speed!
Ma engineer wa kibongo shida tupu! Ile barabara ya kutoka Darajani kwenda ferry au kibada,inahitaji taa za barabarani,na wala siyo hayo matuta ya Rasta za Bob mlioweka! Toweni Mara moja kabla sijawasemea kwa Mama!!!
 
JPM aliliona hili na akalitolea maagizo lakini hakukuwa na sheria inayoelekeza inabidi tusubiri matamko mengine kuondoa hii kero
Harafu ajabu wametumia pesa nyingi kinoma kuweka huo ushubwada!
 
Ma engineer wa kibongo shida tupu! Ile barabara ya kutoka Darajani kwenda ferry au kibada,inahitaji taa za barabarani,na wala siyo hayo matuta ya Rasta za Bob mlioweka! Toweni Mara moja kabla sijawasemea kwa Mama!!!
Ndo wataalam wetu wanakaa ofisini pasipo kwenda site
 
Ma engineer wa kibongo shida tupu! Ile barabara ya kutoka Darajani kwenda ferry au kibada,inahitaji taa za barabarani,na wala siyo hayo matuta ya Rasta za Bob mlioweka! Toweni Mara moja kabla sijawasemea kwa Mama!!!
Taa hapana,round about inakidhi. Hayo matuta hayahitajiki ni uharibifu wa magari na barabara yenyewe.
 
Week iliyoisha yalisababisha Ajali magari matatu yaligongana jioni.

Halafu ujinga ni kuwa hizo Rasta zilikuwepo tayari,

Hizo pesa wangefanya mambo mengine tu.
 
Aina ya matuta waliyoweka ni hatari sana wamefanya kwa komoa pasipo kutumia akili
 
Harafu ajabu wametumia pesa nyingi kinoma kuweka huo ushubwada!
Wana stress za tozo wanaamini maneno ya Madilu kuwa sisi wananchi ndo tulioandamana kuiomba, wanadhani wanatukomoa
 
Wanaotengeneza matuta wanatakiwa waende TBS kuuliza waweke matuta gani yenye viwango. Maana unaweza kuwa na gari lililopishwa na TBS kwa ubora lkn likashindwa kupita kwenye barabara za TARURA NA TANROAD. Hapo huwa nashindwa kuelewa kama watu wanafanya kazi kwenye nchi moja
 
Wanajiwekeaga tu bila hata vipimo
 
Wanajiwekeaga tu bila hata vipimo
Ukiona hivyo wamesha aagiza ma contena ya Shockup za Magari yenu, yaani kila baada ya miezi mitatu lazima mbadilishe vipuli vya chini ya gari zenu!!!
 
dawa ya madereva vichaa wa hii nchi ni kuweka matuta tuu kila mahali ili ajali zipungue, wengine hata zebra hawazingatii, ilitakiwa mita 5 kabla ya kufikia zebra zipigwe tuta kama za viazi daadeki
 
Back
Top Bottom