TARURA nini kinaendelea mpaka deni la maegesho ya gari linaongezeka? Mamlaka itolee ufafanuzi

TARURA nini kinaendelea mpaka deni la maegesho ya gari linaongezeka? Mamlaka itolee ufafanuzi

Cash Generating Unit

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2019
Posts
13,286
Reaction score
39,418
TARURA tunaomba mtolee ufafanuzi kinachoendelea kwenye system zenu nilifikiri ni kwangu tu kumbe ni kilio cha kila mtu. Nilikuwa na deni la 13,000 nikasema ngoja leo niingie nilipe deni lao kufungua app nakuta 83,000 nikashtuka au ni penalty?

Kucheki last payment nimefanya 15/03 sasa hiyo 70,000 imetoka wapi? Ikabidi nimchek jirani yangu naye alikuwa na deni la 4,000 amekuta 72,000 ni kila mtu sijajua wengine huko hali yenu ipoje.

Je, ni system zimecheza? Au ndo upigaji kwa Watanzania? Kumekuwa na ubambikwaji mkubwa sana na hawa TARURA wa barabarani anaweza akakumbakia tu kiasi chochote anachotaka kuweka bila wewe kujua.

Hili limekuwa janga sana kwa wamiliki wa magari. Serikali iliangalie hili jambo kwa kina sana ikiwezekana iangaliwe namna nyingine ya kukusanya huu ushuru. Maisha yamekuwa juu kila kitu sasa hivi, kiukweli kuwa na gari Dar ni mateso.
 
Pole sana.

Kiukweli hii Parking fee imekuwa introduced bila elimu ya kutosha kwa wateja.. Na watanzania bila kukumbushwa huwa tunajisahau sana.

Nadhani TARURA waangalie uwezekano Wa kuweka matangazo Kwenye vyombo vya Habari Mara kwa Mara ili kutukumbusha wateja wao juu ya kulipa haya madeni.
 
Nimesha sahau kama nina deni huko
 
TARURA WAMEANZA KUTOZA FAINI KWA WADENI SUGU WA MATUMIIZI YA MAEGESHO KUANZIA TAREHE 1 MACHI 2022, KAMA UNA GARI NA UNATUMIA MAEGESHO YA SERIKALI LIPA USHURU WA MAEGESHO MAPEMA KUEPUKA FAINI
 
Pole sana.

Kiukweli hii Parking fee imekuwa introduced bila elimu ya kutosha kwa wateja.. Na watanzania bila kukumbushwa huwa tunajisahau sana.

Nadhani TARURA waangalie uwezekano Wa kuweka matangazo Kwenye vyombo vya Habari Mara kwa Mara ili kutukumbusha wateja wao juu ya kulipa haya madeni.
Muda mwingine hili deni, unalikuta tu, ulilipata wapi na lini, haujilikani.
Yaani kama una App ya kuangalie deni inabidi uangalie mara kwa mara.
 
TARURA watu wa hovyo sana,hawajaweka hata namba za Malalamiko ujue unapiga wapi kusaidiwa.
Ila kibaya zaidi wamewaambia wahudumu wao wasitoe Risiti sijui lengo lao ni nini,kwa mfano Mhudumu wao wa Mwembeyanga Temeke kila siku Mashine yake Mbovu haitoi Risiti sasa unajuaje kakuwekea Tsh ngapi na unalipaje hiyo Fee bila Control Number na ukichelewa kulipa ndiyo unakutana na hayo mafaini.
 
IMG_9079.jpg

Wajinga tu hao tuachane nao usilipe
 
Pole sana.

Kiukweli hii Parking fee imekuwa introduced bila elimu ya kutosha kwa wateja.. Na watanzania bila kukumbushwa huwa tunajisahau sana.

Nadhani TARURA waangalie uwezekano Wa kuweka matangazo Kwenye vyombo vya Habari Mara kwa Mara ili kutukumbusha wateja wao juu ya kulipa haya madeni.
huu ni uhuni mie najiandaa kuwadai fidia hawa! nilishawah kwenda ofsn kwao kupeleka madai ya kupigwa picha wakati sikupaki! wakasema watatoa! hawakutoa!

kibaya zaidi ni unaandikiwa bila kuweka karatas na mfumo huu hauleti msg kwenye simu zetu je hawaoni wanaleta wizi na mkanganyiko?

mie kesho naanza nao
 
Hawa tarura watakuwa wanabambika hizi bill Kwa sana!! Mimi huwa nakutana na Hawa madada Wana mashine na huwawezi kutoa risiti, wanajidai vitabu vimekwisha na vivyo wanascan kiwiziwizi au kinyemela bila mhusika kujua
 
mbaya sana! tuwafichue tusiwaache hawa
 
huu ni uhuni mie najiandaa kuwadai fidia hawa! nilishawah kwenda ofsn kwao kupeleka madai ya kupigwa picha wakati sikupaki! wakasema watatoa! hawakutoa!

kibaya zaidi ni unaandikiwa bila kuweka karatas na mfumo huu hauleti msg kwenye simu zetu je hawaoni wanaleta wizi na mkanganyiko?

mie kesho naanza nao
Ndugu huu ni wizi hatari na kuleta mifarakano ya kiwizi, huwezi kudaiwa bila mtu kukupa risiti ya bill, utajuaje!?
 
Mambo ndo kwanzaa yanaanza hii nchi jamani
 
Back
Top Bottom