TARURA na TANROADS yale matuta pale kigamboni mnadani yanaumiza sana! Tunaomba yaboreshwe au muweke moja kubwa

TARURA na TANROADS yale matuta pale kigamboni mnadani yanaumiza sana! Tunaomba yaboreshwe au muweke moja kubwa

Kwa weledi wako Naona hujakosea, ila Kumbuka Kuna standard zinazozingatiwa katika ujenzi WA Kitu Cha public Kwa ajili ya usalama WA public!! Pia kuweka Kitu ambacho kitasababisha madhara zaidi kuliko kuboresha ni Makosa makubwa!! Unamkinga mvukaji (kama ni Kweli) unamuua dereva na abiria WA usafiri mwingine)) Kama bodaboda, hii Haijakaa sawa
Ndo hapo sasa
 
Mtanzania uataraabu zero

Mbongo mpaka awake matuta barabarani asipowekewa
Huo mwendo akatao pita hapo
Kama kichaaa
Narudia tena,mbongo ustarabu wa uendeshaji ni zeroooo

Ova
Basi njia nzima ziwe matuta mwanzo mwisho!!
 
Na nyie waendesha magari,kwann mpaka muwekewe matuta
Mbongo pekee yake anawekewa matuta barabarani...maana hata akiwekewa kibao cha speed ndogo
Awe anapita hapo bado atakuwa anapita na speed 100
Wabongo ustarabu zeroooooo
Kwenye kila kitu

Ova
Si ndiyo maana tukaweka traffic wasimamie madereva wanaovunja Sheria barabarani!? Sasa Kama ma traffic wenyewe wameamua kuwa Marafiki na madereva Wazembe kwa kupeana kitu kidogo ili Maisha yaendee,hiyo ni shauri yao! ila umsituazibu na sisi madereva wafuata Sheria za barabarani kwa kutuwekea hiyo mituta utazani magogo ya tanesco!!!
 
Na kweli Yale siyo matuta ni magogo
 
Kweli Yale matuta sio Ila nikiangalia akili za Madereva wa magari na Bodaboda naishia kusema waongeze matuta zaidi

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
Kwa hiyo wwe unaamini madereva wote barabarani ni wavunja Sheria!? Hakuna hata madereva wachache wanaofuata Sheria!? Je hao wanaofuata Sheria kwa nini nao wahukumiwe kwenye azabu ya matuta!!??
 
madereva wa kibongo wakiwekewa vituta vidogo wanapita shwaaa, gari linatetetema triii, bodaboda ndio usisema mpaka wagongwe watu ndio tuweke matuta?
Nioneshe mtu anaepita na 100 kwenye tuta kubwa liliosanisifa vizuri standard!
 
Kwa hiyo wwe unaamini madereva wote barabarani ni wavunja Sheria!? Hakuna hata madereva wachache wanaofuata Sheria!? Je hao wanaofuata Sheria kwa nini nao wahukumiwe kwenye azabu ya matuta!!??
Matuta yamewekwa kwa faida ya watu wote ...km ww unafuata sheria usidhani kila mtu anafuata sheria

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sometimes unajikuta unakufuru na kuhoji uwezo wa kufikiria wa hawa watu. Matuta yako less than 50m from the round about, nani atapita na speed kubwa kuzunguka round about? Sehemu ambayo ukiikaribia automatically unapunguza mwendo halafu unaweka matuta. Hawana akili.
Hapo unakuta hayo maamuzi yametumika kumkomoa dereva m'moja au watatu ambao hupita kwa fujo eneo hilo badala ya kumvizia wamlambe fine kubwa sana ambayo itamuacha na madeni na akili imkae sawa sawa next time afikirie mara mbili mbili kupita kibwege kama hivyo.
 
Ma engineer wa kibongo shida tupu! Ile barabara ya kutoka Darajani kwenda ferry au kibada,inahitaji taa za barabarani,na wala siyo hayo matuta ya Rasta za Bob mlioweka! Toweni Mara moja kabla sijawasemea kwa Mama!!!
Mkipita hapo muwe na chupa ya diesel hata lita moja kwa siku mkimwagia lita 5 especially kipindi hiki cha jua hayo matuta yatayeyuka kama karatasi imekutana na maji.
 
Ukitafakali Yale matuta waliyoweka hayana tofauti na magogo ya mnazi wanayowekaga wasiyo wataalam uswahilini.
Tofauti ni hawa wametumia lami kuweka na uswazi wanatumia magogo ya miti! Lakini hakuna elimu iliyotumika
,,[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Mainjinia wasomi ni wachina pekee waliotoa mataa ubungo wakati wa ujenzi na kuweka mzunguko Foleni ya miaka mingi iliyosumbua Wasomi wetu ikaisha kabla ya kuweka Flyovers. Wengine wote ni p....ndaaaaaaa
 
Mkipita hapo muwe na chupa ya diesel hata lita moja kwa siku mkimwagia lita 5 especially kipindi hiki cha jua hayo matuta yatayeyuka kama karatasi imekutana na maji.
Wataweka tena konki ya zege
 
Kigamboni mji wa kishua hatutaki matuta.

Kwa sababu
Tajiri wa kwanza kuagiza Ferrari atatokea kigamboni.

Sasa ataendesheje na matuta haya !!!
 
Siku yaliyowekwa nilichelewa sana kurudi kama saa saba usiku ndio napita darajani. Ile nafika pale kona ya mwisho wa walami nilipiga zile tuta jidogo nipate ajali na nilikuwa mwendo wa kawaida ti kama 50km/hr. Nilishuka kuangalia nimekanyaga nini nilitukana sana mainjia wetu japo kimya kimya shwain
 
Back
Top Bottom