TARURA nini kinaendelea mpaka deni la maegesho ya gari linaongezeka? Mamlaka itolee ufafanuzi

TARURA nini kinaendelea mpaka deni la maegesho ya gari linaongezeka? Mamlaka itolee ufafanuzi

Nashukuru mtoa uzi nami nimekuta nina deni[emoji23][emoji23]..!! Hii sijui ningeijulia wapi
 

Attachments

  • IMG_3859.jpg
    IMG_3859.jpg
    36 KB · Views: 24
Nimeshtushwa baada ya kukuta nimewekewa fine ya 10,000 baada ya kuchelewa kulipa parking fee ya tar 22/3/2022 ya 500. Ina maana hata mwezi mmoja haujapita tayari fine kubwa hivyo, huo ni Wizi mchana kweupe. Kama Serikali inaweza kuweka fine kubwa hivi je ingekuwa wao wanapochelewesha malipo ya wakandarasi na watoa huduma wao wangeweza kulipa?

Kagua gari lako kuna wizi Mpya umeibuka

Mbona services unavailable ?
 
Kwa kweli hata kama ni penati hii imezidi sana, nawana fanya kama kumtegea mtu hivi kwa nini wasitume ujumbe kumkumbusha mtu deni lake kama wapo vizuri katika system yao? huu ni uharamia uliojificha ndani yake.wajipange vizuri sehemu nyingi wana scan bila hata kuweka recepts utakumbukaje sasa.
 
Kuna mmoja alikula makofi pale millenium tower mtu kaingia ATM hajachukua dk10 kuchek anakuta kawekewa 1,500 alimchapa makofi 2 ya nguvu watu wakajaa ndo kusikia habari hzo.

Waanga ni wengi sana kuanzia kesho ntakua siriazi na hawa forget watu

Acha kushangilia uharifu, kupigana makofi ni udhalilishaji na unapaswa kukemewa.
 
Utakuwa ni ujanja ujanja wa kubambika tozo, nchi hii wanyonge wanaporwa hata akiba ndogo waliyobakiza ili mafisadi yaendelee kusukuma dili zao..........
 
kuna kipindi walikua wana test mfumo wao data sijui walizichukua TRA waka generate madeni kwa magari yote alafu wakasema watafuta hawakufuta ile buku nimekuja kuilipa juzi tu kwasababu nilikua na hela kuchezea la sivyo nisingelipa
 
Tanzania watumiaji wa vyombo vya moto
Wana sulubiwa dah

Ova
 
TARURA tunaomba mtolee ufafanuzi kinachoendelea kwenye system zenu nilifikiri ni kwangu tu kumbe ni kilio cha kila mtu. Nilikua na deni la 13,000 nikasema ngoja leo niingie nilipe deni lao kufungua app nakuta 83,000 nikashtuka au ni penalty?

Kucheki last payment nimefanya 15/03 sasa hio 70,000 imetoka wapi? Ikabid nimchek jiran yangu naye alikua na deni la 4,000 amekuta 72,000 ni kila mtu sijajua wengine huko hali yenu ipoje.

Je ni system zimecheza? Au ndo upigaji kwa Watanzania? Kumekua na ubambikwaji mkubwa sana na hawa TARURA wa barabarani anaweza akakumbakia tu kiasi chochote anachotaka kuweka bila wewe kujua.

Hili limekua janga sana kwa wamiliki wa magari. Serikali iliangalie hili jambo kwa kina sana ikiwezekana iangaliwe namna nyingine ya kukusanya huu ushuru. Maisha yamekua juu kila kitu sahivi, kiukweli kuwa na gari dar ni mateso.

View attachment 2179187
Hizo hapo

Screenshot_20220408-121325.jpg


Screenshot_20220408-121334.jpg


Screenshot_20220408-121339.jpg
 
Hakuna faini asilimia ya asilimia 538% mtu anaweza kutozwa na serikali kwa kisa cha kuchelewa kulipia huduma za kiserikali.
TARURA WAMEANZA KUTOZA FAINI KWA WADENI SUGU WA MATUMIIZI YA MAEGESHO KUANZIA TAREHE 1 MACHI 2022, KAMA UNA GARI NA UNATUMIA MAEGESHO YA SERIKALI LIPA USHURU WA MAEGESHO MAPEMA KUEPUKA FAINI
 
Back
Top Bottom